Namna matajiri wa Qatar wanavyogusa maisha ya Waingereza
Na Dharshini David, BBC News

Chanzo cha picha, Getty Images
Qatar kuandaa Kombe la Dunia imekosolewa sana kutokana na rekodi yake juu ya haki za wanawake, vikundi vya LGBTQ+ na wafanyakazi wahamiaji.
Mahudhurio ya viongozi, timu, hata mashabiki yametiliwa shaka. Lakini uhusiano wa waingereza na Qatar unaenda mbali zaidi ya mashindano ya sasa, yanayogusa maisha yetu mengi.
Wengine wanaweza kuuliza ikiwa Uingereza ina haki ya kukuza uhusiano kama huo na serikali ambayo maadili yake yanaweza kuonekana kuwa kinyume na ya Waingereza.
Msingi wa uhusiano huo ni gesi. Qatar ni nchi ndogo yenye ukubwa wa kama eneo la Yorkshire lakini ina moja ya hifadhi kubwa zaidi za asili duniani - na Uingereza ni mteja wake mkuu.
Karibu nusu ya gesi ya Uingereza inatoka nje na karibu nusu ya hiyo inakuja kupitia bomba kutoka Norway. Lakini Qatar ni ya pili katika orodha hiyo inayosambaza takriban 9% ya uagizaji wa nishati kutoka nje.
Kinadharia, hiyo ndiyo kiasi kinachohitajika kwenye milioni ya nyumba za Uingereza. Katika muda wa chini ya miaka 20, Qatar imekuwa sehemu muhimu ya mahitaji ya nishati.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwezi Septemba, Qatar ilichukua umiliki wa ndege 24 za kivita zilizotengenezwa Lancashire, sehemu ya mkataba wa £5bn na mifumo ya BAE.
Serikali ya Qatar imekuwa ikirejesha baadhi ya pesa zake kwa kuwekeza nchini Uingereza. Sio moja y wawekezaji wakubwa waingereza - lakini hisa zake zimechaguliwa kimkakati ili kuongeza wasifu na ushawishi. Ni miongoni mwa wamiliki wakubwa wa mali nyingi nchini Uingereza.
Kwa jumla, kitengo cha uwekezaji cha serikali ya Qatar kimewekeza takriban £40bn, katika maeneo ambayo yanagusa mamilioni ya maisha ya Waingereza, na iliyoundwa ili kuhakikisha ushawishi wa nchi hiyo ndogo unazidi uzito wake katika ardhi ya Uingereza.
Mnamo Mei, Waziri Mkuu wa wakati huo Boris Johnson alipendekeza makubaliano ya Qatar kuwekeza hadi £ 10bn katika miaka mitano ijayo nchini Uingereza katika sekta kadhaa kuanzia usalama wa mtandao hadi sayansi ya maisha.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati huo huo, utegemezi wa waingereza kwenye gesi ya Qatar unaweza kuongezeka katika siku zijazo. Serikali ya Uingereza imekuwa ikikuza uhusiano na Doha, ili kuhakikisha usalama wa usambazaji huku hifadhi za Bahari ya Kaskazini zikipungua.
Uingereza katika miezi ya hivi karibuni imefaulu kutoagiza bidhaa kutoka Urusi. Hiyo ilikuwa karibu 4% tu ya mahitaji ya jumla ya Uingereza - lakini inafanya gesi inayotoka Qatar kuwa muhimu zaidi. EU inategemea zaidi gesi ya Urusi kwa hivyo kupata njia mbadala ni muhimu zaidi.
Qatar inamiliki kituo cha South Hook huko Wales, ambapo nishati ya gesi -LNG hupakiwa kwenye makontena maalum. Inadaiwa kuwa kituo hicho kinashika nafasi ya tano kwa kuhudumia mahitaji ya kila siku ya gesi nchini Uingereza - serikali ya Qatar inawekeza mamilioni ya fedha ili kuongeza uwezo huo kwa robo mwaka 2025. Na kufikia hatua hiyo, Qatar inatarajia kuongeza maradufu pato lake la LNG - bila uhaba wa wateja.
Huenda baadhi ya waingereza wasiweze kuiona ukaribu nchi hiyo na uingereza kwenye ramani lakini uhusiano wa Uingereza na Qatar unaonekana kukaribia kuwa karibu zaidi katika miaka ijayo.














