Uhamisho wa Paul Makonda wazua hisia kali mitandaoni Tanzania

.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Paul Makonda
Iliyochapishwa

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali katika serikali yake, wakiwemo mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu , wakuu wa mikoa na Wilaya.

Miongoni mwa walioteuliwa ni katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo ya chama tawala cha CCM bwana Paul Makonda ambaye sasa ndiye mkuu mpya wa mkoa wa Arusha.

Makonda alikuwa amehudumu katika nafasi yake ya awali kwa takriban miezi mitano.

Aliteuliwa na halmashauri kuu ya CCM mwezi Oktoba 2023 akichukua nafasi ya Sophia Mjema.

Vilevile baadhi ya maafisa wakuu serikalini walitenguliwa na rais Samia akiwemo Profesa Joyce Ndalichako aliyehudumu katika baraza la mawaziri kama waziri wa Ofisi ya waziri mkuu , kazi, Vijana Ajira na wenye Ulemavu.

Badala yake Deogratius Ndenjembi aliyekuwa naibu waziri wa Temisemi amepandishwa cheo na kuchukua wizara ya Ndalichako.

Rais Samia vilevile amemteua Fakii Lulandula kuwa mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Gilbert Kalima aliyekuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi ya Chama cha mapinduzi CCM ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Waliohamishwa na rais Samia ni katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja kwenda kuwa katibu mkuu Ofisi ya makamu wa rais Muungano na Mazingira.

Zainab Katimba ameteuliwa kuwa naibu waziri wa Tamisemi akichukua nafasi ya Ndenjembi.

Vilevile Balozi Asha Rose Migiro ndiye mjumbe mpya wa Tume ya Mipango naye Dkt. Edwin Mhende akiteuliwa kuwa naibu waziri wa mifugo na Uvuvi huku Amos Makalla aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwekwa kando.

Uteuzi wa Paul Makonda wazua hisia mitandaoni

Hatahivyo ni uteuzi wa mkuu mpya wa Arusha Paul Makonda uliovutia hisia nyingi katika mitandao ya kijamii.

Wengi wameuchukulia uhamisho wa Makonda kama mpango wa kimkakati huku wengine wakidai kwamba ni hatua ya kumshusha cheo kiongozi ambaye ameonekana akikua kwa kasi.

Kulingana na gazeti la The Citizen Tanzania wakili wa Independent Peter Madeleka anasema alichukua jukumu la kumuelimisha Makonda kuhusu masuala ya kikatiba na kisheria , hususan haki za kibinadamu akisema kwamba atafanikiwa katika kuelewa sheria.

‘Nina jukumu la kumfunza bwan makonda kuhusu katiba na sheria, hususana ile ya haki za binadamu , ninaamini atafanikiwa’, aliandika katika mtandao wake wa X

Anasema kwamba Makonda hakuwa na uwezo wowote wa kutoa maagizo kwa mawaziri kama alivyofanya katika wadhfa wake wa awali.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Mtumiaji mwengine wa mtandao wa X Tobadi Kayusi alinukuliwa akihoji maono ya uteuzi huo wa kisiasa badala ya kuangazia masuala yenye tija , akiongezea kwamba kuna umuhimu wa kufanyika kwa mijadala inayoangazia masuala muhimu badala ya teuzi za kisiasa.

‘’Kwanini tusitumie muda wetu mzuri kujadiliana masuala muhimu badala ya kuchanganua teuzi za kisiasa?’’, Alihoji.

Wengine w alihoji iwapo cheo cha Paul Makonda kimepanda ama kimeshuka

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Watumiaji wengine wa mtandao wa X hawakuficha hisia zao kuhusu uteuzi huo

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 3

Hatahivyo kuna wale waliofurahishwa na uteuzi huo wa Makonda

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 4