Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 15.03.2024
Manchester City wameamua kuahirisha mazungumzo ya kumpa mkataba mpya kiungo wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 32, ambaye amebakiza zaidi ya mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa. (Football Insider)
Manchester City wanatazamiwa kumsajili kinda mzaliwa wa Ufaransa Timeo Whisker, 15, kutoka Cardiff City kwa takriban £250,000. ( Athletic -Usajili unahitajika)
Chelsea wanahofia kuwa watamkosa mchezaji wa Napoli, Victor Osimhen, 25, katika uhamisho wa majira ya joto, huku Paris St-Germain na Arsenal zikiongeza juhudi katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji huyo mahiri wa timu ya taifa ya Nigeria. (Teamtalk).
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 26, hatarajiwi kuhamia PSG msimu huu wa joto kufuatia ripoti kwamba Muingereza huyo atachukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25. (Sky Sports).
Getafe hawataweza kuwa na Mason Greenwood zaidi ya muda wake wa mkopo kwani Manchester United wameamua kumuuza mshambulijai huyo wa Uingereza, mwenye umri wa miaka 22. (Marca kwa Kihispania)
Aston Villa wana imani kuwa wataweza kumbakisha kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz licha ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Arsenal. (90 Min)
Meneja wa England Gareth Southgate amefichua kuwa amekiambia Chama cha Soka kufanya mazungumzo kuhusu mustakabali wake hadi baada ya Euro 2024. (Mirror).
Mchezaji wa zamani wa Manchester City na kocha wa sasa wa Saudi Arabia Roberto Mancini analengwa na Newcastle United iwapo wataamua kuchukua nafasi ya Eddie Howe msimu huu wa joto. (HITC)
Newcastle wanataka kuharakisha kuondoka kwa Dan Ashworth kwenda Manchester United huku mkurugenzi wa michezo wa Monaco Paul Mitchell akiongoza orodha fupi ya wagombea kuchukua nafasi yake. (Telegraph - usajili unahitajika)
Chelsea wana nia ya kumnunua beki wa kati wa Lille Mfaransa, Leny Yoro, 18, wakati wa majira ya kiangazi, huku wakipima nafasi ya beki wa Brazil Thiago Silva, 39. (Standard).
Manchester United, Chelsea na Arsenal wanavutiwa na kijana wa Barcelona na Uhispania Pau Cubarsi, 17. (Football Espana)
Newcastle United na Arsenal wameimarika katika harakati zao za kumtafuta beki wa kati wa Sporting Lisbon Ousmane Diomande, 20, huku Chelsea wakihitaji kuuza wachezaji kabla ya kuthibitisha kuwasili kwa wachezaji wapya msimu huu. (Football Insider)
Santos inaamini kuwa mshambuliaji wa Al-Hilal wa Brazil Neymar, 32, atajiunga tena na klabu yake ya kwanza kabla ya kumalizia soka lake. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
PSV Eindhoven wanatarajia kusajili beki wa pembeni Sergino Dest, 23, na kiungo wa kati Malik Tillman, 21, kwa mikataba ya kudumu msimu huu wa joto huku wawili hao wa Marekani wakiwa wamevutiwa na mikataba ya mkopo kutoka Barcelona na Bayern Munich mtawalia. (ESPN)
Shirikisho la soka nchini Uhispania limefahamisha Chama cha Soka cha Uingereza kuwa wanataka kumchagua mshambuliaji wa Leeds United mwenye umri wa miaka 20 Mateo Joseph, mchezaji wa kimataifa wa Uingereza chini ya umri wa miaka 20, kwa ajili ya michezo ijayo ya timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 21. (AS - kwa Kihispania)
Kiungo wa zamani wa Everton na Iceland Gylfi Sigurdsson, 34, amejiunga na klabu ya Valur ya Iceland baada ya kukaa zaidi ya miezi sita na klabu ya Lyngby ya Denmark. (Talksport)
FA inapanga kuendelea mbele kwa mipango ya kufuta mechi za marudiano za Kombe la FA kutoka kwa raundi ya tatu msimu ujao. (Mail)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi