Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini unaweka vidole kwenye pua yako?
Wengi wetu hufanya hivi, lakini hawakubali. Iwapo watashikwa moja kwa moja, watahisi aibu au kujutia kufanya hivyo.
Na ikiwa wataona wengine wakifanya hivyo hadharani, watahisi kuchukizwa. Kutambuliwa kwa usahihi.
Wote kama binadamu kuna wakati unajipata umeweka kidole kwenye pua.
Je, hii ni tabia mbaya? Na kwanini.
Kuweka kidole kwenye pua yako kunafahamika kama Rhinotylexomania kwa Kiingereza.
Thompson na Jefferson mnamo 1995 wamefanya utafiti juu ya hili huko Marekani.
Alichunguza watu 1000 baada ya kuwatumia barua pepe. Watu 254 walijibu barua pepe hii. Asilimia 91 kati yao wakakiri kuweka kidole kwenye pua zao.
Kati ya hao, asilimia 1.2 walikiri kufanya hivyo kila saa.
Wote walisema kuwa tabia ya kuweka vidole kwenye pua inaharibu maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya watu hata walisema kwamba wameweka vidole vyao kwenye pua zao kiasi kwamba waliharibu kiini kinachotenganisha pua ya kulia na ya kushoto.
Utafiti huo haukuwa wa kina sana kwasababu ni asilimia 25 tu ya watu walioshiriki katika uchunguzi huo.
Ikiwa uchunguzi ungetumwa kwa watu ambao tayari walikuwa na nia ya kuweka vidole kwenye pua, wangeweza kupata majibu bora zaidi.
Hakika hii ni tabia ambayo inahitaji kukabiliwa. Lakini inaweza kusemekana kuwa watu wengi wanaifanya.
Tabia hii imekithiri sana miongoni mwa vijana
Miaka mitano baadaye Chittaranjan Andrade na BS Srihari, watafiti wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Akili na Neuroscience, Bangalore, walifanya utafiti.
Utafiti wao uligundua kuwa tabia hii ni ya kawaida kati ya vijana ikilinganishwa na watu wazima.
Utafiti mwingine ulifanywa miongoni mwa watu matajiri, wenye tabaka la kati na chini huko Bengaluru.
Jumla ya vijana 200 walichunguzwa. Wengi wao walisema kwamba wana tabia hii. Imebainika kuwa hii itafanyika mara nne kwa siku.
Asilimia 7.6 ya vijana walikiri kufanya hivyo mara 20 kwa siku. Asilimia 20 walikubali kwamba ni tatizo kubwa.
Wengi wao walisema kwamba hutumia vidole vyao kupunguza kuwasha kwenye pua au kuondoa uchafu.
Asilimia 12 ya watu walisema kwamba ni vizuri kufanya hivyo.
Wanafunzi tisa walisema sio tu wao huweka vidole kwenye pua bali pensili.
Tabia hii haina umri maalum. Pia haubagui jinsia. Inatokea sana hata kwa watoto.
Kando na hii, pia kuna wale wenye tabia ya kula kucha na kuvuta nywele zao.
Mara nyingi wasichana huchukizwa na tabia hii.
Madhara yanayoweza kutokea
Kuweka vidole kwenye pua yako sio hatari sana.
Lakini katika baadhi ya matukio kuweka vidole kwenye pua husababisha matatizo mengi makubwa.
Srihari na Andrade waliwahi kupata kisa kimojakama hicho ambapo mwanamume mmoja alifanyiwa upasuaji.
Upasuaji wenyewe ulihusisha mishipa iliyokuwa imefura kwenye pua.
Ilibainika kuwa kidonda hakikupoa kwasababu ya kuchokora pua kwa kutumia vidole kila mara.
Katika kisa kingine, kulikuwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 53. Alikuwa anaweka kidole chake kwenye pua yake kiasi kwamba kutoboa tishu.
Mwingine mwenye umri wa miaka 29 alikuwa na tabia ya kuvuta nywele za pua.
Mara nyingi, hii hufanya pua kupata majeraha. Na akalazimika kupata dawa ya krimu ili vindonda vipowe.
Maambukizi ya bakteria
Tabia ya kuchora pua kwa vidole sio kwamba ni hatari sana kwasababu haisababishi magonjwa mengine.
Haimaanishi kuwa ni salama kabisa.
Kulingana na utafiti uliofanywa na watafiti wa Uholanzi mwaka 2006, kuweka vidole kwenye pua kunaweza kusababisha maambukizi ya bakteria.
Watu wenye tabia ya kuweka vidole kwenye pua zao wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya bakteria yajulikanayo kwa jina S.Aureaus.
Hadi kufikia sasa, hakuna jibu na wazi kwanini baadhi ya watu hupenda sana kufanya tabia hii ya kuchukiza.
Pia kuweka vidole kwenye pua inaonekana kama ishara ya uvivu.
Bado baadhi ya watafiti wanafanyia kazi tafiti kujua hasa chanzo cha tabia hii.