Mahangaiko na kashfa za mtoto wa rais wa Marekani

Iliyochapishwa

Hunter Biden, mtoto pekee wa Joe Biden ambaye bado ni hai, anachunguzwa. Waendesha mashitaka wanaripotiwa kuwa wamechunguza ushahidi wa kutosha wa kumshitaki kwa uhalifu unaohusiana na ushuru na kwa kutoa kauli za uongo kuhusiana na ununuzi wa bunduki, kulingana t related to a gun purchase, according to US media.

Hunter Biden - ambaye amekuwa mlengwa wa ukosoaji wa Republican -amekuwa akifanyiwa uchunguzi juu ya uwezekano wa kukiuka sheria za kulipa ushuru na na utakatishaji wa pesa tangu tangu mwaka 2018.

Taarifa zinasema kwamba wachunguzi wameweza kuweka shutuma zake katika mashitaka mawili: iwapo hakuweza kuripoti mapato yake yote, na iwapo alilaghai matumizi yake ya mihadarati wakati aliponunua bunduki ya mkononi.

Rais wa zamani Donald Trump na washirika wake alidai kwa muda mrefu kwamba Hunter Biden mwenye umri wa miaka 52 -anakabiliwa na makosa, akisema mikataba yake ya kigeni ya biashara - hususan katika China Ukaraine - inaonyesha ushahidi wa ufisadi. lakini wakati Hunter amekiri hadharani kwa kufanya mambo ambayo anayajutia, yeye na rais wamekuwa wakikanusha kuwa alivunja sheria yoyote. Rais Biden,a mabaye amesema "anajivunia sana " mwanaye , amesimama na yeye katika mahangaiko yake ya kibinafsi na ya umma.

Iwe Bidern au mwanaye hakuna aliyezungumzia kuhusu uwezekano wa mashitaka yake.

Uwezekano wa kisheria kufuatia miaka ya Hunter Biden ya machungu ya kibinafsi , ikiwa ni pamoja nakuvubjika kwa ndoa na uraibu wa madawa ya kulenvya - matatizo ambayo yameingia katika siasa tangu baba yake alipoingia White House.

Litakuwa ni jukumu la mwanasheria mkuu wa marekani katika Delaware - aliyeteuliwa na Bw Trump mwishoni mwa kwaka 2017 -kuamua iwapo Bw Bw hunter Biden atakabiliwa na mashitaka au la.

Lakini kwa sasa, ni nini tunachokifahamu kumuhusu Hunter Biden? Mkasa wa utotoni

Akizaliwa katika Wilmington, Delaware, mwaka 1970 na wazazi Biden na mke wake wa kwanza Neilia Biden, Hunter alipewa jina la kike la mama yake.

Alikuwa na umri wa miaka mwili pekee Disemba 1972 - wiki moja kabla ya Krismasi na chini ya wiki sita baba yake achaguliwe kuwa seneta wa Marekani - wakati lori lilipoigonga gari ya familia na kumuua mama yake na dada yake ambaye alikuwa mchanga Naomi.

Ajali ilimuacha akiwa na fuvu lililovunjika na kaka yake Beau na mkuu uliovunjika. Biden, baba yao ambaye hakuwemo ndani ya gari hilo - alikula kiapo cha mamlaka kutoka katika chumba cha hospitali.

Hunter baadaye alihudhuria masomo katika chuo kikuu cha Georgetown na shule ya sheria ya Yale , ambapo alihitimu mwaka 1996.

Wakati akisomea shahada hizo mbili, alijiunga na taasisi ya Jesuit Volunteer Corps, kikundi cha Wakatoliki ambacho hujitolea kuzisaidia familia za watu waliotengwa.

Huku, alikutana na mke wake wa kwanza, Kathleen Buhle,wakili, na wakaoana mwaka 1993. Wana watoto watatu - Naomi, Finnegan na Maisy - lakini wawili hao waliachana katika mwaka 2017.

'Giza' la Uraibu

Baba yake ni hanywi pombe, lakini Hunter alianza kunywa pombe alipokuwa kijana mwenye umri wa kubalehe na alikiri kutumia mihadarati aina ya Cocaine alipokuwa mawanafunzi wa chuo.

Amekuwa ndani na nje ya kituo cha kurekebisha tabia, kutokana na mihadarati. Katika mwaka 2013, alijiunga na kikosi cha wanamaji cha akiba cha Marekani na kula kiapo cha mamlaka mbele ya baba yake - aliyekuwa makamu wa rais - katika sherehe ya White Houset.

Katika siku yake ya kwanza ya kazi katika ngome ya kikosi cha majini, alibainika kuwa anatumia cocaine baada ya kufanyiwa vipimo na akaondolewa kikosini, jambo ambalo baadaye alisema''lilimuaibisha''

Kulingana na gazeti la New Yorker, alikunywa pombe kupita kiasi baad ya kifo cha kaka yake mkubwa , Beau, kilichotokana na saratani mwaka 2015, wakati mwingine huondoka nyumbani tu kwa ajili ya kununua vodka.

"Yeye na Beau alikuwa kitu kimoja," binti yake Naomi aliandika wakati mmoja kwenye Twitter. "Moyo mmoja, roho moja, akili moja."

Wakati wa talaka iliyowasilishwa katika mwaka 2017, Bi Buhle alimshutumu Hunter kwa "kutumia pesa kiholela kwa maslahi yake ya kibinafsi (mkiwemo mihadarati, pombe, klabu za utupu, na kununua zawadi kwa ajili ya wanawake ambao ana mahusiano nao ya kimapenzi ) huku akiiacha familia bila pesa za kulipia gharama halali".

Akivunja kimya chake mwezi Juni kuhusu jinsi ndoa yao ya miaka 24 ilivyokuwa ya masaibu, Bi Buhle alikiambia kipindi cha Good Morning America: "Anahangaika sana kutokana na uraibu mkubwa wa madawa ya kulevya, na kwamba hilo linavunja moyo na inamuza na kwamba sio mtu niliyeolewa naye ."

Katika kitabu chake cha 2021 Beautiful Things, Hunter alikiri kwamba ukosefu wake wa uaminifu katika ndoa kwa Bi Buhle ndio uliovunja ndoa yao. Vipimo vya vinasaba DNA katika mwaka 2019 vilibaini kuwa alikuwa "baba halali wa kibaiolojia " wa mtoto aliyezaliwa na mcheza densi za utupu, Lunden Alexis Roberts.

Hunter anadai kuwa "hakuwa na kumbukumbu " juu ya jinsi alivyokutana naye katika kitabu chake. Lakini ametatua kesi ya malezi ya baba na Bi Zoberts na asasa analipia malezi ya mtoto.

Na kabla yakukamilisha talaka na Bi Buhle, Hunter alianza mahusiano na mjane wa kaka yake , Hallie Biden, kwa miaka miwili, ambapo, alisema alikuwa na uhusiano wa karibu kutokana na kushirikiana "kwa maombolezo ya kipekee " ya kifo, aliliambia gazeti la The New Yorker.

Wiki chache baadaye, Hunter alimuoa mtengenezaji filamu wa Afrika Kusini Melissa Cohenbaada ya kimbunga cha siku sita za mahaba. Wana mtoto mmoja pamoja.

Akizungumza kuhusu jinsi anavyohangaika na uraibu mwaka 2019, alisema : "Hauondokani nao. Unatafuta njia ya kukabiliana nao."

Katika kitabu cha Beautiful Things, anashukuru familia yake kwa upendo, akikumbuka ilivyomnusuru jinsi baba yake alivyomshikilia na kumkumbatia, akisema: "Sijui ni kitu gani kingine cha kufanya. Ninaogopa. Niambie la kufanya."

Gazeti la New York Times liliripoti kuwa alianza kuchora kama njia mojawapo ya tiba, likimnukuu akisema kwamba "inanifanyika niwe mbali na watu na maeneo ambayo sipaswi kuwa".

Lakini mwaka 2021 aliuza michoro yake kwenye maonyesho ya sanaa - kwa hadi dola $50,000 kwa mchoro mmoja -jambo ambalo lilisababisha ukosoaji kuhusu mwelekeo wa maadili katika White House inayoongozwa na Biden.

Kuchanganya familia na biashara Baada ya kuhitimu katika Chuo cha sheria cha Yale, Hunter alifanya kazi katika MBNA America, kampuni ya benki yenye makao yake makuu katika jimbo la Delaware na ambayo baadaye ilichukuliwa na benki ya Marekani - Bank of America.

Hatahivyo, uhusiano wa karibu wa baba yake na benki - ambayo ni muajiri mkuu katika Delaware na ikiwa ilikuwa ni mchangiaji mkuu katika kampeni zake za kisasa za baba yake - aliweza kupata upendeleo kutoka kwa benki hiyo".

Wakati Hunter alipopandishwa cheo hadi kuwa Makamu rais mtendaji wa benki hiyo, baba yake alishinikiza mageuzi ya sheria ya kunusuru kufirisika kwa benki kupitia Seneti ambayo yalionekana kuipendelea benki.

Katika mwaka 2006, aliyekuwa seneta wakati huo Biden  alipanga kuihakikishia kamati ya kigeni ya bunge,mwanaye wa kiume Hunter na ndugu wengine walipata ufadhili kutoka kwa  kikundi cha Paradigm Global Advisors.

 Muhula wao katika  Paradigm ulirefushwa kupitia kugombea kwa urais kwa Bw  Joe Biden mwaka  2008 na kuchaguliwa kama  Makamu wa rais wa Obama.  

 Katika kipindi hiki, ufadhili uliuhusishwa na  wahalifu kadhaa mafisadi, akiwemo kiongozi wa  mfumo wa ufadhili wa oliyepatikana na hatia ya mfumo wa ufisadi  mkubwa zaidi unaojulikana kama Ponzi schemes katika historia ya Marekani. Familia ya Biden ilikanusha kufanya kosa lolote na hawakukabiliwa na mashitaka yoyote. Katika mwaka  2010, walirejesha  pesa kwa wawekezaji.