Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mesa: Mji wa kwanza wa Marekani unaoweza kufikiwa kwa urahisi na watu wenye tatizo la usonji
Likizo zinaweza kuwa za mfadhaiko kwa watu wa aina mbalimbali ya matatizo ya neva, lakini mji wa Mesa, Arizona, unazingatia maslahi ya kila mtu aweze kufurahia safari wakati wa likizo yake.
Mnamo 2018, Marc Garcia alishtushwa na sura ya kushangaza na ukosefu wa subira ambao wafanyakazi walikuwa wamekosa kwa mtoto wake mwenye tatizo la usonji.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji na rais wa ofisi ya utalii alipotembelea mji wa Mesa kusini ya kati mwa Arizona, aliapa kurudi kuhakikisha wasafiri wa aina mbalimbali za matatizo ya neva waliotembelea jiji hilo watakuwa na uzoefu bora zaidi katika safari yao kuliko safari ilivyokuwa kwa familia yake.
Kwa kweli, kusafiri kunaweza kuwa na mfadhaiko sana kwa watu wa aina mbalimbali za neva hivi kwamba 87% ya familia zenye watu wenye tatizo hili hazichukui likizo, kulingana na utafiti wa Autism Travel.
Uzito unahusisha mchakato mzima hadi usafiri - ikiwa ni pamoja na kelele za kupita kiasi, na usumbufu katika utaratibu ikiwa mgonjwa hatadhibitiwa na kushughulikiwa kwa huruma.
Lakini miji kama vile Mesa hatimaye unatoa mafunzo na vifaa vya ufikiaji wa sehemu mbali mbali ili kila mtu aweze kufurahia safiri yake.
Kama sehemu ya kuanzia, Garcia alifanyia kazi kupata ofisi nzima ya utalii na kupata mafunzo na kuthibitishwa na shirika la IBCCES, ambalo linafanya kazi ya kutoa mafunzo ya matatizo ya utambuzi na uthibitisho kwa wataalamu ili waweze kuwa na vifaa sahihi na elimu ya kuwezesha watu wenye matatizo ya neva katika mazingira tofauti.
Kwa biashara kama vile hoteli, mikahawa na vivutio mbali mbali, hii inamaanisha kuwa wafanyikazi wamefunzwa kuelewa tatizo la usonji ni nini, jinsi ya kuelewa watu wenye usonji, changamoto wanazopitia na uwezekano wa kuwa na hisia za kawaida, na jinsi ya kuwasiliana nao kwa ufanisi zaidi.
Mnamo mwaka wa 2020, mtoto mmoja kati ya 36 aligunduliwa kuwa na hali ya usonji nchini Marekani, kulingana na Vituo vya Kudhibiti Magonjwa, na Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria mtoto mmoja kati ya 100 ana hali ya usonji duniani kote, idadi ambayo inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka, na kuifanya kuwa ya haraka zaidi kuongezeka duniani.
Pamoja na kushiriki takwimu na elimu kuhusu usonji, mafunzo ya shirika la IBCCES pia yanatoa mwongozo wa vitendo kuhusu njia za kuwashughulikia vyema watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ya neva.
"Kwa mfano, baadhi ya watu hujifunza zaidi katika kiwango cha mwonekano, ili kuweza kuwashughulikia zaidi kupitia vipeperushi, vijitabu na ramani," alisema Zoey Shircel wa Visit Mesa, na mtaalamu wa usafiri wa wenye tatizo la usonji aliyeidhinishwa.
Anasema pia kwamba ilimfundisha kuwa watu wengine wanaweza kuhitaji muda zaidi wa kuchukua habari, kama vile kivutio kilipo au ni nini cha kufanya.
Mafunzo hayo yalimfungua macho kuona ni wasafiri wangapi wanaweza kukabiliana na changamoto zisizoonekana.
"Kabla ya kuthibitishwa sikugundua watu ambao wanaweza kuwa na ulemavu uliojificha," alisema.
"Lakini baada ya kujifunza kuhusu uthibitisho huo, watu zaidi wako wazi kuzungumza kuhusu kile wanachoweza kuhitaji au ni msaada gani wa ziada tunaweza kutoa, bila kuwa na hofu au aibu."
Mesa lilikuwa jiji la kwanza nchini Marekani kupitisha mpango wa Hidden Disabilities Sunflower mwaka wa 2021, ulioanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, huku ofisi ya utalii ikitoa vivutio vingine kama bangili za alizeti bila malipo kwa wageni.
Baada ya kuona mafanikio ya uhakiki wa vyeti katika ofisi ya utalii, jiji zima la Mesa lilielewa thamani ya kujumuisha kila mmoja na kuanza kufanya kazi ya kupata 80% ya wafanyikazi wanaowasiliana na umma moja kwa moja - wakiwemo wafanyikazi wa mbuga na burudani, polisi na maafisa wa usalama wa umma na wazima moto - kuhakikisha wamefunzwa na pia kuwa na Kituo rasmi cha Udhibiti wa Autism (CAC).
Mnamo Novemba 2019, jiji hilo likawa jiji la kwanza la Udhibiti wa Usonji ulimwenguni, na ofisi zingine za utalii na miji imeanza kufuata mkondo huo.
Mjini Mesa, zaidi ya biashara na mashirika 60 tofauti yamekamilisha mafunzo ya kuwa na Kituo rasmi cha Udhibiti wa Autism (CAC). Wageni wanaweza kuona matokeo ya hili katika maeneo kama vile Jumba la Makumbusho la Arizona la Historia Asili ambalo hutoa mwongozo muhimu wa athari za hisia za matunzo mbalimbali, ambayo yanaweza kufikiwa mtandaoni au kutazamwa katika kila mlango wa kwenye makumbusho.
"Makumbusho ni sehemu maalum ambapo watu huja kujifunza, kupumzika na kupata kumbukumbu na marafiki na familia," Alison Stoltman, naibu mkurugenzi katika jumba hilo la makumbusho alisema.
"Hata hivyo, angahewa zinazosisimua sana zinaweza kuwa kikwazo kwa baadhi, kuzuia ufikiaji wake."
Kwa Jennifer Hedgepeth, mratibu wa huduma za matukio katika Kituo cha Sanaa cha Mesa, mafunzo aliyopokea yalikuwa ya kibinafsi hasa kwa kuwa ana mtoto mwenye tatizo la usonji.
"Vipengele vingi vya mafunzo vilikuwa vitu ambavyo tayari nilijua, lakini ilikuwa vizuri kujifunza kuhusu baadhi ya mambo hayo kwa undani zaidi," alisema. "Pia ni vizuri sana kujua wafanyakazi wenzangu wote na jiji la Mesa wanapokea mafunzo sawa."
Ingawa maonyesho yanayoonyeshwa katika Kituo cha Sanaa cha Mesa yanaweza kutofautiana katika uhamasishaji wa hisia, kituo hiki hutoa malazi kama vile blanketi zenye uzani na vipokea sauti vinavyobanwa kichwani vinavyoweza kusaidia wakati wa onyesho, pamoja na nafasi zenye utulivu iwapo mtu atahitaji muda wa kutoka nje.
"Ikiwa unasafiri kwenda nchi ya kigeni na hauongei lugha hiyo, kujua kuwa unaweza kupata mtu kama mkalimani kunaweza kukusaidia kupitia uzoefu wako kwa njia bora," Hedgepeth alisema." Ikiwa watu wanakuja kutembelea kwenye nafasi yako ya utendaji, wanapaswa kuhisi kuwa na raha na usalama."
Mji wa Mesa pia hutumika kama lango la kuingilia, kwa kuwa inapakana na Msitu wa Kitaifa wa Tonto ulio karibu.
Ndani ya mipaka ya jiji, Mbuga za Mesa na Wilaya ya Burudani (pia kituo cha CAC iliyoidhinishwa) hutoa huduma zinazoweza kufikiwa.
Ili kutoa njia ya kuingiliana na vivutio na mikahawa ambayo ni rafiki kwa wenye tatizo la usonji kote jijini, Visit Mesa imeweka pamoja na Autism GeoTour inayofanya familia na wageni kufichua maeneo yaliyofichwa yanayoweza kufikiwa hata na wenye tatizo la sonji.
Ingawa imepiga hatua kubwa katika ufikiaji, mji wa Mesa hauko tayari kupunguza kasi wakati wowote hivi karibuni, ikiweka lengo la kuwa jiji linalofikika zaidi duniani na wenye matatizo ya neva.