Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Putin azungumzia namna ya kulinda ardhi ya Urusi. Je, atafanikiwa?
Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano na kikosi cha wanajeshi, kwa mara ya kwanza ameeleza kwa upana kuhusu mashambulizi katika mkoa wa Belgorod. Kwa mujibu wa Putin, hakuna mtu katika mkoa huo na kazi ya kuimarisha mpaka ili kuulinda mkoa inaendelea.
Ikiwa hilo halitotosha, Urusi itafikiria kuunda eneo la ulinzi katika ardhi ya Ukraine, kwa umbali ambao itakuwa ni vigumu kuyafikia mikoa ya Urusi. Je, hilo linawezekana?
Putin amekutana na makamanda wa kijeshi huko Kremlin, ambao wanaunga mkono vita vya Ukraine. Mazungumzo yalidumu kwa saa kadhaa, ambapo Rais alizungumzia mambo mbali mbali.
“Hakuna haja ya uhamasishaji leo, hatua zaidi za Urusi katika vita zitategemea kiwango cha yale yanayowezekana baada ya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Ukraine kukamilika.”
Pia, Putin ametishia kujiondoa katika makubaliano ya nafaka. Vilevile, amezungumzia mashambulizi katika ardhi ya Urusi.
Alexander Kots, wa gazeti la kila siku la Urusi, Komsomolskaya Pravda, amemuuliza rais, “inawezekanaje droni za adui zikafika Kremlin?” “Na kwa nini Urusi baada ya kuikomboa Donbass, sasa inalazimika kuondoa watu wake katika maeneo ya mipakani?’
Vladimir Putin amejibu maswali hayo kwa undani sana, ingawa maelezo yote yameangukia katika kauli, “haya yote ni matatizo yanayopaswa kutatuliwa” – maneno hayo rais ameyarudia mara nne.
Kauli yake ya kwanza kuhusu mashambulizi ya droni, “kwa wakati fulani ndani ya Khmeimim, droni hizo zilikuwa angani, kwa bahati mbaya mabomu kadhaa yalirushwa katika maeneo yetu, tulipoteza watu. Lakini haraka tukajifunza namna ya kupambana nazo.”
Rais wa Urusi anaamini kwamba droni katika mikoa ya Urusi ni kitu hicho hicho; ulinzi wa anga hugeuka na kuwa makombora, ndege kubwa na droni zimeundwa kisasa na kwa mbao ni ngumu kuzigundua.
“Lakini tunazigundua, ingiwa zikiwa tayari zimeshaingia katika ardhi yetu,” amesema Putin.
Amekiri kuna tatizo katika mikoa ya Urusi inayopakana na Ukraine. Kuzuia ugaidi huu, kwa mujibu wa Rais wa Urusi, “ni lazima kuimarisha mipaka yetu.
Lakini uwezekano wa mashambulizi ndani ya Urusi kutoka Ukraine bado ni jambo linalowezekana.”
Njia ya kupambana na tatizo hilo, ni kuongeza mashambulizi katika vituo vyao vya kushambulia. Ikiwa hili litaendelea, kutengenezwa kwa eneo la ulinzi katika ardhi ya Ukraine, umbali mbao itakuwa ni vigumu kufikia ardhi ya Urusi.”
Hesabu za Urusi
Kwa kuhitimisha Putin amesema, “hakuna mtu katika mkoa wa Belgorod.” Labda anazungumzia kundi la wahujumu ambalo Gavana Vyacheslav Gladkov alitangaza mwezi Mei liliingia katika mkoa huo.
Vladimir Putin, aliuambia mkutano wana bloga wa kijeshi, kuhusu namna Urusi itashughulika na ukweli kwamba vita vimeshaingia katika ardhi yake. Tunazungumzia droni kupaa katika himaya ya Urusi na kufika Moscow, mizinga na makombora kushambulia maeneo ya mipaka, na kundi la watu wenye silaha lililoingia Urusi kutokea Ukraine.
Mbinu zilizopendekezwa na Putin zinavutia masikioni. Kwanza, ni muhimu kuimarisha mpaka ili makundi yenye silaha yasivuke. Pili, kuongeza mashambulizi katika vituo vya mashambulizi vya Ukraine, ili vishindwe kushambulia Urusi. Tatu, kuimarisha ulinzi wa anga, ili uweze kupambana na droni.
Unaonekana ni mpango unaoweza kufanya kazi. Lakini Urusi ni nchi kubwa, mpaka kati ya Urusi na Ukraine ni mkubwa, na maeneo ambayo yanaweza kulengwa pia ni makubwa. Rasilimali zinazohitajika kusawazisha tatizo hilo, tayari zimetumiwa.
“Kuna tatizo, na nafikiri mnaelewa pia. Kwa sababu ya kupeleka vikosi vyetu huko na hali ya upande huu. Kuondoa baadhi ya vikosi katika maeneo ambayo yanajulikana ni muhimu ikiwa yatashambuliwa na vikosi vya Ukraine,” rais wa Urusi amekiri.
Ili kuweka ulinzi wa anga katika majiji makubwa na katika maeneo muhimu, gharama yake itapelekea wanajeshi walio mstari wa mbele kuondolewa.
Mfano ni kama, ulinzi wa anga wa kambi ya Khmeimim huko Syria, ambayo Putin ameitumia kama mfano. Ingawa mfano huo haushawishi kwa sababu kambi hiyo ni ndogo na ni rahisi kuilinda.
Kupanga mashambulizi katika vituo vya Ukraine vilivyo mpakani, kama Putin anavyopendekeza, ni lazima kujihami kwa kutumia rada katika eneo zima la mpaka.
Ili kupambana na droni, ni lazima kuweka ulinzi wa anga wa masafa mafupi, kama vile Pantsir SI, vilevile kuweka vituo vya ulinzi wa kieletroniki katika majiji yote. Kufunga mpaka ili watu wenye silaha wasingie, utalazimika kupeleka vikosi vyote huko.
Hatimaye, eneo la kiulinzi katika ardhi ya Ukraine ambalo Putin amependekeza.
Eneo fulani umbali wa kama kilomita kumi kutoka mpaka wa Urusi, likiwa na silaha, likidhibitiwa na vikosi vya Urusi na ndege za kivita.
Rada na ulinzi wa kieletroniki, makombora, bunduki, risasi na mizinga na vikosi vitakavyo kaa huko. Urusi inahitaji hayo yote katika mstari wake wa mbele wa vita.
Mwezi Aprili, Mkuu wa Kamati ya Ulinzi ya Duma, Andrey Kartapolov, alipendekeza kuwapa ruhusa raia wa Urusi kulinda mpaka wao wenyewe.
Kwa mujibu wake, Urusi haina uwezo wa kulinda mipaka yote kama ilivyokuwa wakati wa Umoja wa Kisoviet.
Ila kuna njia nyingine, tabu zote hizo zina muingiliano na ule ukweli kwamba Urusi inaendelea na vita. Ingawa, kwa rais wa Urusi mpango wa kumaliza vita haupo katika mapendekezo yake.