Paul Pogba: Manchester United ilikuwa ‘kizuizi kwangu’

Iliyochapishwa

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anasema "kila kitu" ikiwemo suala la "kocha, timu, nafasi" "ilimzuia" katika klabu yake ya zamani Manchester United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amejiunga tena na Juventus baada ya kuondoka United baada ya mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford kumalizika.

‘Nafurahia mabadiliko niliofanya katika Maisha yangu’, alisema

‘Mara nynegine unafanya chaguo ambalo halikufurahishi, lakini nafurahia miaka yangu Manchester., Nilikuwa , nikajifunza na kuwa mwanaume’.

Pogba ambaye , alianza soka kupitia chou cha mafunzo ya soka katika timu ya Manchester United aliondoka katika klabu hiyo 2012  na kujiunga na Juventus kabla ya kushinda mataji manne ya Serie A na baadaye kuondoka na kujiunga ten ana man United kwa dau lililovunja rekodi ya dunia la £89m katika uhamisho wa 2016.

Alishinda Kombe la EFL na lile la Ligi ya Yuropa akiichezea United katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo lakini yalikuwa mataji pekee aliyoshinda katika kipindi chake cha pili akiwa nao.

Aliwachezea mameneja Jose Mourinho, Ole Gunnar Solskjaer, Michael Carrick na Ralf Rangnick baada ya kurejea United na akashindwa kuonyesha kiwango chake bora kwa misingi thabiti chini ya kila mmoja wao.

Hata hivyo, Pogba, ambaye ana mechi 91 za kimataifa, alikuwa na ushawishi wakati Ufaransa iliposhinda Kombe la Dunia nchini Urusi mnamo 2018.

"Kubadilishwa kwa makocha [wa Manchester United] kila mwaka ni ngumu – hiki  kilikuwa kipengele kigumu kwangu," alisema Pogba. "Kisha kulikuwa na majeruhi wachache, lakini nadhani pia lilikuwa jambo la kiakili - kucheza na kutocheza kunakufanya upoteze kasi.

"Kuna kila kitu: kocha, timu, nafasi. Haya yote yamenizuia kidogo.

"Sasa, hata hivyo, nimeondoka na utaona Paul mwingine. Ninaweza kufanya vizuri zaidi kuliko miaka ya hivi karibuni."

Pogba amesaini kandarasi ya miaka minne na Juventus, ambayo ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye Serie A msimu uliopita.

Aliongeza: "Nimefurahi kurudi nyumbani, hivi ndivyo ninavyojisikia hapa. Hiki ni kitu zaidi ya ndoto. Nina furaha sana.

"Kulikuwa na timu zingine zilizokuwa na nia, lakini moyo wangu ulichagua Juventus. Nilikuwa vizuri hapa awali na niko sawa sasa, nataka tu kufanya vizuri.