Vita vya Ukraine: Kipi kinahitajika kwa vikosi vya Ukraine kurudisha mapigo?

MIHAIL OSTROGRADSKI 35TH BRIGADE/ANADOLU AGENCY VI

Chanzo cha picha, Anadolu agency

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine kutoka 35th Brigade walichapisha picha, wakisema wanajeshi wake walikomboa tena kijiji cha Storozheve katika eneo la mashariki la Donetsk.
Iliyochapishwa

“Usiite ni kujibu mapigo,” wanasema Waukraini, “haya ni mashambulizi yetu, hatimaye hii ni nafasi yetu ya kuvitoa vikosi ya Urusi katika ardhi yetu.”

Sawa, kipi kinahitajika ili kushinda?

Awali ya yote, tusitatizwe na ushindi wa hivi punde, lakini Ukraine kuchukua eneo dogo, ni kama vile kuchukua huko hakuna uhakika; vijiji vilivyo hamwa Mashariki mwa Donetst na Kusini-Mashariki mwa mikoa ya Zaporizhzhia.

Baada ya miezi ya mkwamo, picha za ushindi, wanajeshi wa Ukraine waliotapakaa damu wamebeba bendera ya nchi ya rangi ya buluu na njano mbele ya jengo lenye matundu ya risasi; ni ukaribisho unaongeza ari kwa raia wa Ukraine. Lakini katika mtazamo mpana wa kimkakati, hili ni onyesho dogo.

Maeneo yanayoshikiliwa na Urusi ambayo yana umuhimu mkubwa katika vita hivi ni yale ya Kusini; eneo kati ya mji wa Zaporizhzhia na bahari ya Azov.

Kile kiitwacho ‘uchochoro wa ardhini’ unaounganisha Urusi na Crimea iliyoinyakua kinyume na sheria, sehemu ya katikati yenye ukanda wa rangi ya zambarau katika ramani ya chini, haijabadilika tangu wiki za mwanzo ya uvamizi wa Urusi mwaka jana.

Ikiwa Ukraine itaweza kuligawa sehemu mbili eneo hilo, na kudhibiti eneo itakalo lichukua, hapo itakuwa mashambulizi yamefaulu kwa sehemu kubwa.

Itavizuia vikosi vya Urusi upande wa Magharibi na kufanya kuwa ngumu kwao kupeleka mahitaji katika ngome ya Crimea.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Haitokuwa na maana ndio mwisho vita, ambavyo baadhi wanatabiri vitaendelea kwa miaka, lakini itaiweka Ukraine katika nafasi imara ya majadiliano, pale mazungumzo ya amani yasiyo-epukika yatakapo fanyika.

Lakini Urusi wameshaiangalia ramani, muda mrefu uliopita na kufikia hitimisho hilo hilo.

Wakati Ukraine inapelekea wanajeshi wake katika nchi za Nato kwa ajili ya mafunzo na kuvitayarisha vikosi vyake 12 kwa mapambano ya wakati wa kiangazi. Moscow imetumia wakati huo kujenga kile kinachoitwa kwa sasa, “ngome ya kutisha zaidi ulimwenguni ya ulinzi.”

Wamevizuia vikosi vya Ukraine visiende upande wa pwani wa nchi hiyo, pia tusisahau, safu ya mabomu ya Urusi ya ardhini, vifaru imara (vinavyojuulikana kama meno ya dragoni), mahandaki, maeneo ya kushambulia, mashimo mapana na marefu ya kuzuia kifaru cha Leopard 2 na M1 Abrams.

Hayo yote yameandaliwa kuendana na hali ya uwanja wa vita, ili kushambulia magari ya kivita ya Ukraine, wakati vikosi vya Ukraine na vifaa vyao wakisubiri wahandisi wao watafute njia ya kupita.

Dalili za awali zinaonesha, na bado ni mapema mno katika kampeni hii, kwamba ulinzi wa Urusi hadi sasa uko imara.

Ukraine bado haijatuma sehemu kubwa ya vikosi vyake, yanayoendelea ni mashambulizi ya uchunguzi na upelelezi, yaliyoandaliwa ili kufichua zilipo silaha za Urusi na kutafuta maeneo dhaifu katika upande wao.

Faida kwa Ukraine ni ari. Wanajeshi wake wana hamasa kubwa na wanapigana ili kukomboa nchi yao kutoka kwa wavamizi. Sehemu kubwa ya vikosi vya Urusi havina hamasa, katika mifano mengi; mafunzo yao, zana na uongozi ni duni kuliko upande wa Ukraine.

Magenerali wa Kijeshi katika mji mkuu Kyiv watakuwa na matumaini ikiwa watapata mafanikio ya kutosha, kupoteza ari kwa Urusi kutaendelea, na kuenea katika mstari wa mbele wa vita wakati vikosi visivyo na ari vitapoteza hamu ya kupigana.

Pia, faida nyingine waliyo nayo Ukraine ni ubora wa zana zao ambapo nchi za Nato wamewapa. Si kama vifaa vilivyotengenezwa wakati wa utawala wa Ki-Soviet, vifatu vya Nato na magari ya kivita vinaweza kuhimili shambulizi la moja kwa moja, au angalau kuweza kulinda timu iliyopo ndani.

.

Chanzo cha picha, Russia Dfence Ministry

Maelezo ya picha, Jeshi la Urusi linadai kwamba idadi ya vifaru vya Ukraine vilivyotolewa na nchi za magharibi na shehena za wanajeshi zimeharibiwa katika mapigano makali.

Je, hilo litatosha kupambana na nguvu za silaha za Urusi na mashambulizi ya droni?

Urusi ni nchi kubwa, ina rasilimali nyingi kuliko Ukraine. Rais Vladimir President, ambaye alianzisha hivi vita, anajua ikiwa ataweza kuidhoofisha Ukraine na kuiweka katika mkwamo, ambayo utafanya vita viingie katika

mwaka mwingine, kuna uwezekano Marekani na washirika wengine kuchoka kuunga mkono juhudi za vita vyenye gharama na wataanza kuilazimisha Kyiv kufikia makubaliano ya usitishaji wa mapigano.

Hatimaye, kutakuwa na ulinzi wa anga au kutokuwepo. Kushambulia maeneo ya adui yenye mashimo yaliyochimbwa vizuri bila ya msaada wa kutosha wa angani ni hatari kubwa.

Ukraine inajua hilo, ndio maana imeomba muda mrefu kwa Magharibi kuwapelekea ndege za kivita vya F 16.

Marekani ambayo inaziunda ndege hizo, haikutoa ruhusa hadi mwishoni mwa mwezi Mei, wakati ambao matayarisho ya awali ya mkondo wa kwanza wa mashambulizi ya Ukraine ulikuwa tayari umeshaanza.

Ndege za 16 ambazo ni muhimu kwa Ukraine na zinaweza kubadilisha hali ya mambo, zinaweza kuwasili zikiwa zimechelewa katika uwanja wa vita kwa ajili ya kufanya kazi muhimu - mwanzoni mwa mkondo wa kwanza wa kujibu mapigo.

Hiyo haina maana Ukraine itapoteza. Wamefanikiwa kuvisukuma nje ya Kherson vikosi vya Urusi, kwa kushambulia maeneo yao ya kimkakati, na kuifanya Urusi ishindwe kupeleka mahitaji kwa vikosi vyake vya mji wa Kusini.

Wakijidhatiti wa silaha za masafa marefu kama vile kombora la Ukraine la Storm Shadow, Ukraine itajaribu kushambulia tena. Lakini katikati ya madai yote hayo na majibizano ya propaganda za vita, itachukua wiki au miezi kabla ya kupata picha ya wazi juu ya nani hatimaye anaweza kushinda vita hivi.