Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
WAFCON 2022: Wenyeji Morocco wailaza Burkina Faso katika mechi ya ufunguzi
Wenyeji Morocco walifungua michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika miongoni mwa Wanawake kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Burkina Faso walioshiriki kwa mara ya kwanza katika mji mkuu Rabat.
Mkwaju wa adhabu wa Nahodha Ghizlane Chebbak kabla ya nusu saa ulitosha kuwapatia Waafrika hao wa Kaskazini ushindi wao wa kwanza katika shindano hilo kwa miaka 24.
Ijapokuwa shambulio hilo halikuwa na nguvu na usahihi lilimhadaa kipa wa Burkinabe Mariam Ouattara, 19, ambaye angefanya vyema zaid kuokoa shambuliz hilo.
Katika Kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika miongoni mwa Wanawake (WAFCON) baada ya miaka 22, Wamorocco baadaye watakutana na Uganda, katika mechi ambayo pia tachezwa mjini Rabat, Jumanne.
Mchezo wa pili katika Kundi A utafanyika Jumapili wakati Ugandan Cranes watafungua akaunti yao dhidi ya Senegal.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza katika fainali za WAFCON katika kipindi cha miaka minne baada ya toleo la 2020 kufutwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona, ambalo Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) lilikuwa limesema linasita kufanya.
Hizi ni fainali za kwanza za michuano hiyo zinazoshirikisha timu 12, baada ya Caf kupanua michuano hiyo mwaka 2019, WAFCON hii pia inafanyika katika ardhi ya Afrika Kaskazini kwa mara ya kwanza.
Nchi mwenyeji Morocco kwa sasa iko katikati ya mpango kabambe wa uwekezaji wa miaka minne katika soka la wanawake, kwa lengo la kuongeza pakubwa umaarufu wa mchezo wa wanawake nchini humo.
Timu hiyo kwasasa inaongozwa na Reynald Pedros, ambaye alikuwa mkufunzi wa timu ya Lyon ya Ufaransa iliofanikiwa kuchukua mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka wa 2018 na 2019,
Amekuwa akiijenga upya timu hiyo tangu wakati huo na ingawa timu yake ilionekana kana kwamba ingeshinda kwa urahisi na tena kwa mabao mengi mchezo huo wakati fulani, mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa alionyesha kuchanganyikiwa baada ya timu yake kushindwa kuongeza mabao .