Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 12.12.2022: Rashford, Guardiola, Mount, Gvardiol, Dalot, Felix, Ramos,

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcus Rushford
Iliyochapishwa

Paris St-Germain wako tayari kumfanya mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika kandanda huku wakiweka kifurushi cha kujaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye mkataba wake na Manchester United unamalizika msimu wa joto. (Mirror)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anasema klabu hiyo itatumia chaguo la kuongeza mkataba wa Rashford na beki wa kulia wa Ureno Diogo Dalot, 23, hadi 2024 huku wakijadili kuongezwa kwa mkataba wa wawili hao. (Metro)

Shirikisho la Soka la Brazil linapanga kuwasiliana na meneja wa Manchester City Pep Guardiola ili kujua kama angependa kuwa meneja wa timu ya taifa mwishoni mwa msimu huu. (Sport – In Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pep Guardiola

Chelsea, Manchester City na Manchester United wamewasilisha ofa kwa mchezaji wa kimataifa wa Croatia mwenye umri wa miaka 20 Josko Gvardiol, huku Bayern Munich pia wakimtaka beki huyo wa RB Leipzig. (Foot Mercato – In French}

Wakala wa mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, ambaye tayari amefanya mazungumzo ya awali na Chelsea na Manchester United, anatarajia kuzungumza na Aston Villa na Newcastle United kuhusu kiwango chao cha kutaka kumnunua mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid, 23. (Mirro)

Arsenal wameingia kwenye orodha ya vilabu, ikiwa ni pamoja na PSG, wanaomtaka Felix. (AS – In Spanish)

.
Maelezo ya picha, Kiungo wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix

Juventus wanaweza kutafuta kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na England Mason Mount, 23, na kumwachia mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, kiungo wa kati wa Argentina Leandro Paredes na Mmarekani Weston McKennie, 24, kuondoka ili kutafuta fedha kwa ajili ya uhamisho huo. (CalcioMercatoWeb – In Itali)

Rais wa Benfica Rui Costa anasema klabu haitamruhusu mchezaji wake yeyote muhimu, akiwemo mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 21 Goncalo Ramos, kuondoka katika klabu hiyo isipokuwa tu iwapo masharti yao ya ununuzi yatatimizwa. Ramos amekuwa akihusishwa na Manchester United. (Correio da Manha – In Portugal)

Newcastle wanatumai kumsajili mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, huku Arsenal na Manchester United pia wakifuatilia hali ya mchezaji huyo wa miaka 24 huko Chelsea. (Mirro)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cristian Pulisic

Newcastle itamruhusu beki wa kati wa Uingereza Jamaal Lascelles mwenye umri wa miaka 29 na beki wa kushoto wa Ireland ya Kaskazini Jamal Lewis, 24, pamoja na winga wa Scotland Matt Ritchie, 33, na Ryan Fraser, 28, kuondoka mwezi Januari iwapo watapewa nafasi hiyo. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Mali Boubacar Traore, 21, anatarajiwa kutimiza masharti katika uhamisho wake wa mkopo kwenda Wolves kutoka Metz ili kuwa mkopo  wa kudumu wa pauni milioni 9.5 katika kipindi cha pili cha msimu. (Express & Star)