Tetesi za soka Ulaya Jumanne 20.08.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Wolves wamewasilisha pendekezo la kumsajili kipa wa Uingereza Aaron Ramsdale kwa mkopo kutoka Arsenal na chaguo la kumnunua msimu ujao. (Athletic – Subscription Required).

Mshambulizi wa Chelsea na Uingereza Raheem Sterling, 29, amekuwa akihojiwa na Juventus huku kukiwa na sintofahamu kuhusu mustakabali wake. (Mail)

Klabu ya Saudi Pro League, Al-Hilal ina mlinzi wa Manchester City Muingereza Kyle Walker na beki wa pembeni wa Ureno Joao Cancelo kwenye orodha yao ya wachezaji wanaowania uhamisho. (Guardian)

Manchester City wana nia ya kutaka kumnunua tena kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 33, kutoka Barcelona. (Athletic – Subscription Required)

Real Sociedad wanakataa kupunguza thamani yao ya kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania anayelengwa na Arsenal Mikel Merino, 28. (Mirror}.

Brentford wanatarajia mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney kujiunga na Al-Ahli katika Ligi ya Saudia Pro League na wanatumai kupokea takriban £50m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Times – Subscription Required).

Hata hivyo, Chelsea wanaweza kujaribu kutaka kumnunua Toney katika saa za mwisho za dirisha la uhamisho. (Sun)

Fulham wanafikiria iwapo watarejea Crystal Palace na ofa nyingine ya kumnunua mlinzi wa Denmark Joachim Andersen, 28. (Sky Sports),

Na Fulham pia wanajiandaa kutuma ofa ya tatu kwa kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland Scott McTominay, 27. (TeamTalks)

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 25 pamoja na nyongeza kwa mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah, 23, kutoka Nottingham Forest. (Sun)

Newcastle bado wanaamini kuwa wanaweza kumsajili beki wa Uingereza Marc Guehi, 24, kutoka Crystal Palace, lakini pia wanamfikiria mlinzi wa Liverpool na England Joe Gomez, 27, pamoja na beki wa kati wa Chelsea, 25, Mwingereza Trevoh Chalobah. (i Sport).

Manchester United wako tayari kusubiri hadi siku ya mwisho ya kuhama ili kumsajili Manuel Ugarte, 23, kwa matumaini kwamba Paris St-Germain itapunguza thamani ya £51m kwa kiungo huyo wa kati wa Uruguay. (Guardian)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Argentina Giovani Lo Celso, 28, anawavutia Aston Villa, Real Betis na Roma. (Express)

Everton wameuliza kuhusu kuanzisha kipengele cha kutolewa cha euro 60m (£51.2m) kwa mshambuliaji wa Atletico Mineiro mwenye umri wa miaka 18 kutoka Brazil Alisson Santana. (Globo – In Spanish)

Nottingham Forest inafikiria kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Feyenoord na Mexico Santiago Gimenez, 23, baada ya ofa yao ya euro 25m (£21.3m) kukataliwa. (Athletic – Subscription Required)

Wolves wanamfuatilia beki wa kati wa Sheffield United na Bosnia na Herzegovina Anel Ahmedhodzic, 25. (Football Insider).

Chelsea imeifahamisha klabu ya Napoli kuwa wanataka angalau euro 40m (£34m) kwa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, huku The Blues wakipanga kukataa ofa ya mkopo yenye dau la la euro 30m (£25.6m) kumnunua kutoka kwa klabu hiyo ya Italia. (Ben Jacobs)

Beki wa Chelsea na England aliye chini ya umri wa miaka 21 Bashir Humphreys, 21, anatazamiwa kujiunga na klabu ya Burnley kwa mkopo ikiwa na chaguo la kumnunua. (Athletic – Subscription Required).

Beki wa Burnley Mbrazil Vintinho, 25, amekubali masharti ya kibinafsi ya kujiunga na klabu ya Brazil Botafogo. (Globo – In Portuguese}

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla