Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kasisi asiyetaka 'kumsikitisha' Mungu ajenga kanisa na msikiti Ethiopia
Kasisi mmoja nchini Ethiopia anachangisha fedha za kujenga kanisa na msikiti katika mji uliopo eneo la mashariki la Hararge katika jimbo la Oromia.
Kiongozi huyo wa dini Abba Aklilemariyam Komos amesema kwamba hataki kumsikitisha Mungu kwa kujenga kanisa pekee.
Makanisa na Misikiti katika miji mikubwa ya taifa hilo yameharabika na waumini wameshindwa kuchangisha fedha zinazohitajika ili kufanya marekebisho.
Komo aliambia BBC Afaan Oromo kwamba ujenzi wa kanisa pekee na kupuuza hali mbaya ya misikiti iliopo 'utamsikitisha' Mungu.
Wazo lake la kuchangisgha fedha lilianza 2015 wakati wa ziara yake huko Lange wakati alipogundua hali mbaya ya makanisa.
Na mara tu alipoona hali hiyo aliamua kupanua wazo lake na kushirikisha misikiti.
''Iwapo nitachangisha fedha za ujenzi wa makanisa na huku hali ya misikiti ya ndugu zetu waislamu ipo katika hali mbaya, nitamsikitisha Mungu.
Dini zetu ni tofauti lakini sio imani zetu'', alielezea.
Aliwataka viongozi wa baraza la maswala ya Kiislamu nchini Ethiopia kumuelezea kuhusu misikiti iliopo katika mji mkuu wa Addis Ababa.
''Nilianza kuchangisha fedha tangu Oktoba 2018 mara ya kwanza nikienda katika msikiti wa Nur mjini Adis Ababa. Chini ya kipindi cha miezi miwili pekee tulifanikiwa kuchangisha $6,200'', alisema.