Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Madrid yamtaka Branthwaite
Real Madrid wanasaka beki wa kati msimu huu wa joto, huku beki wa England kutoka Everton, Jarrad Branthwaite, mwenye umri wa miaka 22, akiwa katika mipango yao (Teamtalk).
Klabu ya Serie A, Napoli, iko tayari kumnunua mshambuliaji wa Denmark, Rasmus Hojlund, kutoka Manchester United, kama klabu hiyo ya ligi kuu itakuwa tayari kumuuza kwa hasara ya mchezaji huyo wa miaka 22 aliyesajiliwa kwa pauni milioni 72 (Talksport).
Mshambuliaji wa England, Cole Palmer, mwenye umri wa miaka 22, ataulizwa ikiwa ana furaha kubaki Chelsea msimu huu wa joto, endapo klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. (Times).
Manchester City inataka kuwasajili beki wa kulia wa England na Newcastle, Tino Livramento, 22, na beki wa kushoto wa Italia na Juventus Andrea Cambiaso, 25. (Telegraph)
Hakuna klabu yoyote inayovutiwa kwa dhati kumsajili kiungo wa Brazil, Casemiro, kutoka Manchester United, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 akiwwka msimamo wake kuhusu mshahara wake wa sasa. (Teamtalk)
Timu mpya ya MLS, San Diego, haijapiga hatua yoyote katika juhudi za kumsajili kiungo wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne, kwa uhamisho wa bure kutoka Manchester City msimu huu wa joto, licha ya madai kuwa mipango hiyo iko karibu kukamilika. (Teamtalk)
Newcastle United itasikiliza ofa kwa ajili ya kipa wa England, Nick Pope, mwenye umri wa miaka 32, msimu huu wa joto. (Football Insider)
Neymar hivi karibuni alirejea katika klabu yake ya kwanza, Santos, lakini wakala wake Pini Zahavi amesema kuwa mshambuliaji huyo wa Brazil, mwenye umri wa miaka 33, anaweza kurejea Barcelona msimu huu wa joto kwa uhamisho wa bure. (Sport - in Spanish).
Kiungo wa Southampton mwenye umri wa miaka 19, Tyler Dibling, ataondoka klabuni hapo ikiwa itashuka daraja daraja kutoka kutoka ligi kuu England msimu huu. (Football Insider), external
Kocha Ruud van Nistelrooy anazidi kukumbwa na shinikizo kubwa na kufukuzwa katika klabu ya Leicester City. (Football Insider)