Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.02.2024

Chanzo cha picha, Shaun Botterill
Beki wa Liverpool na Scotland Andy Robertson, 29, ndiye mlengwa mkuu wa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakati wakipanga jinsi ya kujaza nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Canada Alphonso Davies, ambaye anaonekana yuko tayari kujiunga na Real Madrid. (Daily Mail)
Wasiwasi wa Arsenal juu ya kiwango cha majeruhi ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus ni sababu kubwa ya kutafuta mshambuliaji wao, huku Ivan Toney wa Brentford, Victor Osimhen wa Napoli, Joshua Zirkzee wa Bologna na Viktor Gyokeres wa Sporting wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa. (Daily Mail)
The Gunners wanamtaka beki wa Ajax Jorrel Hato, 17, lakini klabu hiyo ya Uholanzi ina matumaini ya kumshawishi asaini mkataba mpya. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili Kylian Mbappe, 25, Real Madrid pia wamekubali kumsajili mdogo wa mshambuliaji huyo wa Ufaransa Ethan, 17, kutoka Paris St-Germain. (OK Diario - kwa Kihispania)
Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 51, yuko juu ya orodha ya Sir Jim Ratcliffe kuchukua nafasi ya Erik ten Hag kama mkufunzi wa Manchester United. (FootMercato - kwa Kifaransa)
Kocha wa Brighton Roberto de Zerbi pia anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Mholanzi huyo. (MEN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich pia wanavutiwa na kocha wa Seagulls De Zerbi huku Xabi Alonso wa Bayer Leverkusen na mkufunzi wa zamani wa Ujerumani Hansi Flick ni wagombea wengine watarajiwa. (Sky Germany)
Kazi ya Vincent Kompany haipo mashakani huko Burnley, licha ya timu yake kutarajia kurejea kwenye mashindano. (The Athletic)
Barcelona wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa zamani wa Manchester United David de Gea, 33, huku Mhispania huyo akiwa mchezaji huru kwa sasa. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Reuters
Newcastle United na Tottenham wanamtaka mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 25 Omar Marmoush, mchezaji wa kimataifa wa Misri ambaye amefunga mabao 10 katika michezo 18 ya Bundesliga msimu huu. (Bild via Shields Gazette)
Liverpool wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Porto na Argentina Alan Varela, 22. (Mirror)
Barcelona wana nia ya kujaza nafasi ya kocha Xavi, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu, na kumchukua mkufunzi wa Inter Milan Simone Inzaghi. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












