Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 29.04.2024

Iliyochapishwa

Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen ataondoka Napoli msimu huu wa joto, huku Chelsea na PSG zikitarajiwa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Gazetta - kwa Kiitaliano)

Crystal Palace wanahofia kwamba beki wa England mwenye thamani ya pauni milioni 55 Marc Guehi huenda akaondoka msimu huu, huku Manchester United na Arsenal wakimwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Times - usajili unahitajika)

Borussia Dortmund itajaribu kubadilisha mkataba wa mkopo wa winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, kutoka Manchester United kuwa mkataba wa kudumu msimu huu. (Fabrizio Romano)

Liverpool wanajiandaa kupokea dau la hadi pauni milioni 150 kutoka kwa vilabu vya Saudi Arabia kumnunua mshambuliaji wa Misri mwenye umri wa miaka 31 Mohamed Salah. (Football Insider)

Beki wa Uholanzi Lutsharel Geertruida, 23, anaweza kuondoka Feyenoord pamoja na kocha Arne Slot kujiunga na Liverpool baada ya mlinzi huyo kuonekana uwanjani wakati wa mechi ya Jumamosi yao Reds dhidi ya West Ham Jumamosi. (Express)

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski anataka kusalia Barcelona msimu huu wa joto, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kunyatiwa na klabu za Saudi Arabia. (Sport - kwa Kihispania)

Arsenal, Liverpool na Manchester United wanavutiwa na kiungo wa kati wa Brighton raia wa Cameroon Carlos Baleba, 20. (Caught Offside)

Leeds wanataka kumsajili beki wa Liverpool Muingereza Nat Phillips, 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Cardiff. (Mirror, kupitia Yorkshire Post)

Beki wa kati wa Brazil Thiago Silva anataka kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 akihusishwa na Fluminense. (TEAMtalk)

Everton huenda ikalazimika kumuuza beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite mwenye umri wa miaka 21 ili kutii sheria za Usawa wa Fedha michezoni, na hivyo kufungua mlango wa kuhamia Manchester United. (Sun)

Arsenal wameanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na beki wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Gabriel. (Fichajes - kwa Kihispania)

Arsenal na Borussia Dortmund wanavutiwa na kiungo wa kati wa Barcelona Mhispania Brian Farinas mwenye umri wa miaka 18. (Caught Offside)

Blackburn wanataka hadi pauni milioni 20 kumnunua mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Sammie Szmodics, huku Brentford, Luton na Sheffield United wakimwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sun)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi