Utafiti: Mchwa wanaoweza kugundua saratani

Chungu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanasayansi waliweza kutoa mafunzo kwa Formica fusca, kugundua dalili za saratani ya matiti kwa binadamu.
Iliyochapishwa

Mchwa siku moja wanaweza kutumika kusaidia kugundua saratani kwa wanadamu, utafiti mpya unapendekeza.

Wanasayansi kwa mara ya kwanza wamegundua kuwa mchwa wanaweza kugundua ugonjwa huo kwa panya.

"Mchwa wanaweza kufunzwa ndani ya dakika kumi kunusa kansa kwenye mkojo wa panya," Baptiste Piqueret, mwandishi mkuu wa utafiti huo aliambia BBC.

Piqueret alianza utafiti wake katika uwanja huo mnamo 2017 na aliweza kutoa mafunzo kwa mchwa kutofautisha kati ya seli zenye afya na seli za saratani zilizokuzwa kwenye maabara.

Lakini sasa, timu yake imepiga hatua zaidi: wakati huu mchwa wamegundua uvimbe wa binadamu katika panya.

Kufundisha mchwa kutambua harufu mbaya

Piqueret na timu yake walitumia mbinu inayoitwa xenografting - kupandikiza saratani ya matiti ya binadamu katika panya na kuiruhusu kukua.

Kisha walikusanya sampuli za mkojo kutoka kwa panya wenye afya na wale walio na saratani.

"Wakati wa mafunzo, tuliweka mchwa kwenye uwanja wa duara na kuweka chakula kama zawadi karibu na mkojo kutoka kwa panya wenye saratani," alisema.

Mchwa wanapopata zawadi, huhusisha harufu kutoka kwa seli za saratani na hujifunza kuitambua

Mchwa

Chanzo cha picha, Getty Images

"Seli ni kama viwanda, zinahitaji virutubisho ili kuishi na hutoa taka. Seli za saratani huzalisha taka ambazo zinaweza kugunduliwa katika harufu," Piqueret alisema.

Hasa, utafiti unaelezea, seli za saratani zina misombo maalum ya kikaboni ambayo inaweza kugunduliwa kwenye mkojo au pumzi.

Wakati wa mchakato wa mafunzo, mchwa bado wangekaa kwa muda mrefu karibu na sampuli za mkojo wenye saratani hata baada ya wanasayansi kuondoa zawadi.

Je mchwa wanaweza kutumiwa kugundua saratani kwa binadamu?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

La bado, Piqueret alisema.

"Ili kupiga hatua zaidi ingebidi tuanze kupima mkojo wa binadamu," aliongeza, lakini hilo lingekuwa gumu zaidi kuliko kupima mkojo wa panya.

Kufunza mchwa kugundua harufu ya saratani kwa wanadamu kungejumuisha anuwai nyingi, kama vile umri, jinsia, lishe, lakini pia harufu maalum ambayo kila mwanadamu anayo.

"Binadamu hawana harufu sawa, inatofautiana kati ya mtu na mtu, na hatujui kama mchwa wanaweza tu kuzingatia seli za saratani," Piqueret alielezea.

Lakini amejitolea kufanya utafiti zaidi kwani anaamini kuwa mchwa wanaweza kuwa wagunduzi bora na gharama ya chini ambao havihitaji muda mwingi kufunzwa.

"Moja ya faida ni kwamba mchwa wanaishi katika makoloni na kubadilishana habari," alisema.

Piqueret anashuku kwamba ikiwa 10% ya kundi la chungu wanapata mafunzo ya kutambua saratani, wanaweza kueneza ujuzi huo kwa wengine.

"Labda taarifa zingeenea, na hatungelazimika kupoteza muda kutoa mafunzo kwa koloni zima," alisema.

Nadharia hii tayari imethibitishwa kufanya kazi na nyuki, lakini ingehitaji uchunguzi zaidi na mchwa, Piqueret alisema.

Ni wanama wapi wengine wanaweza kugundua saratani ?

Dr Debajit Saha and his team

Chanzo cha picha, Derrick L. Turner/Michigan State University

Kwa kipindi cha miaka 10, Dkt Debajit Saha kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan imekuwa akichunguza nzige na uwezo wao wa kusaidia kugundua seli za saratani.

Timu yake imegundua kuwa nzige wanaweza kunusa tofauti kati ya seli za saratani na zenye afya

Lakini hawajaribu kufundisha nzige, badala yake wanajaribu kuingia kwenye akili zao.

"Tunaweza kwenda moja kwa moja kwenye ubongo na kutumia ujuzi uliopo wa sayansi ya neva kutengeneza kielelezo kutoka kwa ishara za neva," Dk Saha aliiambia BBC.

Wanatumai kuwa ujuzi wanaoukusanya wakichunguza ubongo wa nzige utawapa msingi wa kutengeneza kifaa kinachotumia nyuroni za hisi za wadudu kugundua saratani kwa kutumia pumzi ya mgonjwa pekee.

"Ninapenda wazo zima la kutumia viumbe vya kibaolojia na kufikiria jinsi ya kuvitumia kugundua magonjwa," Saha alisema.

Lakini sio wadudu tu wanaoweza kusaidia.

Mbwa akiwa amekalia bechi kwenye bustani

Chanzo cha picha, Getty Images

Nchi Uingereza Shirika la Medical detection dogs linalotoa misaada ya kimatibabu limekuwa likifanya shughuli ya kutengeneza pua ya kielektroniki ambayo inaweza kunusa na kubaini saratani ya tezi dume.

"Kazi yetu ilianza na kuchunguza iwapo mbwa wanaweza kubaini saratani ya kibofu cha mkojo. Ilichunguza uwezo wa mbwa kubaini sampuli ya mkojo kutoka kwa wagonjwa wa saratini ," Sophie Aziz, mkuu wa utafiti na maendeleo ya kibiashara aliambia BBC.

Shirika hilo lilitoa mafunzo kwa mbwa sita wa aina tofauti mwaka wa 2004 na iligundua kuwa usahihi wa uchunguzi ulikuwa mara tatu zaidi ya kiwango kilichotarajiwa.

Uchunguzi wa baadaye ulithibitisha kuwa mbwa wanaweza kunusa saratani ya kibofu cha mkojo kwa usahihi wa karibu asilimia 90.

Utafiti mwingine umeonyesha kuwa mbwa wanaweza pia kunusa saratani ya ovari kutoka kwa sampuli za damu za wagonjwa. Mbwa waliofunzwa waliweza kuigundua katika asilimia 99 ya visa.

Baadaye ukaja utafiti wa kutengeneza pua ya kielektroniki, lakini imekuwa na changamoto kwa sababu ya nuances ya harufu.

"Hasa linapokuja suala la magonjwa, harufu inaweza kuwa tofauti kulingana na microbiome ya mtu mwenyewe, majibu yao ya kinga kwa ugonjwa," Aziz alisema.

Lakini anaamini kuwa utafiti huo mpya wa wadudu unaweza kuambatana na tafiti zingine za kugundua saratani.

"Kadiri tunavyoweza kujifunza zaidi kuhusu ufalme wa wanyama, ndivyo inavyokuwa bora zaidi. Kadiri utafiti unavyotoka kwa vikundi kama sisi, au kutoka kwa wanasayansi wanaoangalia jinsi mchwa wanaweza kugundua saratani, ndivyo inavyokuwa bora zaidi. Yote yanaongeza katika kujenga picha kubwa," Aziz. sema.