Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Arsenal, Chelsea na Manchester United zampigania Dusan Vlahovic

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Klabu tatu za ligi ya Premier bado zinavutiwa na Dusan Vlahovic, Liverpool watoa ofa ya kwanza kwa Mohamed Salah na pia wanataka Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold kusaini mikataba mipya.

Arsenal, Chelsea na Manchester United bado wanavutiwa na Dusan Vlahovic, huku Juventus wakifikiria kumuuza mshambuliaji huyo wa Serbia, 24, isipokuwa kama atakubali mkataba mpya. (TBR Football)

Liverpool wametoa ofa ya mkataba mpya wa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32. (Athletic – Subscription Required)

Liverpool pia wanatazamia kuwafunga beki wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, na mlinzi wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, kwa mikataba mipya. (Star)

Manchester City wanaweza kuharakisha kuipiku Liverpool katika mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, kutoka Real Sociedad. (Football Insider)

Jitihada za Crystal Palace kumsajili winga wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki mwenye umri wa miaka 21 zimezuiliwa na wababe wa Ulaya Paris St-Germain pamoja na Borussia Dortmund wanaojiunga katika kinyang'anyiro hicho. Sun)

Aston Villa ni moja kati ya klabu nne za Ligi Kuu ya Uingereza zinazomtaka winga wa Juventus na Uturuki Kenan Yildiz, 19, ambaye klabu yake inawweza kumuuza kwa takriban £66m. (BirminghamLive, nje)

AC Milan wana nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Carney Chukwuemeka, 21, ambaye pia anawavutia Celtic kwa mkopo. (Soccer Italia,)

Mshambulizi wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 18, Endrick ameamua kutoondoka kwa mkopo mwezi Januari na ataendelea kupigania nafasi ya kuanzishwa. (Marca – In Spanish)

Winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, anakaribia kusaini mkataba wa nyongeza na Napoli hadi 2029. (Corriere dello Sport – In Itali)

West Ham ilimchukulia Massimiliano Allegri kama mrithi wa kocha wa sasa Julen Lopetegui lakini gharama inayohusika inafanya uwezekano wa kutoanza. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla