Kutana na mahali ambapo bia ndio kifungua kinywa maarufu na chenye heshima

Chanzo cha picha, Alamy
Maeneo mengi duniani yana utamaduni wake wa kipekee wa kifungua kinywa cha asubuhi. Huko Lyon, Ufaransa, ikifika saa tatu asubuhi ni utamaduni wao kupata mvinyo na vinywaji vingine.
Huko Van, Uturuki, ni kawaida kuona watu wakipata kifungua kinywa chenye mkusanyiko wa sahani mpaka tisa zenye mkusanyiko wa vitafunwa na vikorombwezo vingine.
Lakini hapa Bavaria, jimbo linalojulikana kwa mavazi yake ya kitamaduni na tafrija ya 'Oktoberfest', mila hii ya upishi huakisi kitu cha furaha zaidi huko.
Kinajulikana kama "Weißwurstfrühstück", kifungua kinywa cha jadi cha soseji-pretzel-na-bia kinaweza kuwa ndo mlo wa "Kijerumani" maarufu zaidi nchini humo.
Ilikuwa Jumamosi asubuhi huko Gaststätte Großmarkthalle, japo ni asubuhi lakini ilionekana kama Ijumaa usiku. Vyumba vilivyotengenezwa kwa mbao vilijaa watu na wahudumu waliokuwa wamevalia vizuri wakibeba trei za vinywaji na sauti zilikuwa zinaongezeka taratibu kadri muda ulivyozidi kwenda.
Kusini mwa Munich, ipo baa moja ambayo inakusanya umati wa watu kwa ajili ya kujipatia kifungua kinywa cha Bavaria: Weißwurstfrühstück ("kifungua kinywa cha soseji nyeupe"). Chakula hicho kina sausage nyeupe pamoja na pretzels laini ambacho huoshwa na kuandaliwa kwa kutumia bia.

Chanzo cha picha, Alamy
"Weißwurstfrühstück ni zaidi ya mlo; ni kinatumika kwenye mikutano isiyo rasmi wakati kahawa imechelewa lakini labda ni mapema sana kwa chakula cha mchana," anasema Frauke Rothschuh kutoka bodi ya utalii ya Munich, na kuongeza kuwa watu kwa kawaida huishia kukaa ili kufurahia anga na bia.
Ingawa vifungua kinywa vingine vinapatikana kote Munich, Gaststätte Großmarkthalle huwa ni cha tofauti na ni maarufu chenye heshima nchini humo.
Nyumba moja ya kulala wageni inayoendeshwa na ndugu wawili, kaka na dada, Ludwig Wallner na Gabi Walter, ambao walirithi biashara hiyo kutoka kwa baba yao mnamo 1999.
"Haijabadilika sana katika miaka 55 [familia yangu] imekuwa ikisimamia," Wallner aliniambia.
Wallner ndiye mmiliki pekee wa nyumba ya wageni katika jiji hilo ambaye pia bado anafanya kazi kama mchinja nyama. Huamka mapema kila asubuhi, hutengeneza soseji kwa mikono yake, akitumia ujuzi aliojifunza akiwa mtoto kwneye familia. Anapata viungo vyake kutoka wilaya ya karibu na soko kubwa la jumla (Großmarkthalle) lililo karibu.

Chanzo cha picha, Alamy
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katikati ya wiki, baa inapokea wafanyabiashara na wateja wengi kutoka sokoni. Mwishoni mwa wiki, meza kubwa zinachukuliwa na familia na marafiki, au zinajaazwa na makundi madogo ya wageni wanaosakaa kwa furaha "Servus!".
Ni mahali ambapo watu wa umri wote wanakwenda. "Baadhi ya siku zetu zenye shughuli nyingi zaidi ni wakati wa Oktoberfest au msimu wa kanivali," Wallner alielezea, "au siku ambazo moja ya timu za kandanda za Munich zinacheza."
Leo ni moja ya vyakula vinavyojulikana zaidi vya Bavaria, na moja ya mambo ya kwanza ambayo wenyeji watakuambia muhimu kujaribu. Kifungua kinywa hutumiwa katika jimbo lote la kusini, hasa Oberbayern (Upper Bavaria).
"Ni chakula ninachotumia na familia yangu mashambani," alisema Theresa Portenlänger, ambaye anaendesha baa ya kisasa ya Munich Xaver's pamoja na ndugu zake. "Siku zote huwa natumia Weißwurstfrühstück katika mkesha wa Krismasi."
Nilipomuuliza kuhusu wazo la kunywa bia asubuhi, alisema, "Nadhani watu wengi hapa hawaoni au hawachukulii kama kileo au pombe - wanaona ni chakula kama ilivyo mkate!".












