Zainab: Malkia mwenye ushawishi mkubwa katika historia ya Kiislamu, kwa nini aliitwa mchawi?

Iliyochapishwa

Katika mtandao wa kijamii wa X, maneno yaliyoandikwa kwa Kiarabu juu ya picha ya shule huko Afrika Kaskazini yalinivutia.

Kwa kujua kidogo kuhusu lugha hiyo, nilijua maneno haya yalimaanisha nini. Ilisomeka, 'Zainab Al-Nafsawiya - Shule ya Sekondari ya Wasichana'.

Kutokana na picha kwenye bamba la karibu, ilifichuliwa kwamba malkia huyu, aliyeishi kutoka 1009 hadi 1106, alikuwa mke wa Yusuf bin Tashfin. Kulingana na mwanafalsafa na mwanahistoria Ibn Khaldun, alijulikana kama "mmoja wa wanawake maarufu ulimwenguni kote kwa uzuri na uongozi wake".

Nimesoma kuhusu Yusuf bin Tashfein kwamba ufalme wa kamanda mkuu wa kilemba cha jadi cha rangi ya bluu, jangwa na mbio za Berber, ulienea kutoka sehemu ndogo na isiyolindwa ya Afrika hadi sehemu za Morocco ya leo, Algeria na Uhispania.

Kwa vile Ibn Khaldun alizungumza kuhusu uongozi wa Zainab, nilitaka kupata taarifa kumhusu. Haya ndiyo niliyoyapata katika safari yangu ya maisha ya Zaynab al-Nafsawiya, mwanamke maarufu katika historia ya Kiislamu.

Mwandishi wa Morocco, Fatima Marnissi amempa malkia nafasi kubwa katika kitabu chake 'Forgotten Queens of Islam'.

Kati ya 1061 na 1107 Zaynab al-Nafsawiya alikuwa mtawala wa ufalme mkubwa ulioenea kutoka Afrika Kaskazini hadi Uhispania. Na alitawala na mumewe Yusuf bin Tashfin.

Wanahistoria walimwita Zainab 'Al-Qayma Bamlakihi', ambayo ina maana ya mtawala wa ufalme wa mumewe au mhusika mkuu anayeuendesha.

Mshauri mwenye busara

Zainab ni binti wa mfanyabiashara tajiri kutoka kabila la Nafsawa. Alizaliwa Aghmat (mji wa Morocco) ambapo alijifunza kusoma na kuandika.

Alilelewa na mwanamke kutoka familia ya kifalme ya Kiafrika kabla ya kuwa mtumwa. Alimfundisha Zainab kuhusu dawa za mitishamba.

Kwa mujibu wa Ibn Khaldun, aliolewa na Lakhut al-Mughrawi, amir (kiongozi) wa Ahmad. Baada ya Lagud kuuawa katika vita mali yake ilimwendea Zainab.

Aliolewa na al-Murawi Abu Bakr ibn Umar pili.

Wakati Abu Bakr alipokwenda kusini mwa jangwa kuzima uasi wa kikabila, aligawa mgawanyiko wa majeshi yake upande wa magharibi kwa binamu yake Yusuf bin Tashfin kabla ya kuondoka. Kwa kuogopa vita vya muda mrefu, alimtaliki Zainab.

Zainab aliolewa na Yusuf baada ya Iddat (muda uliokatazwa baada ya talaka) kwisha. Zainab alikua sio tu mwenzi wa maisha wa Yusuf bali pia mshauri wake mwenye busara.

Uwezo wa kijeshi wa Yusufu uliweka misingi ya usultani huu mkuu wa al-Murawi, ambao ulianzia Bahari ya Atlantiki kuvuka Algeria, Senegal, na Uhispania ya Kiislamu.

Kwa upande mwingine, ushauri wa Zainab na uelewa wa kisiasa ulikuwa na nafasi muhimu katika hili.

Kwa mujibu wa wanahistoria wengi, akiwemo Ibn Azari, al-Bakri, na Ibn Khaldun, Zainab alikuwa mrembo sana, aliyejaa nguvu, na kipaji kisicho cha kawaida.

Alikuwa na ujuzi mkubwa wa masuala ya sera. Wanahistoria wamemwita 'mchawi' kwa sababu hii.

Alisaidia kuandaa jeshi la Yusuf bin Tashfeen

Mwanahistoria Ibn Havgal anamtaja Zainab kama mmoja wa watu mashuhuri wa karne ya kumi na moja huko Afrika Magharibi. Kwa sababu ya ujuzi wake mkubwa wa masuala ya kisiasa, alikuwa na nafasi muhimu katika historia ya 'Maghrib' ya zama za kati.

Maghrib ni sehemu ya magharibi ya ulimwengu wa Kiarabu, pia inajulikana kama 'Arab Maghreb'. Ni eneo la Afrika Magharibi na Kati-Kaskazini linalojumuisha Algeria, Libya, Mauritania, Morocco na Tunisia na eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

Yusuf hakuwa na jeshi lenye nguvu la kuendeleza ushindi. Kulingana na jopo hilo, Zainab alitoa mali yake kwa Yusuf ili kupanga upya jeshi. Pia alimuagiza kukusanya ushuru kutoka mikoa mbalimbali.

Kwa hili alilitayarisha jeshi kwa kuunganisha makundi mbalimbali.

Ibn Abi-Zar anaandika katika kitabu chake 'Raus al-Qardas' kwamba Yusuf aliiteka Afrika Magharibi kwa amri ya Zaynab na Zaynab akafanya mazungumzo. Pia alijulikana kama 'Mchawi' kwa sababu ya ujuzi wake katika mazungumzo.

Yusuf alijenga mji wa Marrakesh (Morocco). Ikawa mji mkuu wa nchi inayokua. Inaonekana kwamba ni Zainabu aliyependekeza chaguo la mahali hapa.

Mji mkuu huu mpya hauko mbali na anapoishi Zainab. Katika sehemu nyingi inasemekana kwamba 'Qasr al-Hajr' (Ngome ya Mawe) ilijengwa kwa ajili yake na kwamba Yusuf mwenyewe alisaidia katika ujenzi wake kwa mikono yake mwenyewe.

Mume wa pili aliyerudi alikuwa Abubakar

Abu Bakr Ibn Umar akamjulisha binamu yake Yusuf kwamba amerejea kutoka vitani. Bila shaka alikuwa na matumaini ya kupata nguvu zake na mke wake nyuma.

Abul Hasan ibn Abu Zahar al-Fazi anaandika kwamba Zaynab aliingilia kati na kumwamuru Yusuf amkaribishe Abu Bakr pamoja na walinzi weusi wa Qana.

Yusufu aliketi juu ya farasi wake na kumkaribisha kama mfalme na kumpa zawadi nyingi.

Akiwa ameshangazwa na utajiri huo, Abu Bakr alimuuliza Yusuf sababu ya ukarimu wake na akajibu, "Ili usije ukakosa chochote jangwani ambako matukio mapya yanakungoja."

Abu Bakr alielewa maana ya ujumbe huu na aliamini kwamba lingekuwa jambo la busara kuzikubali zawadi hizo.

Baada ya kukaa kwa muda mfupi Aghmat, aliandika waraka wa uhamisho wa mamlaka. Na akasonga kuelekea jangwani ambako aliteka sehemu kubwa ya Ghana na Sudan.

Baada ya hayo, al-Murawi alibaki kuwa mkuu rasmi wa usultani hadi kifo chake mnamo 1087.

Nafasi ya Zainab katika kuwapa nafasi wanawake

Yusuf bin Tashfin akawa mtawala asiyepingika wa 'Maghrib' na mmiliki wa usultani mkubwa. Kulingana na Charles Noel, kunaweza kuwa na sababu kadhaa ya ushawishi mkubwa wa Zainab.

Kwanza, Zainab alielimishwa na ujuzi mdogo wa Yusuf wa Kiarabu ulimpa Zainab faida.

Pili, Zainab alipata ushawishi wa kisiasa kwa sababu ya imani ya mumewe katika nguvu zake za utu na uwezo wa kufanya maamuzi.

Sababu ya tatu inaweza kuwa kampeni za kijeshi zilizowaruhusu kufanya kazi wakati Yusuf hayupo.

Zainab alisaidia kuunda familia na mila zake ambazo ziliathiri sana hadhi ya wanawake katika usultani wa al-Murawi.

Kulingana na mila zao wenyewe, wanawake walishikilia nyadhifa za juu nchini Morocco wakati wa nasaba ya Al-Murawi.

Binti mfalme aliruhusiwa kushiriki katika masuala ya utawala. Kwa hili, elimu ya kike ikawa ya kawaida.

Kulingana na Alison Baker, takribani wanawake wawili wanaaminika kuwa madaktari. Vivyo hivyo, Princess Finu alishiriki katika utetezi wa mji mkuu wakati wa kuanguka kwa familia ya kifalme mnamo 1147.

Katika miongo ya hivi karibuni, maisha ya Zainab al-Nafsawiya yamejadiliwa katika televisheni na sinema. Lakini hali ya kudumu ya urithi wake inaonekana katika shule ambazo wasichana wanasomeshwa.

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga​.