Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 27.08.2022: Fofana, Ronaldo, Antony, Firmino, Aubameyang

Ronaldo

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Mwakilishi wa Cristiano Ronaldo Jorge Mendes amezungumza na Napoli kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji huyo wa Manchester United na Ureno, 37. (Sky Sports).

Manchester United wanatafakari iwapo wataachana na harakati zao za kumnunua Antony baada ya Ajax kukataa ofa ya tatu ya pauni milioni 76 kwa mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 22. (Telegraph)

Liverpool huenda wakamtoa mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino, 30, kumpata kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Argentina Leandro Paredes, 28. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Fermino

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wamefikia makubaliano ya kumsajili beki wa Leicester City Wesley Fofana mwenye umri wa miaka 21, kwa ada inayoaminika kuwa pauni milioni 70. (The Athletic- Usajili unahitajika)

Leicester wanafikiria kumnunua kwa mkopo beki wa Borussia Dortmund na Uswizi Manuel Akanji, 27, kama mbadala wa Fofana anayelengwa na Chelsea. (Mail)

Chelsea wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Urusi Arsen Zakharyan, 19, kutoka Dynamo Moscow. (Mail)

Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juhudu za Chelsea kumnasa mshambuliaji wa Barcelona na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang zagonga mwamba

Juhudu za Chelsea kumnasa mshambuliaji wa Barcelona na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang imekwama katika masuala ya kibinafsi huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 akitaka mkataba wa miaka miwili naoThe Blues wakijiandaa kumpatia mkataba wa mwaka mmoja pekee. (Sun)

Nottingham Forest wamewasiliana na Everton kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Uingereza Michael Keane, 29, kwa mkopo. (Football Insider)

West Ham wamekubali dili ya kumnunua kiungo wa kati wa Lyon Lucas Paqueta baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kukataa ombi lao la kwanza la mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)

Michael Keane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Beki wa Everton Muingereza Michael Keane

Celta Vigo wamewasilisha ofa y akumnunu mshambuliaji wa Blackburn Rovers na Chile anayenyatiwa na Everton Ben Brereton Diaz, 23. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Celtic na Denmark aliye na umri wa chini ya miaka 21 Matt O'Riley, 21, anavutia hisia kutoka kwa Borussia Dortmund, Liverpool, Arsenal na Manchester United. (ESPN)