Mjasiriamali wa teknolojia anayelipa mamilioni ya dola 'kurejesha nyuma' umri wake

Iliyochapishwa

''Kibiolojia, nimekula chumvi kiasi cha haja. Sikio langu la kushoto ni la mtu wa miaka 64 na ukaguzi wa ubora wake unasema nina miaka 18. Mapigo ya moyo wangu ni wa mtu wa miaka 37 na uwezo wangu wa kupumua vyema ni wa kijana miaka 18.''

Hii ni kauli ya mjasiriamali wa teknolojia Bryan Johnson ambaye anatumia mamilioni ya dola kwa mwaka kujaribu kurejesha nyuma umri wake halisi wa kibiolojia.

Muonekano wa mwili wake hauendani na miaka aliyoishi duniani.

''Nasema kwa utani kwamba nataka kuwa kama kijana wa miaka 18. Mwanangu wa kiume ana umri wa miaka 17, kwa hivyo kila wakati namtania nikimwambia: ''Nitakapokuwa mdogo nataka kuwa kama wewe''.

''Laiti tungepunguza umri wa uzee na hata kuubadilisha, tungebadilisha maana ya kuwa binadamu,'' Brayan anaongeza.

Kundi la wataalamu linaojumuisha madaktari 30 na wanasayansi linamfanyia Byan vipimo vya mara kwa mara na kumtibu.

''Nilikuwa nikiamka mara kwa mara usiku kwenda msalani, lakini nilipofanya hivyo nilipata usingizi wa hali ya chini. Kwa hivyo tulinunua mashine iliyonisaidia kuimarisha utendakazi wa kibofu changu mkojo ili nisiamke usiku kwenda chooni. Na ilifanya kazi.''

Bryan pia anasema madaktari wake wametumia karibu miaka 22 kubadilisha umri wa ngozi yake.

Mashine inayofanya kazi hiyo inapiga picha kadhaa za muonekano wa uso wake na kutoa karibu ripoti 10 za zinazonesha ukubwa wa pua yako na uso mzima kwa ujumla.

''Msikio yangu pia yana hitilafu kidogo kwa hivyo tunatumia mashine maaluma ya kushughulikia hilo,'' aliambia BBC.

Anasema mashine hiyo inasaidia kufuatilia mara kwa mara uwezo wake wa kusikia.

''Tunafanya teknolojia ya ufufuaji, kujaribu kuboreaha usikivu wangu tena’’.

Bryan anasema juhudi hizo hazijapata ufanisi wa kuridhisha lakini anajitahidi kufikia lengo lake ijapoku anakiri sio rahisi.

Mjasiriamali huyo hata hivyo anafurahia kuona hatua aliyopiga katika mpango wake huo usio kuwa wa kawaida.

''Ni watu wachache wamevutiwa na jambo hili hasa watafiti kwani ni mwanzo mpya wa kuendeleza pale nitakapofikia. Lakini pia kuna wale walionikosoa sana. Hata hivyo nawapenda.’’

Daktari Jordan Shlaine, muanzilishi wa kliniki ya kibinafsi anasema haelewi kwa nini watu wanafanya mzaha na afya yao.

''Ikiwa ni salama na haifai kama vitamini au baadhi ya vitamini utakuwa unacheza kamari na pesa zako. Lakini kama haijathibitishwa kuwa salama utakuwa unahatarisha maisha yako,’’ aliongeza Dkt Shlaine.

Brayan kwa upande wake anakubaliana na wale wanaohoji kile ninachofanya lakini anasisitiza- ‘’Tunafanya hili kwa kuzingatia umakini wa hali ya juu kwa sababu tunafanya vipimo vya kila aina kwa ushauri wa kitaalamu.’’

Daktari Eric Verdin,Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya The Buck anadhani Brayan ni mwanzilishi wa kweli. Kuna wasiwasi na bila shaka tunasubiri kuona kutakachotokea.

Kwa sasa vipimo vyake vinaonyesha anaendelea vyema na anadai kuridhishwa navyo.