Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hekalu la Kishetani: "Dini" inayotaka kupinga ushawishi wa makundi ya kidini nchini Marekani
Katika chumba kilichowashwa mishumaa kilichohifadhiwa kwa sherehe za kishetani , ishara ya neon inakukaribisha katika eneo La petite Chapelle Noire. Katika upande mmoja wa chumba ni madhabahu na katika mbele ya sakafu ni pentagram. Matambiko yanayofanyika hapa ni ubatizaji ambapo washiriki walikataa kubaatizwa wakati walipkuwa Watoto.
‘’Hakuna majina’’, anasema mmoja ya waliohudhuria ambaye ameniruhusu kuhudhuria sherehe hiyo bora tu nisiwatambue.
Huvalia kofia ndefu na barakoa . Mikono yake imefungwa kwa kamba , ambayo hufunguliwa kuonesha uhuru wao. Kurasa kadhaa hukatwa kutoka kwa biblia ili kuonesha ishara ya kufutiliwa mbali kwa ubatizo wake wa kuwa mkristo.
Kwa kweli tukio hilo lilikuwa kubwa kwake.
‘’Kwa kuwa ni mtoto wa mapenzi ya jinsia moja na ambaye alikuwa chukizo na alihitaji kubadilishwa ni swala lililoniathiri . Ufuasi wangu wa hekalu la shetani ulinisaidia kukumbatia ukweli na kuwa mwenye huruma’’.
Hekalu la shetani linatambuliwa kama dini na serikali ya Marekani na lina mawaziri na wafuasi wake nchini Marekani, Ulaya na Australia.
Zaidi ya watu 830 walinunua tikiti za mkutano wake uliofanyika mwishoni mwa Aprili, unaoitwa SatanCon.
Wanachama wa kikundi hiki wanasema hawaamini kabisa kuhusu shetani au Kuzimu.
Badala yake, wanadai Shetani ni sitiari ya kutilia shaka mamlaka na kutegemeza imani yao katika sayansi. Wanasema hisia ya jumuiya inayozunguka maadili haya ya pamoja yanaifanya kuwa dini.
Wanatumia alama za Shetani kufanya matambiko, kama vile wakati wa kufanya harusi au kupewa jina jipya. Hii inaweza kujumuisha kuwa na msalaba wa neon uliopinduliwa chini kwenye madhabahu yako unapopaza sauti, "Shikamoo Shetani!"
Kwa Wakristo wengi, hii ni kufuru mbaya sana.
"Si vibaya," anakubali Dex Desjardins, msemaji wa hekalu la shetani. "Picha zetu nyingi ni za kukufuru."
"Tuna watu wanaobeba misalaba juu chini. Na sherehe yetu ya ufunguzi ilijumuisha kuraruliwa kwa Biblia kama ishara ya ukandamizaji, hasa ukandamizaji wa watu na wanawake wa LGBTQ.
Pia kutoka kwa jumuiya ya BIPOC (kifupi cha watu Weusi, Wenyeji, na Watu wa Rangi), na karibu mtu yeyote ambaye alikua na kiwewe cha kidini, ambayo ni idadi kubwa ya washiriki wetu."
Wafuasi wa Shetani wanasema wanaheshimu haki ya kila mtu ya kuchagua imani yao na hawajaribu kuwaudhi wengine.
Wakati wa hafla ya ufunguzi ya SatanCon, kurasa zillikatwa kutoka kwa biblia, na hivyo kuzua ukosoaji mkubwa mtandaoni.
Lakini waandamanaji wa Kikristo wa imani nyingi walikusanyika nje ya hoteli hiyo, wakiwa na mabango ya kuonya kwamba watalaaniwa.
“Tubuni na kuiamini Injili,” inahimizwa. "Shetani anatawala Watoto wote wa Kiburi," unasema ubao mwingine wa matangazo ambamo herufi "kiburi" zimetiwa kivuli na rangi za upinde wa mvua za bendera ya LGBTQ.
Waumini wa Kikristo waliandamana nje ya hoteli ambako kongamano la kishetani lilikuwa likifanywa.
“Tunataka kumwonyesha Mungu kwamba hatukubali kufuru hii na kwamba Wakatoliki hawajawaacha waumini wake kwa Wafuasi wa Shetani,” alisema Michael Shivler, mwandamanaji kutoka kikundi cha Kikatoliki chenye msimamo mkali.