Utafiti: Unajua mbwa anaweza kupunguza msongo wa mawazo kwa wanaume?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika majaribio mapya ya kisayansi, kwa mara nyingine tena imethibitisha jinsi mbwa wanavyoweza kuelewa hisia za binadamu.
Wanasayansi wamegundua kwamba sasa mbwa wanaweza kukubaini msongo wa mawazo alionao binadamu. Hasa mwanamume kupitia pumzi na chanzo chake.
Wanasayansi walitumia mbwa wanne kufanya utafiti wao. Mbwa hao walikuwa na mafunzo maalumu. Na walichukuliwa kutoka kwa wamiliki wao kwa kujitolea kushiriki katika utafiti huo.
Utafiti huo ulifanyikaje?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbwa hao wanne walitakiwa kuchagua sehemu moja kati ya tatu zilizokuwa na takataka zenye harufu.
Mbwa hao wakatambua kwa usahihi kabisa sampuli ya takataka iliyochukuliwa kutoka kwa mtu ambaye alikuwa na msongo wa mawazo mara 650 katika jaribio lililofanyika mara 700.
Watu 35 waliamua kujitolea kurekodiwa viwango vyao vya msongoi wa mawazo kabla na baada ya kutakiwa kujibu hesabu ngumu. Wote walionyesha kupumua au kutapika kabla au baada ya kuongezeka kwa shinikizo la damu na kasi ya moyo na mishipa.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Queensland huko Belfast wanatumai utafiti wao huo utasaidia kuwafunza mbwa wanaotumiwa katika matibabu ili kupunguza msongo wa mawazo kwa wanaume, kwa mujibu wa makala ya utafiti iliyochapishwa katika jarida la Plus One.
Mbwa hao wanahaha kuijua saikolojiaya binadamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbwa hao wanaleta taswira ya dunia kupitia harufu, wakiwa na uwezo wa kugundua dawa za kulevya, milipuko na baadhi ya saratani, pamoja na magonjwa mengine kama kisukari na Corona.
"Tuna ushahidi mwingi kwamba mbwa wanaweza kutofautisha harufu ya binadamu inayohusishwa na magonjwa na hali fulani, lakini hatuna ushahidi mwingi kwamba wanaweza kutambua tofauti za hali yetu ya kisaikolojia," anasema Clara Wilson, mwandishi mkuu wa utafiti huo.















