Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 12.06.2024

Iliyochapishwa

Juventus wamepiga hatua katika juhudi yao ya kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, kutoka Aston Villa. (Sky Sports)

Chelsea wamefufua nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 20. (Telegraph - usajili unahitajika)

Mlinzi wa Chelsea na England Levi Colwill, 21, bado ananyatiwa na Bayern Munich ambao pia wanataka kumnunua beki wa Ujerumani na Bayer Leverkusen Jonathan Tah,28. (Sky Germany)

Colwill, hata hivyo, ametulia Chelsea na klabu haitaki kumuuza. (Standard)

Bayern pia wameanza mazungumzo na Leverkusen kumhusu Jonathan Tah. (Bild)

Manchester United wanajiandaa kuchuana na Arsenal katika harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 23, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 34. (Metro)

Arsenal wanakabiliwa na changamoto ya kumbakisha mashambuliaji wa chini ya miaka 17 wa Denmark Chido Obi-Martin, 16, ambaye anasakwa na Bayern Munich. (Metro)

Manchester United wameandaa orodha fupi ya washambuliaji huku mshambuliaji wa Brentford ya Uingereza Ivan Toney, 28, na mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David, 24, wakizingatiwa sana. (ESPN)

West Ham wamempa beki wa Uingereza Ben Johnson, 24, mkataba ulioboreshwa wa miaka mitano. (Athletic - michango inahitajika)

Fulham wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua Silas Katompa Mvumpa, 25, kutoka Stuttgart, huku fowadi huyo wa DR Congo akiwa na thamani ya £15m. (HITC)

Arsenal wako tayari kumuuza mlinzi wa Scotland Kieran Tierney kwa hasara msimu huu, na ofa ya pauni milioni 15 itatosha kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 32, anajadiliana na Brighton kuhusu kuongeza mkataba wake. (Athletic - usajili unahitajika)

Crystal Palace, Ipswich na Southampton wanamuwania beki wa Rochdale George Nevett ,18, kutoka Wales . (HITC)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi