Je Kisspetin ni homoni ya aina gani na ni kwanini inaongeza uwezo wa kujamiiana?

Chanzo cha picha, Getty Images
Matokeo ya majaribio ya kimaabara yanaonyesha kuwa homoni ya kisspeptin husaidia kuchochea hamu ya tendo la ngono katika ubongo wa wanaume na wanawake waliokosa hamu hiyo.
Vipimo vya scani vya ubongo wa washiriki wa tafiti zinazohusiana na homoni hii walipokuwa wakitazama video za ngono vilionyesha kwamba homoni hii iliweza kuchochea maeneo muhimu yanayohusika na hamu ya kujamiiana katika ubongo wao.
Watafiti wa Uingereza wanadai kuwa kisspeptin ina uwezo wa kutibu hali ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya kitendo 0cha kijamiiana, tatizo ambalo huwaathiri asilimia 10 ya watu.
Watafiti kutoka Chuo kikuu cha Imperial College London wanasema kuwa vijana wadogo ndio wenye uwezekano zaidi wa kuhisi tatizo wakati hamu yao ya kujamiiana inapoongezeka , tofauti na watu wenye umri mkubwa ( ambao hawaone kupungua kwa hamu yao kama tatizo linalohitaji matibabu).
Watafati wanasema kwamba kuna wale ambao hawajali kuhusu tatizo hili , lakini wakati suala hili linapokusababishia wasi wasi, linaweza kusababisha uharibifu unaoweza kukuathiri vibaya kisaikolojia na kusababisha athari za kijamii.
Peter, sio jina lake halisi, mwenye umri wa miaka 43, alipata tatizo la kuwa nah amu ya chini ya tendo la kujamiiana maisha yake yote wakati alipojitolea kushiriki katika majaribio ya homoni hii.
“Kila mara huwa ninapata sababu ya kutofanya tendo la ngono, mfano huwa ninasema nimechoka sana au nina msongo wa mawaz,” anasema Peter.
"Lakini sikuweza kumwambia mtu mwingine ambaye nilikuwa na mahusiano naye kwasababu sikutaka wakanganye ukosefu wa utashi na kukosa mvuto," aliongeza.
’Kutofurahia"
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kisspeptinni homoni asilia ambayo huchochea kuachiliwa kwa homoni nyingine za uzazi mwilini. Inajukumu muhimu katika kipindi cha kubalehe.
Utafiti wa awali umeuonyesha kuwa inaweza kuchochea mifuko ya mayai ya uzazi ya wanawake(ovaries) kutengeneza mayai, huku ikiboresha hisia katika afya ya wanaume.
Ni mara ya kwanza kwamba homoni hii imefanyiwa vipimo kwa watu wanaumwa ukosefu wa hamu ya kujamiiana, tatizo ambalo limeathiri maisha yao.
“Wanaume na wanawake wenye kiwango cha chini cha hamu ya ngono wanasema wanajipata wakifikiria sana na kukanganyikiwa wanaposhindwa kutekeleza kitendo cha kujamiiana ipasavyo ,” anasema mwandishi mwenza wa utafiti huu Dr. Alexander Komnenos wa Imperial College.
"Kisspeptin hurejesha uwiano asilia, ambao hupunguza hali ya mtu kujilaumu kuhusiana uwezo wake wa hamu ya kujamiiana," anasema Komnenos.
Homoni hii hufanya kazi tofauti na dawa ya kuongeza nguvu za kiume Viagra, inayotibu ukosefu wa kusimama kwa uume kwa kuongeza mtiririko wad amu katika uume.
Tafiti, zilizowahusisha watu 32, wanaume wanaoshiriki ngono ya mume na mke (wenye umri wa kati ya miaka 21 na 52) na wanawake wamnaoshiriki ngono kna wanaume wenye umri wa kati ya miaka 19 hadi 48, ni jaribio la kwanza la homoni ya kisspeptin kufanyika kwa watu wenye matatizo yah amu ya kujamiiana.
Washiriki walipewa kwanza tone la homoni ya kisspeptin, kisha wakapewa matone kadhaa na kuambiwa kuwa ilikuwa ni kisspeptin.
Hisia zao, mienendo yao na shughuli za akili zao walipokuwa wakitazama video za ngono vilifanyiwa tatathmini kwa kutumia kipimo cha scani ya ubongo ya MRI.
Kusimama kwa uume wao pia kulipimwa wakati huo huo.
Peter anasema kuwa uzoefu wa kuchukuliwa kipimo cha scani wakati walipokuwa na hamu ya kujamiiana kilikua cha "ajabu".
Anafurahia kushiriki. Anasema, "Mimi sasa ni baba.Katika kipindi cha wiki moja cha kupata dozi , niliweza kuwa na ngono ya kawaida, ambayo baada ya miezi kadhaa iliweza kuwa na matokeo ya kuzaliwa kwa mtoto."
Hakuna yeyote anayeweza kuthibitisha kuwa ujauzito huu ulihusiana na iwapo Peter alipokea homoni au la, lakini anasema anahisi "kuwa na hamu zaidi ya kufanya ngono sasa ".
Homoni ya kisspeptin imebainika kuboresha shughuli ya maeneo muhimu ya ubongo yanayohusiana na hamu ya kujamiiana kwa wanaume na wanawake kwa pamoja.
Wale ambao walisumbuliwa zaidi na ukosefu wa hamu wameonyesha kuboreka zaidi kwa hali zao katika hilo.
Utafiti unaripoti kuwa ugumu wa uume uliongezeka kwa 56% wakati wanaume walipopewa homoni ya kisspeptin cikilinganishwa na placebo.
"Wengi wao waliona athari chanya katika kipimo cha scani ya MRI , ambacho kwa kawaida sio mazingira mazuri yanayoweza kuamsha hamu ya kujamiiana, kwahiyo athari ilikuwa ni kubwa zaidi walipokuwa katika vitanda vya vyumba vyao," Dr. Komnenos alisema.
Kwa ujumla, wanawake walisema walihisi "kuamka zaidi kwa hamu ya kujamiiana" walipotumia kisspeptin, huku wanaume wakiripoti kuongezeka kwa "raha yakujamiiana".
Waovuti wa wizara ya afya ya Uingereza unasema kuwa kiwango cha chini cha hamu ya ngono ni tatizo la kawaida linalosababishwa na mambo mbali mbali mkiwemo matatizo ya mahusiano, msongo wa mawazo, viwango vya chini vya homoni wakati wa ukomo wa hedhi na mchoko baada ya kujifungua , kushindwa kusimama kwa uume au kukauka kwa uke.
Kutumia aina fulani za dawa, kama vile antidepressants, au kutumia njia fulani za kudhibiti uzazi vinaweza kuathiri hamu ya kujamiiana.
Sababu nyingine ni pamoja na matumizi ya vilevi ya kupindukia, magonjwa ya kudumu kama vile, maradhi ya moyo, kisukari, pamoja na saratani.

Chanzo cha picha, Getty Images
















