Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
B-21 Raider:Ndege mpya ya kivita ya Marekani ina uwezo gani dhidi ya maadui?
Je la wanahewa la Marekani wiki jana lilizindua ndege yake ya kisasa yenye uwezo wa kinyuklia B-21 Raider ambayo imetajwa kama ‘yenye uwezo mkubwa’ sana kivita.Hatua hiyo iliyojiri wakati huu ambapo kuna mvutano mkubwa wa kisiasa wa kijiografia kati ya Marekani, Urusi na China huku kukiwa na vita vya Ukraine mzozo kuhusu Taiwan.Haya hapa baadhi ya mambo kuihusu ndege hiyo unayofaa kujua
Gharama
Jeshi la Wanahewa la Marekani linapanga kununua angalau 100 ya ndege ya B-21, ambayo inagharimu $700m kwa kila ndege, msemaji wa Northrop Grumman alisema. Marekani inalenga kununua ndege hii ili kuchukua nafasi ya ndege ambazo zilitumika wakati wa kipindi cha vita baridi .
Silaha za Nyuklia
Ndege hii ina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia na nyingine za kawaida .Ina uwezo wa kujificha ili isionekana na rada na sifaa hii inaifanywa kuwa hatari sana kwa ndege nyingine za mashambulizi katika uwanja wa vita .
Kama inavyotarajiwa, maelezo maalum ya ndege bado yamegubikwa na usiri.
Lakini Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema ni "ushuhuda wa manufaa ya kudumu ya Marekani katika ustadi na uvumbuzi".
Bw Austin alisema ndege hiyo itatoa maendeleo makubwa dhidi ya ndege za mashambulizi zilizopo katika jeshi la Marekani, akisema kwamba "hata mifumo ya kisasa zaidi ya ulinzi wa anga itajitahidi kugundua B-21 angani".
"Miaka hamsini ya maendeleo katika teknolojia isiyoonekana sana imeingia kwenye ndege hii," alisema.
Silaha za siku zijazo
Aliongeza kuwa ndege hiyo pia ilijengwa kwa "usanifu wa mfumo wazi," ambayo inaruhusu kuingizwa kwa "silaha mpya ambazo hata hazijavumbuliwa".
Ingawa uwezekano wa safari ya ndege isiyo na marubani haukutajwa wakati wa hafla hiyo, msemaji wa Jeshi la Wanahewa la Marekani alisema ndege hiyo "imetolewa kwa uwezekano huo, lakini hakujawa na uamuzi wa kuruka bila marubani".
Safari ya kwanza ya ndege ya B-21 inatarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Hatimaye itachukua nafasi ya ndege aina za B-1 na B-2 ndgez hizo zinakadiriwa kugharimu $203bn (£165bn) kuendeleza, kununua na kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30, kulingana na Bloomberg.
Ndege sita kwa sasa ziko katika uzalishaji, mtengenezaji alisema, akiongeza kuwa zitaangazia "kizazi kijacho cha siri" na kwamba kinatumia "mbinu na nyenzo mpya za utengenezaji" ambazo hazijabainishwa.
Jeshi la Wanahewa la Marekani linapanga kununua takriban ndege 100.
Ndege za ‘maadui’
Moscow na Beijing pia kwa sasa wanaunda ndege za kivita zenye uwezo wa kimkakati - Xian H-20 ya Uchina na Tupolev PAK DA ya Urusi yenye uwezo wa nyuklia - ambayo inatarajiwa kushindana na B-21.
Ingawa B-21 ina uwezo wa kupaa angani bila rubani, Jeshi la Wanahewa la Marekani lilisema ndege hiyo "imetolewa kwa uwezekano, lakini hakujawa na uamuzi wa kuruka bila marubani".