Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: City, Man U, Barca, Madrid zapigana vikumbo kwa Frimpong

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester City, Manchester United, Barcelona na Real Madrid wanavutiwa na winga wa Bayer Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong, 24. (Teamtalk)

Arsenal wana nia ya kumsajili winga wa Ujerumani Leroy Sane kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 wa Bayern Munich utakapokamilika msimu huu wa joto. (Christian Falk)

Mkurugenzi mpya wa kandanda wa Arsenal Andrea Berta anataka kumfanya kiungo wa kati wa Newcastle Brazil Bruno Guimaraes na kiungo wa kati wa Real Sociedad, 26 Martin Zubimendi kuwa usajili wake wa kwanza. (AS - in spanish)

Barcelona pia wanamuweka kiungo wa Newcastle Guimaraes kwenye orodha ya walengwa wa uhamisho wa majira ya joto. (Football Espana)

Liverpool imetuma maskauti kumtazama mlinzi anayecheza upande wa kushoto wa Ajax, Jorrel Hato, 19, ambaye amechezeshwa mara tano na Uholanzi. (Mail)

Everton wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle mwenye umri wa miaka 27 Sean Longstaff msimu wa joto. (Talksport)

Barcelona wamekataa dau la pauni milioni 57.8 kutoka kwa Manchester United kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 27. (Fichajes)

Mkufunzi wa Barcelona Hansi Flick anataka kumbakiza De Jong bila gharama yoyote na klabu hiyo ya Catalan imeanzisha tena mazungumzo kuhusu mawasiliano mapya. (Sport)

Everton wanafuatilia maendeleo ya kiungo wa kati wa Tottenham mwenye umri wa miaka 25, Manor Solomon, ambaye yuko Leeds kwa mkopo. (Teamtalk)

Bayer Leverkusen bado wana imani kuwa mchezaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 21, ataongeza mkataba wake katika klabu hiyo, licha ya kuhusishwa na Bayern Munich na Manchester City. (Bild)