Faida za kushangaza za mikunjo ya ngozi ya vidole kwenye maji

Chanzo cha picha, Getty Images
Unatumia dakika chache kuoga msalani ama hata katika kidimbwi cha maji utagundua kwamba kuna mabadiliko makubwa katika mikono yako.
Utagundua kwamba katika mikono yako au wayo wako wakati ambapo kulikuwa na mikunjo michache ya ngozi yako unapoingia katika maji mikunjo hiyo inaongezeka.
Mabadiliko hayo yasio ya kawaida yanashangaza kwa kweli.
Ni ngozi yetu iliopo katika vidole vya mkononi na mguuni inayokunjana inapoingizwa katika maji huku shemeu zingine za mwili ikiwemo mikono,miguu na uso ukisalia kuwa nyororo zinapoingia katika maji.
Hali ya mikunjo hiyo katika ngozi ya vidole vyetu imewashangaza wanasayansi wengi kwa miongo kadhaa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wengi wametaka kuelewa ni nini kinachosababisha mikunjo hiyo , lakini zaidi hivi karibuni swali ni kwanini , na nini lengo lao linavutia watafiti.
Lakini inaweza kuvutia zaidi kuhusu kinachoweza kugundulika katika afya yetu.
Mikunjo
Huchukua sekunde 3.5 katika maji ya hali ya nyuzi joto ya 40 kwa vidole vyako kuanza kukunjana , huku katika nyuzi joto za baraidi za 20 inaweza kuchukua dakika 10.
Utafiti mwingi imebaini kwamba unapoweka vidole vyako kwa zaidi ya dakika 30 unaweza kupata mikunjo mingi zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Iliaminika kwamba mikunjo iliopo katika vidole vyako It was lilikuwa jibu ambalo tabaka za juu za ngozi zilivyonza maji yaliofurika ndani ya seli kupitia mchakato unaojulikana kama osmosis : mchakato ambao molekyuli za maji huvuka utando ili kusawazisha mkusanyiko wa miyeyusho katika pande zote mbili za membrane yenyewe.
Lakini mapema mwaka 1935, wanasayansi walishuku kwamba kulikuwa na kitu zaidi ya mchakato huu wote.
Madaktari waliokuwa wakichunguza wagonjwa walio na majeraha ambayo neva ya wastani (moja ya mishipa mikuu inayopita kwenye mkono na kushuka chini hadi mkononi) ilikuwa imekatwa waligundua kuwa vidole vya wagonjwa havikuwa na mikunjo ndani ya maji.
Miongoni mwa majukumu yake mengi, neva ya wastani husaidia kudhibiti kinachojulikana kama kama vile kutokwa na jasho na kubanwa kwa mishipa ya damu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ugunduzi huo ulipendekeza kuwa hatua ya kukunja ya vidole ndani ya maji ilidhibitiwa na mfumo wa neva.
Usambazaji wa damu
Tafiti zaidi za madaktari katika miaka ya 1970 zilitoa ushahidi zaidi kuhusu ugunduzi huu, na ilipendekeza kutumia kuzamishwa kwa mikono ndani ya maji kama mtihani rahisi kutathmini kiwango cha aina ya uharibifu wa neva ambao unaweza kuathiri udhibiti wa michakato.
Kisha, mwaka wa 2003, madaktari wa neva Einar Wilder-Smith na Adeline Chow, waliokuwa wakifanya kazi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kitaifa huko Singapore wakati huo, walipima mzunguko wa damu wa mikono ya watu waliojitolea iliyotumbukizwa ndani ya maji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Waligundua kuwa ngozi kwenye ncha za vidole ilipoanza kukunjana, mtiririko wa damu kwenye vidole ulipungua.
Walipotumia krimu ya kienyeji ya ganzi ambayo ilisababisha mishipa ya damu kwenye vidole kubana kwa muda, waligundua kuwa viwango sawa vya mikunjo vilitokea kama wakati wa kuzamishwa ndani ya maji.
"Inaleta maana unapozingatia vidole vyako vinapokunjana," anasema Nick Davis, mwanasayansi wa neva na mwanasaikolojia katika Chuo Kikuu cha Manchester Metropolitan ambaye amechunguza jinsi vidole vinavyokunjana.
"Ncha za vidole vinageuka rangi na ni kwa sababu mkazo wa mishipa yad amu unapunguza usambazaji wa damu kutoka juu ya sakafu ya ngozi."
lakini kwanini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa usaidizi wa watu 500 wa kujitolea waliotembelea Jumba la Makumbusho la Sayansi huko London mnamo 2020, Davis alipima kiwango cha nguvu kinachotumiwa na kushika kitu cha plastiki.
Labda haishangazi, wale walio na mikono mikavu, isiyo na mikunjo walipaswa kutumia nguvu kidogo kuliko wale walio na mikono yenye maji, kwa sababu mshiko wa kitu uliimarika zaidi. Majibu yake yalikuwa wazi, alisema Davis "Mikunjo iliongeza msuguano kati ya vidole na kitu kilichoshikwa na mkono. Kinachovutia zaidi ni kwamba vidole vyetu vinaathiriwa na mabadiliko haya ya msuguano wa sakafu iliokamatwa na kwamba tunatumia habari hii kutumia nguvu kiasi wakati wa kukamata kitu kwa ili kiwe salama." .
Matokeo yao yanakubaliana na yale ya watafiti wengine, ambao wamegundua kwamba mikunjo kwenye vidole hurahisisha kushika vitu vyenye unyevunyevu.
Baadhi ya wanasayansi wamesema kwamba mikunjo kwenye vidole inaweza kufanya kazi kama michirizi kwenye matairi au nyayo za viatu.












