Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 01.01.2024
Manchester City wamekubali mkataba wa kumsaini kiungo wa kati wa River Plate na Argentina, Claudio Echeverri kwa kandarasi ya miaka sita, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 atasalia na klabu hiyo ya Amerika Kusini hadi Desemba 2024. (Fabrizio Romano).
Manchester United wameamua kutoongeza mkataba wa Raphael Varane kwa miezi 12 zaidi, ikimaanisha kuwa beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30 anaweza kufanya mazungumzo na vilabu vingine kuhusu uhamisho kuanzia Januari 1. (Mail)
Leicester wanataka kumsajili winga wa Liverpool, Fabio Carvalho kwa mkopo baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno chini ya umri wa miaka 21, kuondolewa kwa mkopo katika klabu ya RB Leipzig. (Sky Sports)
Liverpool wametuma mawakala kumtazama winga wa zamani wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Michael Olise, 22, mzaliwa wa Crystal Palace, Uingereza katika wiki za hivi karibuni. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Senegal, Pape Matar Sarr, 21 - ambaye alipata majeraha wakati wa mchezo wa Jumapili dhidi ya Bournemouth akiwa na tatizo la misuli ya paja - anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu. (Athletic)
Monaco wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Ujerumani Thilo Kehrer, 27 kutoka West Ham. (Fabrizio Romano)
Juventus, Nice na timu kadhaa za Ligi Kuu ya Uingereza zinavutiwa na winga wa Atalanta, Muingereza Ademola Lookman, 26. (Mail)
West Ham wana nia ya kuinasa saini ya Montpellier, kwa mshambulizi wa Nigeria Akor Adams mwezi Januari lakini klabu hiyo ya Ufaransa inasita kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka katikati ya msimu. (Football Insider)
Sheffield United wanataka kumsajili golikipa kwa mkopo mwezi Januari, huku golikipa wa kimataifa wa Anderlecht wa Denmark, Kasper Schmeichel, ndiye anayepigiwa mahesabu. (Sun)
Brentford wametoa dau la euro milioni 25 (pauni milioni 21.6) kumnunua winga wa Real Betis mwenye umri wa miaka 18 Mhispania, Assane Diao. (Mundo Deportivo)
Southampton wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Burnley na Ubelgiji, Manuel Benson, 26. (Echo Daily)
West Ham wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja Vladimir Coufal, lakini beki huyo wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 31 anataka mkataba mrefu zaidi. (Sun)
Eintracht Frankfurt wanakaribia kukubali mkataba wa mkopo na Wolves kwa mshambuliaji wa Austria mwenye umri wa miaka 26 Sasa Kalajdzic. (Bild)
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah