'Hii ndiyo ndoto' - unachohitaji kujua kuhusu fainali ya Ligi ya Mabingwa

Erling Haaland na Romelu Lukaku
Maelezo ya picha, Erling Haaland na Romelu Lukaku
Iliyochapishwa

Manchester City wanapania kushinda Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza na kukamilisha Treble (kushinda mataji matatu kwa mpigo) watakapocheza dhidi ya Inter Milan katika fainali itakayogaragazwa katika Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk mjini Istanbul.

Kikosi cha Pep Guardiola tayari kimeshinda Ligi Kuu na Kombe la FA.

Ni mara ya pili ndani ya miaka mitatu City kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kushindwa na Chelsea msimu wa 2020-21.

"Tunahitaji tu kutafuta njia ya kushinda la kwanza," mchezaji wa City Kevin de Bruyne aliiambia BBC Radio 5 Live.

"Tukifanikiwa kufanya hivyo, itakuwa fahari kubwa kwa wachezaji, klabu na mashabiki."

Manchester United ndio timu pekee ya Uingereza iliyowahi kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa na kufikia mafanikio hayo msimu wa 1998-99.

City wanatinga fainali Jumamosi wakiwa katika hali nzuri wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 26 zilizopita katika mashindano yote na pia kutofungwa barani Ulaya msimu huu, wakishinda mechi saba kati ya 12.

Guardiola anasaka taji la Uropa kwa mara ya kwanza tangu ashinde taji hilo mwaka 2011 akiwa na Barcelona, ​​ambayo pia aliisaidia kushinda mataji matatu miaka miwili iliyopita.

Kimsingi, kikosi chake cha City kinaonekana kuwa kikali zaidi kuliko kile cha Barcelona mnamo 2008-09 - Barca, ambao walipoteza mara moja kwenye fainali, walifunga mabao 32 na kufungwa 13 msimu huo huku City, wakisalia na mechi moja, wamefunga mabao 31 mpaka sasa na kufungwa matano pekee.

Alipoulizwa kuhusu mafanikio yake, Guardiola alisema: "Nilikuwa na [Lionel] Messi siku za nyuma na [Erling] Haaland sasa. Haya ni mafanikio yangu. Sifanyi mzaha, huo ndio ukweli wa mambo."

Inter, chini ya Jose Mourinho, iliiondoa Barcelona ya Guardiola katika nusu fainali ikiwa ni njia ya kushinda mataji matatu pekee yake mwaka 2010, lakini hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Waitaliano hao kukutana na City.

"Huu ndio mwisho. Ligi ya Mabingwa ni mashindano ya ajabu," aliongeza Guardiola. "Ni fahari kubwa.''

Inter wanawania taji la nne la Uropa

Wachezaji wa Inter

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Manchester City ndio wanapigiwa upatu zaidi kushinda dhidi ya mabingwa mara tatu wa Uropa, Inter, ambao walimaliza wa tatu kwenyeLigi ya Serie A na kushinda Coppa Italia kwa msimu wa pili mfululizo.

Inter, hata hivyo, haipaswi kupuuzwa, kwa kuwa wamecheza bila kushindwa mara nane katika mechi 12 hadi sasa, huku mlinda mlango Andre Onana akiwa ndiye mchezaji wao bora.

Kikosi cha Simone Inzaghi pia kina uwezo mkubwa katika safu yake ya mashambulizi. Wakiongozwa na Lautaro Martinez, ambaye amefunga mabao 28 na kusaidia kufunga mabao 11 katika mechi 58 msimu huu, Waitaliano hao pia wana mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko na Romelu Lukaku - ambaye hajaanza mchezo wowote barani Ulaya msimu huu.

"Hii ni mechi yangu muhimu zaidi haijawahi kutokea, lakini ninaamini hivyo ndivyo ilivyo kwa wachezaji wangu, kwa sababu tuna wachezaji kama Dzeko na Onana ambao wamecheza nusu fainali," Inzaghi alisema.

Mshambulizi wa Argentina Martinez aliongeza: "Natumai tutafanya vyema, kupata matokeo na hatimaye kupeleka kombe mjini Milan. Ni ndoto kubwa kwetu. Ni ngumu sana kutimiza lakini tumesalia na hatua moja.

Haaland anata kumwiga Ole wa United

Mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland amekuwa na msimu mzuri wa kwanza katika soka la Uingereza tangu ajiunge nayo akitokea Borussia Dortmund majira ya joto yaliyopita.

Amevunja rekodi ya Ligi Kuu ya England kwa mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja akiwa na mabao 36 na amefunga mara 52 katika michuano yote kwa kasi ya kufunga kila baada ya dakika 78.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Chama cha Waandishi wa Soka (FWA) na anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo za mchezaji bora na mchezaji chipukizi wa Ligi Kuu katika msimu huo huo.

Haaland anatamani sana kuongeza Ligi ya Mabingwa katika kabati lake la makombe na uwiano wa dakika kwa kila bao kwenye shindano hilo umefikia dakika 63, kwa muda wote akiwa na City, Dortmund na Red Bull Salzburg.

Alishindwa kufunga katika nusu fainali, lakini mabao yake 12 yanasalia kuwa mabao mengi zaidi katika msimu wa Ligi ya Mabingwa kwa klabu ya Uingereza pamoja na Ruud van Nistelrooy kwa Manchester United mnamo 2002-03.

Alipoulizwa kama alikuwa na wasiwasi kuhusu Haaland kushindwa kufunga mabao, Guardiola alijibu: "Ikiwa una shaka kuhusu Erling Haaland kufunga mabao, wewe ni mtu mpweke sana.

Haaland anatazamia kuwa raia wa Norway wa kwanza kufunga bao kwenye fainali tangu Ole Gunnar Solskjær, ambaye bao lake liliiwezesha United kushinda Treble mnamo 1999.

"Hii ndiyo sababu walininunua bila shaka, ili kupata huu ushindo, hatupaswi kuficha hilo," Haaland alimwambia mhariri wa michezo wa BBC Dan Roan.

"Nitafanya kila niwezalo kufikia azama hiyo. Ni ndoto yangu kubwa na natumai ndoto zitatimia."

Safari ya Manchester City kuelekea fainali

Erling Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Erling Haaland alifunga mabao 12 ya katika Ligi ya Mabingwa msimu huu ni manne zaidi ya mchezaji wa pili katika orodha ya wafungaji bora, Mohamed Salah wa Liverpool.

Manchester City walitinga hatua ya makundi, wakimaliza bila kushindwa kileleni mwa Kundi G na pointi tano mbele ya Borussia Dortmund walio nafasi ya pili.

Kikosi cha Guardiola kilishinda michezo yake yote kwenye Uwanja wa Etihad, huku kikiichapa Sevilla nyumbani na ugenini kutinga hatua ya mtoano.

Katika hatua ya 16 bora walikutana na RB Leipzig ya Ujerumani, kwa mara nyingine tena wakiangazia nguvu zao nyumbani kwa kichapo cha 7-1 - ambapo Haaland alijisaidia kufunga mabao matano - kusonga mbele kwa jumla ya 8-1.

Robo-fainali ilishuhudia Manchester City ikitoka sare na timu ya zamani ya Guardiola, Bayern Munich. Ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza uliihakikishia City kuwa na mguu mmoja katika nusu fainali. Kisha wakapata sare ya 1-1 huko Ujerumani ili kuendelea na kampeni yake.

Nusu fainali hiyo ilishuhudia City wakikabiliana na mtihani wao mgumu zaidi kufikia sasa kwani walicheza na mabingwa mara 14 Real Madrid. Mechi ya kwanza nchini Uhispania ilimalizika kwa sare ya 1-1 kabla ya City kufanya vyema katika uwanja wao wa nyumbani kuibuka tena waliposhinda 4-0 na kutinga fainali.

Safari ya Inter Milan kuelekea fainali

Vichapo viwili kutoka kwa mechi sita za makundi viliifanya Inter Milan kumaliza katika nafasi ya pili katika Kundi C nyuma ya Bayern Munich lakini wakamaliza mbele ya Barcelona baada ya kuwalaza 1-0 nyumbani na kisha kutoka sare ya 3-3 nchini Uhispania.

Katika hatua ya mtoano walishinda Porto na Benfica na kuanzisha mchezo wa nusu fainali na wapinzani wao wa jiji AC Milan.

Mabao mawili katika dakika 11 za kwanza yaliwafanya kuongoza kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza na baadaye kushinda 1-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0.

Tangu enzi ya Ligi ya Mabingwa ilipoanza 1992-93, ni timu ya nne kutinga fainali baada ya kupoteza mchezo wao wa ufunguzi - kufuatia AC Milan msimu wa 1994-95, Bayern Munich mnamo 1998-99 na Tottenham 2018-19, na zote zilifungwa katika fainali.