Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 09.03.2024

Iliyochapishwa

Newcastle wamejadili uwezekano wa kumsajili Pedro Neto kutoka Wolves msimu huu, kwa dau la takriban £60m inayodhaniwa kuwa inatosha kumsajili winga huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 - ingawa Liverpool pia wanamtaka. (Mail)

Tottenham wameanza mazungumzo na nahodha Son Heung-min kuhusu mkataba mpya na wana imani kwamba makubaliano na mshambuliaji huyo wa Korea Kusini, 31, yatakamilika msimu huu. (Football Insider)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes amezungumza na wanafamilia wa mshambuliaji wa Bournemouth Muingereza Dominic Solanke mwenye umri wa miaka 26 kuhusu uwezekano wa kuhama msimu ujao. (Football Transfers)

Vilabu vya Saudi Pro League vimejiandaa kutoa zaidi ya pauni milioni 100 kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin De Bruyne, 32, kutoka Manchester City. (Football Insider)

Arsenal , Manchester United , Newcastle na Chelsea zote zinaonyesha nia ya kumnunua beki wa kushoto wa Borussia Monchengladbach Mjerumani Luca Netz, 20. (HITC).

Bayern Munich wamemuongeza meneja wa Brighton Roberto de Zerbi kwenye orodha fupi ya warithi wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel mwishoni mwa msimu huu lakini kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso, ambaye pia anasakwa na Liverpool, anasalia kuwa chaguo la kwanza la klabu hiyo. (Mirror)

Chelsea ni moja ya vilabu kadhaa vinavyomfuatilia winga wa Athletic Bilbao Mhispania Nico Williams, 21. (ESPN)

Michael Edwards anakaribia kukubaliana juu ya nafasi ya juu na wamiliki wa Liverpool Fenway Sports Group, ambayo itajumuisha mtendaji mkuu wa zamani wa Reds kuchukua udhibiti wa shughuli za kandanda za kilabu. (Athletic - subscription required)

Chelsea wako tayari kukubali ofa kutoka kwa Roma kwa Romelu Lukaku, 30, ambayo ni chini ya chaguo la pauni milioni 37 la kununua lililojumuishwa katika mkataba wa mkopo wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji. (Calcio Mercato, via Team Talk)

West Ham wanaweza kumlenga kiungo wa kati wa Arsenal Mwingereza Emile Smith Rowe, 23, katika dirisha la usajili. (Caught Offside)

Arsenal wanamfuatilia beki wa Brazil Douglas Mendes, 19, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Red Bull Bragantino kutoka Red Bull Salzburg. (Football Transfers)

The Gunners na Newcastle United wanavutiwa na beki wa kati wa Sporting Lisbon Ousmane Diomande lakini vilabu vyote viwili vinasubiri kuona kama Chelsea watatoa dau la pauni milioni 69 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 20. (TeamTalk)

Beki wa Uingereza Jamaal Lascelles, 30, ameanzisha mazungumzo ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Newcastle. (Chronicle)