Tabia tatu zinazokuchosha bila kutambua na jinsi ya kukabiliana nazo

Iliyochapishwa

Je umechoka kiasi kwamba ni huwezi hata kuielezea huku tayari ukiwa umehakikisha kuwa huna shida yoyote ya kiafya?

Labda tayari umefuata ushauri wa kawaida kutoka kwa wataalam kama kula chakula bora, mazoezi, na kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha.

Na bado...

Inaonesha kuwa kuna tabia fulani za kila siku ambazo zinaweza kumaliza nguvu zako bila hata kuzishuku.

Miongoni mwa vitu vinavyokula nguvu zako ni mambo ya kawaida, kama vile kukaa katika sehemu isiyofaa au kuahirisha muda wa chakula.

Pia mambo tunayofanya bila kutambua, kama vile kupumua vibaya pale tunapokuwa na mawazo mengi sana, kama mwanasaikolojia Uma Naidoo alivyoongea na gazeti la Huffington Post au kufungua vipengele vingi kwenye kompyuta kama daktari wa neva Rana Mafee alivyodokeza katika chapisho hilo.

Lakini kuna zisizotarajiwa na ili kuzichunguza daktari wa magonjwa ya akili Leela R. Magavi wa Vituo vya MindPath huko California alizielezea.

1. Mfululizo wa filamu katika televisheni, sinema na habari

Kutazama mfululizo wa filamu au sinema ni kitu tunachofanya ili kupumzika, kwa nini tulimuuliza Dk. Magavi, wataalam kama yeye wanajumuisha katika orodha ya sababu zinazoweza kusababisha uchovu wa akili?

"Kama binadamu, sisi ni viumbe wenye hisia na wengi wetu ni wenye huruma na hupokea hisia za wahusika katika vipindi vya televisheni na sinema”.

"Wanaweza kutukumbusha uchungu tuliopitia katika maisha yetu, aina yoyote ya mapungufu, udhaifu, hasara au kutojiamini na yote hayo yanaweza kusababisha hisia nyingi, kama vile huzuni, wasiwasi, hofu, hasira, ambazo hatakama ziko chini ya fahamu zetu zinaweza kutuathiri”.

"Kwa hivyo unapotazama vipindi vingi vya TV, hata kama haunekani kufikiria waziwazi, hisia hizo zitakuwa wazi.

"Wakati unafanya kazi, ukiwa na familia yako, hisia hizo nyingi zinaweza kukutawala na kukufanya uhisi uchovu siku nzima bila wewe kujua."

Magavi aliongeza kuwa kitu kama hicho kinaweza kutokea baada ya kutazama au kusoma habari, "kwa sababu zinakufanya ufikirie juu ya kile kinachotokea ulimwenguni." Na alifafanua kuwa hamaanishi ni vibaya kutazama televisheni au kusoma magazeti.

Namna ya kukabiliana

"Ninachopendekeza ili kupambana na uchovu huo ni baada ya kusoma au kutazama kitu, kifafanue iwe kupitia jarida au kwa kuandika (kuandika mawazo na hisia zako ili kuzielewa kwa uwazi zaidi), au kuzungumza na rafiki au mtu wa familia.

"Hiyo inaruhusu hisia kutoka, ili zisikae ndani na hivyo hazitumii nguvu yako."

 Lakini sio kila wakati una muda wa kujitunza sana ... kuna njia ya haraka zaidi?

 "Ni vizuri kujichunguza akili tu : makala au kipindi gani cha televisheni kiliibua hisia ndani yangu?

 "Hiyo inaweza kuwa haraka sana na rahisi kufanya.

 “Mfano ukiangalia tu ‘The Lion King’ unajisikia huzuni kwa sababu baba anakufa, hiyo inaweza kukusababishia wasiwasi wa kifo cha watu unaowapenda, lakini kwa kufanya uchunguzi wako wa akili utakumbuka kuwa kila mtu anafanya kila linalowezekana ili kuwa na afya.

 "Kitu kifupi kama hicho kinaweza kukusaidia kutoingiza hisia hizo ndani na kujiruhusu kushambuliwa nazo."

Isipokuwa

Kusoma hadithi katika vitabu, kunaweza kuwa na athari tofauti.

"Siyo tu kwamba kuna mwanga wa bluu kutoka kwenye kioo cha televisheni ambao husababisha mkazo wa macho na maumivu ya kichwa, lakini unaposoma unatumia mawazo yako mwenyewe, watu wengi wanaona kuwa kusoma, hata kama kuna leta hisia sana, ni tiba nzuri na ya kutuliza. ".

2. Michezo

Kwa kweli, jambo lingine kati ya yale yanayoburudisha, ambayo hututoa nje siku hadi siku, inaweza kuwa njia nyingine ya kunyonya nguvu mwilini.

"Mashabiki wa Avid wanaweza kuzama sana katika mchezo na kuchukua ushindi na kupoteza kama ndio wahusika weneywe , wakihisi huzuni kupita kiasi na kukata tamaa au kufurahia.

"Hisia yeyote iliyopita kiasi au hisia kali kwa kawaida huchosha, furaha iliyozidi inaweza kuchosha ubongo; huzuni kubwa inaweza kuhusishwa na wasiwasi, ambayo huzidi katika ubongo na kukufanya uhisi huzuni sana, kuchoka".

Namna ya kukabiliana na hili

"Jambo muhimu ni kufahamu kile unachohisi.

"Ikiwa umesisimka sana, jiulize: je, ninahitaji kupumzika, kupata vitafunwa, kuoga haraka ... ninahitaji kufanya nini ili kutuliza kwa wakati huu?

"Pumua kwa ndani, jinyooshe na tembea kidogo."

3. Mipango

Kupanga ni njia ya kudhibiti ukweli, kupanga maisha, kushinda machafuko, shika usukani.

Ni kitu ambacho tungeweka katika kipengele cha vitu vinavyoondoa msongo wa mawazo, lakini ni kinaweza kusababisha.

Katika kesi hii, taarifa kwamba (karibu) kila kitu kinachozidi ni kibaya inajirudia tena.

Kupanga ni muhimu sana ... hadi katika hatua hii

Kuweka wazi ratiba yenye shughuli nyingi kunaweza kusababisha wasiwasi ulioongezeka na kuathiri vibaya kumbukumbu na kasi ya kutafakari.

"Watu wengine hutumia saa nyingi kutengeneza ratiba na orodha ambazo hawawezi kuishi  nazo kwa akili na kufurahiya maisha yao. Wanakuwa na wasiwasi kila wakati kwamba wanaweza kushindwa kwa hili." wenyewe kwa yale waliyoyatimiza siku hiyo.

"Hiyo inaweza kusababisha hisia nyingi za huzuni, kukata tamaa au uchovu." Kwa watu wengine hiyo inaisha kwa ndoto.

"Nina wagonjwa watu wazima wanaota kwamba watachelewa shuleni, hawakumaliza kazi zao za nyumbani ... wana ndoto nyingi ambazo zinawarudisha utotoni, ambapo wanahisi kama wako nyuma na hilo huwafanya wajisikie vibaya asubuhi".

Namna ya kukabiliana

"Siku zote napendekeza kutumia dakika 5-10 kufikiria tu malengo makuu ya siku ni yapi na mwisho wa siku, hata kama hayajafikiwa usitumie muda mwingi kufikiria juu ya hayo bali juu ya yale yaliyopatikana, kwa nini ni muhimu.

Daktari wa magonjwa ya akili pia anapendekeza kutofanya mipango mapema sana, "kwa sababu maisha daima yanabadilika na ni muhimu kubadilika."

"Wakati watu wanamipango ya muda mrefu, wanatarajia tu kwamba kila kitu katika ulimwengu wao wa kigeni kitaenda kama saa inavyofanya kazi ili kufikia lengo hilo kwa wakati.

"Lakini ikiwa kitu kinabadilika katika familia zao, kwa marafiki zao, katika kazi zao na hawawezi kufikia lengo hilo, wanahisi kuzidiwa kabisa."

Ujanja mmoja ni kupanga mipango ya lazima mikutano, miadi, sherehe za familia na kuwa huru katika muda ulibakia