Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatano 17.08.2022
Newcastle United imeonyesha nia ya kusajili wachezaji watatu kutoka Chelsea - Muingereza Callum Hudson-Odoi, 21, na Connor Gallagher, 22, na Marekani Christian Pulisic, 23 - na pia wanamtaka mshambuliaji wa Blues Armando Broja, 20, wa Albania. , lakini wanaweza kuchukua mchezaji mmoja tu kwa mkopo kutoka kwa klabu na kuwa na vikwazo vya kifedha kwa idadi ya usajili wa kudumu ambao wanaweza kufanya.(Telegraph - subscription required)
Chelsea itaruhusu mchezaji anayelengwa na Newcastle United Callum Hudson-Odoi kuondoka kwenye klabu, lakini kwa mkopo pekee. Mmiliki mwenza Todd Boehly amemsihi kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 kutolazimisha uhamisho wa kudumu. (Evening Standard - subscription required)
Wesley Fofana wa Leicester City 21, amekubali masharti ya kibinafsi na Chelsea lakini klabu hizo mbili bado hazijamalizana kuhusu ada - huku klabu hiyo ya Stamford Bridge ikikataa kulipa pauni milioni 85 ili kumnunua beki huyo wa kati wa Ufaransa.(Fabrizio Romano)
Chelsea imekubali dili la kumsajili kiungo wa kati wa Italia Cesare Casadei mwenye umri wa miaka 19 kutoka Inter Milan kwa £12.6m pamoja na nyongeza za £4.2m.(Sky Sports)
Atletico Madrid itakuwa tayari kumpa mshambuliaji wa Manchester United ama Mfaransa Antoine Griezmann, 31, au fowadi wa Uhispania Alvaro Morata, 29, katika mabadilishano ya nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37. (Times, via Sun) Hata hivyo, meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone anasema anataka Morata anayelengwa na Manchester United "kuendelea" katika klabu hiyo baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi yao ya kwanza ya La Liga. (Mirror)
Na Morata pia alisema "anafuraha" katika Atletico Madrid na "anataka kuendelea kufanya kazi huko", akiweka shaka zaidi juu ya nia yake ya kuhamia Manchester United. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Real Madrid na Brazil Casemiro, 30, pia analengwa na Manchester United (Marca)
Lakini, kwa mujibu wa vyanzo vya Real Madrid, Casemiro hana nia ya kutaka kuhamia Manchester United na klabu hiyo ya La Liga haijapokea ofa. (Lucas Navarrete)
Barcelona hawana nia ya kumsajili mlinzi wa pembeni wa Ureno Diogo Dalot, 23, kutoka Manchester United kama sehemu ya mkataba ambao unaweza kumfanya kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kwenda upande mwingine wa Old Trafford. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Besiktas ya Uturuki inataka kumsajili Dele Alli wa Everton – iwe kwa mkopo au mkataba wa kudumu. Klabu hiyo ya Ligi ya Premia iko tayari kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 26, kuamua kubadili (Fabrizio Romano)
West Ham wanatumai kukamilisha usajili wa mlinzi wa Paris St Germain wa Ujerumani Thilo Kehrer, 25, kwa wakati wa mechi ya Alhamisi ya Ligi ya Europa Conference dhidi ya Viborg FF baada ya kuafikiana dili la thamani ya euro 12m (£10.1m), pamoja na nyongeza. (Sky Sports)
Sevilla, ambao walikuwa wakishindana na West Ham kumsajili Kehrer, wamekubali ada ya euro 20m (£16.8m) na Bayern Munich kumnunua beki wa kati wa Ufaransa, Tanguy Nianzou, 20. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele, 23, hatahamia klabu ya Serie A Napoli. (Corriere Dello Sport - in Italian)
Mawakili wa fowadi wa Uholanzi Memphis Depay wamekutana na Barcelona kujadili kuhusu kuondoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwenda Juventus, ambako kunatarajiwa siku zijazo. (Sport)
Marseille wanatazamia kutangaza kumsajili kiungo wa kati Mfaransa Sayha Seha, 17, kutoka Estac Troyes licha ya Manchester United kumtaka. (L'Equipe)
Arsenal imemtoa kwa mkopo kipa wa Iceland Runar Alex Runarsson, 27, kwa klabu ya Uturuki ya Alanyaspor. (L'Equipe)
Mshambulizi wa Juventus Lina Hurtig, 26, anakaribia kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Ligi Kuu ya Wanawake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi anatarajiwa kuwasili London siku ya Jumatano kwa ajili ya kumalizana na Arsenal. (Tom Garry)