Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kuporomoka kwa daraja la Morbi: Jinsi eneo la watalii lilivyogeuka kuwa daraja la kifo
Maswali yanaulizwa nchini India baada ya daraja maarufu la miguu kuporomoka, na kuwatumbukiza watembea kwa miguu wengi kwenye mto katika jimbo la magharibi la Gujarat.
Hali ya kutisha katika mji wa Morbi Jumapili jioni ni mojawapo ya majanga mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini India kwa miaka mingi, na kuua watu 135, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee.
Daraja lililokuwa limefungwa lenye umri wa miaka 137 lilikuwa limefunguliwa tena siku tano tu zilizopita baada ya matengenezo - kwa hivyo ni nini kilienda vibaya?
BBC ilizungumza na walionusurika, wanahabari wa ndani na maafisa ili kufahamu zaidi mkasa huo.
Wakazi wa eneo hilo na waandishi wa habari wanalaumu kampuni iliyosimamia daraja hilo - na polisi na mamlaka za mitaa pia wanashutumiwa kwa kushindwa.
Dakika chache kabla ya maafa
Mara tu baada ya saa 12:30 saa huko (13:00 GMT) Jumapili, Mahesh Chavda na marafiki zake wawili walinunua tikiti zao na kuingia kwenye 'jhulto pul' ya Morbi (daraja linaloning'inia).
Inafafanuliwa na tovuti ya utalii ya jimbo hilo kama "maajabu ya kiteknolojia" na ni maarufu kwa watazamaji - palikuwa pamekuwa pahali pazuri pa Mahesh tangu alipokuwa mtoto.
Kupitia mto Machchu, wenye refu wa 230m (754ft) unaunganisha Darbargarh Palace na Chuo cha Uhandisi cha Lakhdhirji.
Tarehe za ujenzi wake zinatofautiana, lakini wenyeji wanasema ilijengwa katika miaka ya 1880 na Maharaja wa huko, Waghji Thakore.
"Nilikuwa nikiitembelea pamoja na wazazi wangu na, kwa miaka michache iliyopita, nilikuwa naenda huko kila Jumapili na marafiki zangu," anasema Mahesh. "Alifurahishwa" aliposikia wiki iliyopita kwamba daraja lilikuwa limefunguliwa tena na kijana huyo wa miaka 18 na marafiki zake waliamua kuendelea na utaratibu wao wa Jumapili jioni.
Akiwa amekaa kwenye kitanda chake cha hospitali huku akiwa amevaa plasta shingoni, Mahesh aliniambia kuwa walipokaribia daraja waliona kuwa kulikuwa na watu wengi kupita kiasi.
"Kwa hiyo tulidhani tungoje kidogo lakini mkagua tikiti alisema ni lazima tuendelee.
Daraja liliporomoka tulipokanyaga," alisema. Sehemu ambayo Mahesh na marafiki zake walikuwa wamesimama ilipinduka na kutupwa ndani ya mto mita 15 (45ft) chini.
Vijana hao watatu walijeruhiwa lakini wakanusurika.
Lakini wengine wengi hawakufanya hivyo na maafa hayo yameharibu familia nyingi ambazo watu wake wengi walipoteza maisha walipokuwa wakitembea jioni kwenye mto.
Shutuma kuhusu matengenezo
Watu wengi sasa wanauliza jinsi msiba wa kiwango hiki unaweza kutokea na kwa nini haukuzuiwa?
Daraja hilo lilifunguliwa kwa umma Jumatano iliyopita, ili kuendana na mwaka mpya wa Kigujarati.
Siku moja kabla, Jaysukh Bhai Patel, mmiliki wa kundi la Oreva, kampuni iliyopewa kandarasi ya kutunza na kuendesha daraja hilo tangu 2008, aliuambia mkutano na waandishi wa habari kuwa kazi ya ukarabati iligharimu rupia milioni 20 ($242,000; £211,200).
"Hakuna kitakachofanyika kwa daraja hilo kwa miaka 8-10 ijayo.
Na ikiwa litatumika kwa uwajibikaji, daraja hilo halitahitaji matengenezo kwa miaka 15," Times of India ilimnukuu akisema.
Anaripotiwa kusifia ubora wa kazi ya ukarabati, mitambo na mkandarasi ambaye kampuni hiyo ilimwajiri. Tangu ajali ya Jumapili, polisi wamewakamata watu tisa wanaohusishwa na Oreva - ikiwa ni pamoja na mameneja wawili na makarani wawili wa tikiti kwenye orodha yake ya malipo, pamoja na wakandarasi wawili na walinzi watatu iliowaajiri.
Wanachunguzwa kwa mauaji ya bila kukusudia.
BBC imewasiliana na Oreva ili kuuliza majibu yake kuhusu madai yanayowakabili. Mapema wiki hiyo msemaji wa kampuni aliiambia Indian Express kulikuwa na watu wengi sana katikati mwa daraja hilo, na baadhi walikuwa wakijaribu kulifanya liyumbe.
Oreva pia ameshutumiwa kwa makosa mengine, ikiwa ni pamoja na kushindwa kupata kibali kutoka kwa mamlaka ya kuendesha daraja hilo. Chifu wa manispaa ya eneo hilo Sandipsinh Zala aliwaambia wanahabari Jumatatu kwamba Oreva hakupewa cheti cha usalama kabla ya kulifungua tena.
Lakini wengi wanahoji kwa nini kampuni inayojulikana kwa kutengeneza saa iliruhusiwa kutunza daraja. Pia hutengeneza bidhaa za taa, baiskeli zinazoendeshwa na betri na vifaa vya nyumbani.
Bw Zala hakujibu simu zetu wala kujibu ujumbe wetu, lakini msaidizi katika ofisi yake aliniambia kuwa Oreva alikuwa amepata kandarasi ya kukodisha daraja hilo kutoka kwa wasimamizi wa wilaya mwaka wa 2008.
"Bw Zala amesasisha kandarasi hiyo mwezi wa Machi," msaidizi huyo aliongeza. BBC imeona nakala ya makubaliano hayo ambayo ni halali kwa miaka 15 - hadi Machi 2037.
Inasema kuwa matengenezo na usalama ni jukumu la kampuni ambayo pia huhifadhi mapato kutoka kwa mauzo ya tikiti.
Kwa mujibu wa waraka huo, kampuni hiyo inaruhusiwa bei ya tikiti kwa rupia 15 kwa watu wazima na rupia 12 kwa watoto, lakini ilikuwa ikitoza rupia 2 kwa kila tikiti.
Mamlaka imeahidi uchunguzi kamili na timu maalum ya uchunguzi imeundwa kuchunguza sababu za maafa.
Nani wa kulaumiwa kwa msongamano wa watu?
Kwa maelezo yote ya Morbi, kilichosababisha kuporomoka ni idadi kubwa ya watu walioruhusiwa kupanda daraja kwa wakati mmoja.
Watu wengi wanasema zaidi kungekuwa na watu 100-150 kwenye daraja hilo, lakini watu wengi walioshuhudia wanakadiria kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 500 kwenye daraja hilo.
Mwanahabari na mkazi wa muda mrefu wa Morbi Pravin Vyas, ambaye anaishi karibu na daraja hilo, anasema hajawahi kuliona likiwa na watu wengi kiasi hicho." Likizo ya wiki moja ya Diwali. Wengi pia walifurahi kuwa nje wakisherehekea baada ya miaka miwili ya vizuizi vya Covid-19," alisema.
"Ni jukumu la usimamizi kuona ni watu wangapi wanaweza kuruhusiwa kwa usalama wakati wowote kwenye daraja. Lakini inawanufaisha kuruhusu watu zaidi kwa sababu kuingia kumekatiwa tikiti," akaongeza.
Bw Vyas anasema uongozi wa mji na polisi pia hawana lawama." Kulikuwa na maelfu ya watu wanaotembelea daraja hilo kila siku tangu lilipofunguliwa, kwa hivyo mamlaka haiwezi' walisema hawakujua kuhusu hilo kwa sababu Oreva hakuomba ruhusa kutoka kwao."
Wakosoaji wanashangaa jinsi eneo ambalo lilivuta maelfu ya wenyeji na watalii kila siku lilikosa hatua za usalama kukabiliana na dharura? Ilikuwaje hapakuwa na polisi karibu , hakuna wazamiaji na na boti, wanauliza.
Uongozi wa wilaya unasisitiza kwamba kuhakikisha usalama wa wageni lilikuwa jukumu la kampuni.
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Ziada NK Muchhar aliniambia kuwa anajivunia jinsi walivyoitikia kwa haraka mgogoro huo na operesheni kubwa ya uokoaji waliyoanzisha ambayo imeokoa maisha."Tulipata wazamiaji, waogeleaji, kamba, boti na huduma za zimamoto hapa kwa dakika 10," alisema.
Wengi hata hivyo wanaeleza kuwa idadi ingekuwa kubwa zaidi kama si kwa waokoaji wa kwanza ambao walijumuisha wenyeji na kundi la vibarua wa karibu wanaojenga hekalu jipya kwenye kingo za mito.
Niranjan Das alikuwa amemaliza tu kazi yake ya siku kwenye eneo la hekalu na alikuwa ameketi na wenzake kando ya daraja, wakitazama giza likianza kuufunika mji.
"Tuliona watu waking'ang'ania kwenye sehemu za daraja," anasema. Kamba za eneo la ujenzi zilitumika kumshusha yeye na wenzake saba ndani ya maji.
"Tuliokoa watu wanane na kutoa maiti kadhaa." Anaonesha majeraha kwenye mikono na miguu ya mwenzake ambaye pia alishiriki katika uokoaji.
Parbat Govind, mwenye umri wa miaka 61 ambaye alihamia Morbi miaka miwili iliyopita na kuwasimamia wafanyakazi, alikuwa hekaluni pia, na alitazama mkasa ulivyokuwa ukiendelea. "Vidonda hivyo vitapona," alisema. "Lakini hatutasahau tulichoshuhudia siku hiyo. Hatutaweza kusahau mayowe hayo."