Je, mihimili ya kijeshi ambayo Putin aliitegemea inaanza kuporomoka?

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Uhamasishaji uliotangazwa nchini Urusi kuhusiana na vita vya Ukraine uliwalazimisha wengine kuondoka nchini au kujificha, wengine kununua risasi peke yao na kwa utiifu kwenda kwa kamisaa ya kijeshi.

Kwa nini mshtuko uliathiri karibu kila familia na kusababisha hisia tofauti kwa watu na jinsi gani uhamasishaji unaathiri ari ya jamii?

BBC ilizungumza na mwanasosholojia na mwanasaikolojia.

Katika siku za kwanza za uhamasishaji "wa sehemu" uliotangazwa na Putin mnamo Septemba 21, kiwango cha wasiwasi cha Warusi kiliongezeka maradufu. Utafiti uliofanywa na mfuko wa serikali wa "Maoni ya Jamii" (IFJ) unathibitisha hili.

Mnamo Septemba 25, asilimia 69 ya waliohojiwa walijibu: wana wasiwasi. Wiki moja iliyopita, kabla ya uhamasishaji kutangazwa, ni 35% tu ya waliohojiwa walizungumza kuhusu wasiwasi.

Kituo cha Levada, kilichoorodheshwa na serikali ya Urusi kama "mawakala wa kigeni" katika usajili wa shirika lisilo la kiserikali, NGOs, kilionesha matokeo sawa: asilimia 47 ya waliohojiwa walihisi "wasiwasi, hofu" katika tangazo la uhamasishaji, na asilimia 23 walishtuka.

13% ya waliohojiwa walisema walikuwa wamejaa hasira na chuki. 23% tu walizungumza juu ya hisia chanya, "kiburi cha Urusi".

66% ya waliohojiwa walikiri kuwa wanaogopa tangazo la uhamasishaji.

Huduma ya utafutaji ya mwanasaikolojia ya "Yasno" iliripoti kwamba idadi ya maswali kutoka kwa wateja wanaolalamika kuhusu wasiwasi imeongezeka sana.

"Tangu Februari 24, wasiwasi imekuwa sababu ya kawaida ya kuwasiliana na mtaalamu wa kisaikolojia (63% ya wateja wapya wa Yasno walibainisha hili katika uchunguzi).

Kabla ya hili, matatizo ya jadi ya waombaji yalihusiana hasa na hali katika mahusiano ya kimapenzi. Mienendo wasiwasi uliendelea hadi Aprili, kisha ukapungua polepole hadi 57% (Agosti, mapema Septemba), na baada ya Septemba 21, uliongezeka kwa kasi hadi 62%," Yasno iliiambia BBC.

Malalamiko kwa wanasaikolojia pia yanahusiana na mafadhaiko: tangu Februari 24, wakati Urusi ilipoanza uvamizi kamili wa Ukraine, idadi ya maombi inayoonyesha sababu ya mafadhaiko imeongezeka hadi 51%, katika msimu wa joto ilipungua hadi 44%, na baada ya hapo. uhamasishaji ulitangazwa, uliongezeka hadi 48%.

"Mnamo Februari-Machi, nilikutana na uzoefu fulani unaohusiana na ukweli mpya, lakini kwa wengi ulihusiana na uhamasishaji. Watu wanasema kwamba hili halipaswi kutokea kamwe, lisitokee kwangu mimi binafsi," Anton Savin, mtaalamu wa gestalt huko. huduma ya Yasno, iliambia BBC.

Vita vilianza

Vita viliathiri maisha ya Warusi wa kawaida, ambayo mazoezi ya binafsi ya Savin ina mifano mingi.

Watu wanaweza kuwa hawajagundua ni kiasi gani uvamizi wa Ukraine ulibadilisha ulimwengu wao, kwa sababu hadi wakati fulani mamlaka haikuhitaji idadi kubwa ya watu wa Urusi kushiriki kikamilifu katika vita.

Tayari kuna visa kadhaa vinavyojulikana vya kujiua kwa wale ambao walihusika katika uhamasishaji au walikuwa na uwezekano wa kuandikishwa katika vita.

Mwanaume mmoja wa Moscow alijaribu kujiua baada ya kupokea wito. Vyombo vya habari viliripoti kwamba aliokolewa. Wanajeshi wengine wawili walijiua katika vituo vya mafunzo vya jeshi.

Rapa Ivan Petunin mwenye umri wa miaka 27, anayejulikana kama Walkie, alijiua huko Krasnodar. Kabla ya kifo chake, aliandika kwamba hakuna njia nyingine: "Kuingia vitani ni kuua na kufa, na kuandamana ni kuteswa gerezani."

Hofu

Kujiondoa, kutokuwa na uwezo wa kutabiri maisha yako ya baadaye, hisia kwamba hatima yako huijui ni hali chungu, anaelezea mtaalamu wa kisaikolojia Anton Savin.

"Jambo lisilovumilika zaidi ni kwamba wakati mtu hawezi kujihisi wakala katika tukio , anapoteza ari yake ya kujitolea," anasema Savin, kwa kutumia maneno ya kitaaluma. Watu wengine hujaribu kupata tena udhibiti wa kitu fulani maishani mwao, mtaalamu anasema. Kwa mfano, wanaepuka utumishi wa kijeshi. wanasimama kwenye mstari mpakani au wanaondoka kwenda kijijini, mkoa mwingine.

"Inatisha sana kuwa katika hali ya kutatanisha, kwa hivyo ni bora nidhibiti hali hiyo." Kutokuwa na uwezo wa kuona siku zijazo ni uchungu sana, husababisha kifo au mauaji ya wengine katika mawazo ya mwanadamu. Inakuwa ngumu kwake hapa na sasa," mwanasaikolojia anaelezea mantiki ya wale wanaojiua.

Watu wengine kwa makusudi huchagua njia tofauti kabisa ya kujiondoa, ambayo mtaalamu anaelezea kama:

"Kama siwezi kufanya chochote, ni afadhali nijiunge na wakubwa na wenye nguvu na kufanya kile ninachoambiwa." Katika suala la uhamasishaji, nchi kubwa na yenye nguvu inamaanisha kufanya kile wanachosema, kuchukua barua ya wito na kuikubali kwa utumishi wa kijeshi.

Mwanzoni mwa vita na Ukraine, mnamo Februari-Machi, Savin alizingatia njia hii ya kukabiliana na ukweli mpya kati ya wale walio karibu naye.

Kutojali

"Ni muhimu kujitenga na watu walioaga sio kihisia tu, bali pia kijamii na kiuchumi. Watu hawa sio wadogo sana, lakini sio wazee pia," anasema Stepan Goncharov, mwanasosholojia wa Kituo cha Levada.

Mwanasosholojia anaamini kwamba wastani wa umri wao ni miaka 30.

"Huu ndio mtaji muhimu zaidi kwa uchumi: watu katika miji mikubwa ambao wanaweza kulipa, wana rasilimali za kutosha za kifedha na wakosoaji wa ukweli."

Na wanathamini sana maisha yao.

Lakini Goncharov anaamini kwamba tamaa ya kujiunga na serikali ni tabia zaidi ya watu ambao hawajaweza kujionyesha katika kazi au mafunzo, ambao wana mishahara ya chini na kujihisi wako chini.

Kwa maoni yake, fursa ya kwenda mbele inaonekana kama kitu cha maana katika maisha ambayo haikujengwa kwao. Watu wengi wanafikiri kwamba hii ni kazi nzuri. Na wanafikiri kwamba huko wanaweza kuanza tena na kuwa sehemu ya tukio la kihistoria."

"Mara nyingi serikali inabakia kuwa taasisi kuu pekee ambayo hutoa ajira kwa watu hawa na kuweka malengo makubwa.

Nilisikia majuto kwamba USSR ilikuwa na dhamira kubwa kabla ya kuanza kwa "Operesheni Maalum", na kwamba hatuna hivi sasa. . Hii ndiyo maana maalum ya maisha, ambayo huwa zaidi ya "kupata pesa kwa chakula na kupeleka mtoto shule", anaelezea mwanasosholojia.

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi