Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Arsenal yapiga hatua usajili wa Guimaraes

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano ya awali ya kuilipa Newcastle euro milioni 90 kumsajili kiungo wa Brazil, Bruno Guimaraes, mwenye umri wa miaka 28. (L'Equipe)

Inter Milan iko tayari kulipa pauni milioni 30 kwa ajili ya kiungo wa Uingereza, Curtis Jones, lakini Liverpool inakadiria thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa pauni milioni 35. (Mail)

Jitihada za Inter Milan kumsajili Cristian Romero wa Tottenham zimegonga mwamba kutokana na masuala ya masharti yake binafsi, na wawakilishi wa beki huyo wa Argentina sasa wanachunguza uwezekano wa yeye kuhamia Uhispania, huku klabu za Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid zikionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Teamtalk)

AC Milan imekuwa ikiwasiliana na Arsenal kuhusu uwezekano wa dili la kumsajili winga wa Ebgland, Ethan Nwaneri, mwenye umri wa miaka 19. (Corriere dello Sport)

Real Madrid haina mpango wa kumuongeze mshahara Vinicius Jr na iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa Brazil, mwenye umri wa miaka 26, iwapo hatakubali mkataba mpya. (ESPN)

Newcastle United iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kipa wa Jamhuri ya Czech, Lukas Hornicek (24), kutoka Braga kwa ada ya pauni milioni 25. (Talksport)

Hull City inakabiliwa na ushindani mkali katika mbio za kumsajili kiungo wa Neom, Amadou Kone (21), kwani klabu nyingine kama Leeds na West Ham nazo zinamtaka mchezaji huyo raia wa Ivory Coast. (Teamtalk)

West Ham inataka kumsajili winga wa Kiingereza, Morgan Whittaker (25), kutoka kwa wapinzani wao wa ligi ya Championship, Middlesbrough, kabla ya kuanza kwa msimu mpya. (Talksport)

Middlesbrough inakamilisha makubaliano ya kumsajili beki wa pembeni wa Marekani, Max Arfsten (25), kutoka Columbus Crew kwa dili lenye thamani ya hadi pauni milioni 5.6. (Goal)

Wolves imekataa ofa ya Real Sociedad kwa ajili ya beki wa Jamhuri ya Czech, Ladislav Krejci (27). (Fabrizio Romano)