Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (24.08.2022)
Mchezaji mpya Emerson Palmieri anasema kuwa soka la Ulaya ni kiwango sahihi kwa West Ham baada ya kujiunga na The Hammers kutoka Chelsea kwa £15m.
West Ham ilifuzu kwa European Conference League baada ya kumaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita lakini ndio timu pekee ya Ligi Kuu ambayo bado haijavuna pointi moja katika kampeni mpya.
"Ni kiwango cha timu hii, klabu inastahili hivyo mradi ni huu. Ni wazi tunapaswa kujaribu kupigania hili.
"Nina mawazo mazuri kwani nataka kushinda kila mchezo."
Leicester City wamekataa ofa ya tatu kutoka kwa Chelsea kwa Wesley Fofana, inayoaminika kuwa kati ya £60m na £70m.
Inafahamika kuwa ofa ya beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 21 inajumuisha vipengele vya nyongeza, ambavyo baadhi yao vinachukuliwa na Leicester kuwa si vya kweli.
Lakini Foxes ambao bado hawajashinda msimu huu, wameshikilia msimamo wao kwamba Mfaransa huyo hauzwi.
Na inaweza kuchukua ada ya rekodi ya dunia kwa mlinzi - zaidi ya £80m - kwa City kuzingatia uhamisho wa Chelsea.
Gazeti la Mirror linaripoti kwamba Everton tayari inawaangalia wachezaji wachache wanaoweza kuchukua nafasi ya Gordon.
Majina yanayotajwa ni Che Adams wa Southampton au Joao Pedro wa Watford ambaye pia amekuwa akiwindwa na Newcastle.
Kwa mujibu wa The Athletic na wengine, West Ham wanatarajia kumsajili Lucas Paqueta kutoka Lyon.
Je, huyu ndiye mchezaji wa kubadilisha msimu ambaye West Ham wanamhitaji?
Callum Wilson ana imani kuwa anaweza kujipata katika kikosi cha England cha Gareth Southgate kwa Kombe la Dunia mwaka huu.
Mchezaji nambari tisa wa Newcastle amecheza mechi nne tu za England hadi sasa, akifunga mara moja.