Tetesi kubwa tano za siku

Cristiano Ronaldo
Maelezo ya picha, Cristiano Ronaldo
Iliyochapishwa

Miamba ya Italia Inter na Milan zote zinanuia kumsajili Cristiano Ronaldo msimu huu wa joto.

Corriere dello Sport inasema wakala Jorge Mendes aliwasiliana na vilabu hivyo  viwili mwishoni mwa mwezi Juni na mwanzoni mwa Julai ili kuangalia ofa nzuri kwa kwa mteja wake.

Inadaiwa Ronaldo hana wasiwasi kujiunga na timu yoyote kati ya hizo mbili kutokana na ukubwa wao katika soka la Italia na duniani kwa ujumla.

Barcelona itahitaji ada kubwa kutoka kwa Chelsea ili kumpata Pierre-Emerick Aubameyang ingawa alijiunga na klabu hiyo kwa uhamisho wa bure mapema mwaka huu, kulingana na ripoti za michezo.

Klabu hiyo ya London Magharibi ina nia ya kuongeza nguvu zaidi kwenye eneo la ushambuliaji kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa baada ya kumtoa kwa mkopo Romelu Lukaku kurudi Inter na kumuuza Timo Werner kurudi RB Leipzig.

Mercelo Bersovic

Chanzo cha picha, Reuters

Manchester United imekua timu iliyo mstari wa mbele kuhitaji kumnunua kiungo wa Inter Marcelo Brozovic.

Tarifa za michezo kutoka Italia zinasema Liverpool inaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa United na Paris Saint-Germain kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Youri Tielemans

Ripoti mpya zinadai Leicester wanaweza kuwa tayari kumuachia kiungo wake Youri Tielemans ajiunge na Arsenal bure.

Gazeti la The Sun linasema The Gunners wanaweza kuwa tayari kumsubiri bila malipo yoyote mara tu mkataba wake na Foxes utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.

Mbelgiji huyo aliwasili Leicester msimu wa joto wa 2019, baada ya kipindi cha awali cha mkopo, na kusaini mkataba wa miaka minne.

AS Monaco imethibitisha kumnunua kiungo mkabaji Mohamed Camara kutoka Red Bull Salzburg.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mali mwenye umri wa miaka 22 anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa majira ya kiangazi kwenye kikosi hicho cha Ligue 1 , huku mkataba wa Camara ukitarajiwa kuwa wa miaka 5.

Mohammed Camara

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohammed Camara

Camara, ni miongoni mwa viungo wa ulinzi mahiri na ameshinda ubingwa wa  Austria mara tatu akiwa na Salzburg.

“Tunaomba sote tuwe na subira na michakato yote inayoendelea kwa sasa na kuiombea IEBC ili waweze kukamilisha zoezi hili kwa jinsi tulivyopiga kura,” Ruto alisema.

"Tumekuwa na uchaguzi wa amani, ni maombi yangu kumaliza mchakato huu kwa amani,"