Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.09.2024
Paris St-Germain wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuitaka imlipe Mbappe £46m,Alphonso Davies anakaribia kuondoka Bayern Munich kwa uhamisho wa bila malipo, Napoli na Inter Milan wanamlenga Takehiro Tomiyasu wa Arsenal na Manchester United wanawania saini ya 'Jude Bellingham' mpya.
Paris St-Germain wamekata rufaa dhidi ya uamuzi ambao utawalazimu kumlipa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25 - ambaye alihamia Real Madrid msimu huu wa joto - £46m ambazo zimezuiliwa kama mshahara wake na marupurupu kutokana na muda aliohudumu katika klabu hiyo. ( Athletic-Usajili unahitajika)
Beki wa Arsenal na Japan Takehiro Tomiyasu, 25, amezivutia Napoli na Inter Milan. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Mkufunzi wa AC Milan Paulo Fonseca, ambaye timu yake inacheza na wapinzani wao Inter Milan siku ya Jumapili, anasema hafikirii juu ya uvumi kuhusu mustakabali wake baada ya timu yake kuanza vibaya msimu huu. (Football Italia)
Mkufunzi wa Liverpool Arne Slot anasema klabu hiyo "imesonga mbele" kutokana na kushindwa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi mwenye umri wa miaka 25 kutoka Real Sociedad msimu wa joto. (Mirror)
Liverpool wanaendelea na mazungumzo ya kandarasi ya winga wa Colombia Luis Diaz, 27, licha ya kukatishwa tamaa na wawakilishi wa mchezaji huyo katika majira ya joto. (Teamtalk)
Kipa wa Espanyol Joan Garcia anasema hakukengeushwa na nia ya Arsenal katika msimu wa joto, ingawa The Gunners wanaweza kumnunua Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 23 katika dirisha la uhamisho la Januari. (Mirror)
Bayern Munich wamekata tamaa ya kurefusha mkataba wa Alphonso Davies mwishoni mwa msimu huu, huku Real Madrid wakimtaka beki huyo wa Canada mwenye umri wa miaka 23. (Relevo - kwa Kihispania)
Newcastle United itamfuta kazi mkurugenzi wa michezo Paul Mitchell kabla ya kufikiria kuachana na meneja Eddie Howe iwapo mvutano kati ya wawili hao utaendelea. (Football Insider)
Manchester United inamvutiwa na winga wa Southampton mwenye umri wa miaka 18 Tyler Dibling lakini klabu hiyo ya pwani ya kusini inapanga kuongeza mkataba wake. (GiveMeSport)
Kiungo wa kati wa Sunderland Chris Rigg, 17, ni chipukizi mwingine kwenye rada ya Manchester United , huku klabu hiyo ya Old Trafford ikimtazama kijana huyo wa kimataifa wa Uingereza kama 'Jude Bellingham' mpya. (HITC)
Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi anasema amepokea ofa za kuvutia lakini bado hayuko tayari kurejea kwenye usimamizi wa soka. (Revelo - kwa Kihispania)
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah