Tazama: Droni zawapelekea maji waliokwama katika mafuriko Ukraine

Tazama: Droni zawapelekea maji waliokwama katika mafuriko Ukraine
Iliyochapishwa

Jeshi la Ukraine limetoa picha za video zinazoonyesha ndege zisizo na rubani zikitoa chupa za maji kwa watu waliokwama kutokana na mafuriko katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi katika eneo la Kherson.

Maji kutoka katika bwawa la Kakhovka lililoharibiwa yamelifunika eneo hilo na kusababisha maelfu ya watu kutoroka makaazi yao huku kukiwa na maafa ya kibinadamu.