Kwa nini kuwa mkarimu kwa wengine kunaweza kuwa na faida kwa afya na mwili wako?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sote tungependa njia za haraka na rahisi za kuboresha afya zetu, lakini tunapata ushauri unaokinzana.
Kwa hiyo, ikiwa utajaribu jambo moja tu kuboresha hali yako ya kiakili na kimwili, inaweza kuwa vipi?
Labda chai ya kijani ili kuongeza nguvu ya ubongo au kucheza michezo ya kuchangamsha ubongo kwa dakika chache ili kudhibiti shinikizo la damu.
Na vipi kuhusu kufanya matendo madogo ya ukarimu ili kunufaisha mfumo wako wa kinga?
Ni saa 11 alfajiri na nimefanya jambo ambalo linaweza kuboresha hali yangu, kupunguza maumivu, na kupunguza uvimbe (inflamation) wa kudumu: Nilimtengenezea mke wangu, Claire, kikombe kitamu cha kahawa, ambayo anaipenda kahawa ya saa za asubuhi.
Kumtengenezea mtu kikombe cha kahawa hakutabadilisha afya yake kwa kiasi kikubwa. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba matendo ya kawaida ya ukarimu au msaada yanaweza kuleta mabadiliko makubwa.
Ni wazi, ukarimu humnufaisha mpokeaji. Lakini utafiti mpya unaonyesha kwamba ukarimu pia unaweza kuwawa manufaa kwa mtu anayeizuzoea.
Kuwa mwenye ukarimu mara kwa mara kunaweza kuongeza furaha na kupunguza dalili za mfadhaiko na wasiwasi.
Lakini kile ninachoona cha kushangaza ni kwamba inaonekana pia kuwa na athari kubwa kwenye mfumo wetu wa kinga kwa kupunguza uvimbe mwilini(inflamation).

Chanzo cha picha, Getty Images
Uzoefu kidogo
Nilipokuwa nikitafiti jinsi matendo ya ukarimu yanavyoweza boresha afya, nilitaka kufanya jaribio dogo: kumshawishi Sam, meneja wa mradi kutoka Kent, Uingereza, kujumuisha vitendo vichache vya ukarimu katika utaratibu wake wa kila siku.
Ili kufanya hivyo, nilimuuliza kwanza Sam jinsi hali yake ilivyokuwa.
"Hakika inabadilika. Nina kazi inayonisumbua sana na inanileme,” ananiambia.
Zaidi ya hayo, ananiambia kwamba anaishi peke yake na "kujishughulisha mwenyewe."
Ninashauri kufanya kwa wiki kufanya ishara tatu za ukarimu, labda niandike dokezo kwa rafiki ambaye anahitaji usaidizi kidogo kwa sasa, au kitu chochote, lakini mambo matatu tofauti.
Kubali... Itakuaje? Tutajua katika makala hii.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uwezeshaji wa ubongo
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa kuanzia, tafiti nyingine zinaonyesha kuwa kuwa ukarimu kwa wengine kunaweza kuboresha hali yetu kwa kiasi kikubwa.
Katika utafiti uliofanywa mnamo 2023, wanasayansi waligawanya watu tofauti wanaougua msongo wa mawazo mdogo , wasiwasi au mfadhaiko katika vikundi vitatu.
Kundi moja lilifanya matendo matatu ya ukarimu kwa wiki kwa muda wa wiki tano. Kikundi kingine kiliagizwa kuwa na urafiki zaidi na kikundi cha mwisho kilipitia aina ya maandishi ya tiba ya tabia ya utambuzi.
Wanasayansi waligundua kuwa kati ya shughuli hizi tatu, matendo ya ukarimu yalikuwa na athari kubwa juu ya hisia na kupunguza kwa kiasi kikubwa wasiwasi na msongo wa mawazo.
Kwa nini na kwa jinsi gani ukarimu huboresha hali yetu?
Ubongo unaweza kuonyesha wakati mtu anaamua kuwa mkarimu au kushirikiana na watu wengine kwa sababu eneo la ubongo linalojulikana kama corpus au striatum huchangamka.
Sehemu hii ya ubongo hujibu kwa vitu ambavyo vinaweza kuwa na athari nzuri, kama vile kula vyakula vitamu.
Safu yake inaaminika kuwa msingi wa kibaolojia wa joto hilo la hisia nzuri tunazohisi tunapokuwa naukarimu.
Lakini kufanya uchunguzi wa ubongo kunaonyesha jambo lingine la kushangaza: wema unaweza kusaidia kupunguza maumivu.
Katika utafiti wa hivi majuzi, wa kutisha, watu waliojitolea walipewa mshtuko wa maumivu wa umeme walipokuwa wakiamua kutoa au kutotoa pesa. Wale waliochangia walihisi maumivu kidogo.
Utafiti mwingine uligundua kuwa kutoa damu kunaumiza kidogo kuliko kuchukua damu kwa kipimo, ingawa sindano ilikuwa nene mara mbili.
Mwanzo wa Sam
Ninaingia na Sam katikati ya wiki ili nione anaendeleaje na wema wake.
Ananiambia kuwa tayari amekamilisha mawili kati ya matatu niliyomuagiza.
“Nilifanya jambo zuri sana kwa rafiki yangu na mama yangu. Nilimwandikia barua ndefu ya ukarimu kutoka kwa baba yangu, mimi na kaka yangu nikimwambia jinsi tulivyomthamini. Alifurahi sana,” Sam aliniambia.
Ananiambia ameona tofauti katika hali yake: "Ninahisi matumaini zaidi kuliko kawaida na hii pia imekuwa na athari nzuri kwa baadhi ya mahusiano yangu. »
Alishangaa sana kuona jinsi watu walivyothamini ishara ambayo ilitoka kwa ghafla.
"Kwa kweli nataka kufikiria jambo kubwa kwa tendo langu la mwisho la ukarimu mwishoni mwa juma," aliniambia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shukrani zaidi, dhiki kidogo
Mbali na athari za ukarimu juu ya hisia na maumivu, kuna utafiti wa kuvutia kuhusu jinsi wema kwa wengine unavyoweza kupunguza homoni za mkazo na uvimbe wa mwilini wa kudumu, ambao unaweza kunufaisha afya yako kwa ujumla.
Dk. Tristane Inagaki wa Chuo Kikuu cha Jimbo la San Diego alichunguza faida za kiafya za ukarimu na kugundua kwamba unaweza kupunguza uvimbe wa kudumu (inflammation).
Kwa kufanya hivyo, utafiti ulifanyika kwa watu wazima wenye umri wa miaka 25 hadi 76 ambao walikuwa na mtihani wa damu na kupima kiwango cha interleukin-6 au IL6, inayosababisha uvimbe mwilini.
Watu waliojitolea waliripoti ni watu wangapi na mashirika waliyotoa msaada, usaidizi au wema kwao.
"Tuligundua kuwa kuwa na ukarimu kwa watu na mashirika zaidi, kama marafiki na familia, lakini pia kujitolea, hata bila kupokea matibabu, kunahusishwa na kushukwa kwa kiwango cha uvimbe (inflammation) mwilini ," anabainisha Inagaki.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tunajua kuwa aina hii ya uvimbe husababisha magonjwa mengi tofauti. Kwa hivyo ni vizuri kuwa na uchochezi mdogo wa kimfumo. "Kuvimba kwa muda mrefu kunatabiri magonjwa yote yanayojulikana, ugonjwa wa moyo na mishipa, saratani au hata msongo wa mawazo," anasema.
Katika utafiti mwingine, Inagaki alichunguza uhusiano kati ya wema na mafadhaiko. Na, kama ilivyotokea katika kisa kilichotangulia, kwa watu ambao walikuwa wamefanya mazoezi ya vitendo yanayohusisha kuonyesha ukarimu baadaye mwitikio wao wa msongo wa kisaikolojia ulishuka kwa mfano, shinikizo la damu lilikuwa chini, anaelezea.
"Kuna uhusiano mkubwa sana: watu wanaosumbuliwa na matatizo ya muda mrefu wana uvimbe unaowapata taratibu," anaelezea Dk Inagaki.
Kwa hiyo, asema, “Kupunguza mfadhaiko na uvimbe ni mojawapo ya manufaa makubwa zaidi ya ukarimu.” »

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwisho wa wiki ya Sam
Baada ya siku 7 na matendo ambapo alikuwa amekamilisha matendo matatu ya ukarimu maishani mwake Sam, aliniambia kuwa alifurahia mchakato mzima na kwamba alimchagua kaka yake kama mhusika wa tendo lake la mwisho la ukarimu katika jaribio hili dogo.
"Ndugu yangu amekuwa na wakati mgumu hivi karibuni, kwa hivyo niliwatunza watoto wake kwa siku ili yeye na mke wake wapumzike. Na najua aliithamini sana,” ananieleza.
Na aliona faida, pia.
"Imeathiri maisha yangu kwa njia nzuri sana. "Nina furaha sana, ni rahisi kuungana na baadhi ya watu maishani mwangu baada ya kufanya hivi... Bila shaka, ni jambo ambalo ninataka kuendelea kulifanya," anasema.
Inafurahisha kuona jinsi Sam alivyothamini changamoto yake ya ukarimu. Pia ninajaribu kujumuisha matendo ya wema katika utaratibu wangu wa kila siku.
Kwa nini usijaribu? Utamfurahisha mtu mwingine na inaweza kupunguza uvimbe wako wa kudumu mwilini (inflammation).
Hili ni jambo unaloweza kufanya sasa hivi ambalo linaweza kuufaidi sana mwili wako na maisha yako.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












