Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 11.05.2024

g

Chanzo cha picha, Gettu Images

Maelezo ya picha, Jordan Henderson
Iliyochapishwa

Mustakabali wa kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson mwenye umri wa miaka 33 katika klabu ya Ajax umetiwa shaka baada ya timu hiyo ya Uholanzi kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo. (Athletic - subscription required)

Ripoti zinazomuhusisha kiungo wa kati wa Newcastle Bruno Guimaraes na kuhamia Paris Saint-Germain msimu huu sio sahihi na Timu hiyo ya Ufaransa haina nia ya kumsajili Mbrazil huyo. (Mirror)

Meneja Mholanzi Arne Slot anatazamiwa kuhamia katika nyumba ya sasa ya Jurgen Klopp iliyoko Formby atakapomrithi Mjerumani huyo ukufunzi wa Liverpool . (Mirror)

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, atakuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi Real Madrid ikiwa atasaini klabu hiyo baada ya kuondoka Paris Saint-Germain . (RMCsport)

Kuondoka kwa Mbappe kutaokoa PSG €220m (£189m) licha ya mshambuliaji huyo kuondoka kwa uhamisho huru. (Sky Sports)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohamed Amoura

Liverpool wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Algeria mwenye umri wa miaka 24 Mohamed Amoura kutoka Union Saint-Giloise . (TEAMtalk)

Mazungumzo kuhusu mkataba mpya kati ya Barcelona na kiungo wao wa kati Mhispania Marc Casado mwenye umri wa miaka 20 yamekuwa yakiendelea tangu Aprili. (Fabrizio Romano)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hansi Flick

Bayern Munich wameanza mazungumzo na aliyekuwa kocha wao mkuu Hansi Flick kuhusu kurejea kwenye uongozi na kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel. (Sky Germany)

Barca wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa Arsenal na Juventus kwa mkataba na Real Sociedad kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 25. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi