Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 15.06.2024
Arsenal imetangaza bei yao ya mchezaji Emile Smith Rowe ya £30m , huku Reiss Nelson akiwafahamisha Gunners kuhusu nia yake ya kupima chaguo lake, Chelsea wanapewa ruhusa ya kuzungumza na Jhon Duran.
Arsenal wako tayari kukubali dau la pauni milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe, 23, msimu huu. (Football Insider), ya nje
Winga wa Uingereza Reiss Nelson, 24, ameifahamisha Arsenal kwamba anataka kutathmini chaguo lake kuhusu uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo. (Athletic - subscription required)
Chelsea imepewa ruhusa na Aston Villa kujadili masuala ya kibinafsi na mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 20.(Telegraph- subscription required)
The Blues , hata hivyo, hawana uhakika kama wanataka kuendelea na mpango wa kumnunua Duran (Guardian)
Villa pia wamefanya uchunguzi na Chelsea kuhusu beki wa kushoto wa Uholanzi Ian Maatsen, 22, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Borussia Dortmund . (Sky Sports)
Manchester United wako tayari kutafuta safu nyingine ya ulinzi ikiwa Everton hawako tayari kufanya mazungumzo ya kumnunua beki wa kati wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21. (ESPN)
Everton wameungana na Tottenham , Aston Villa na West Ham kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Roma Mwingereza Tammy Abraham, 26. (Mail)
Chelsea wamekubaliana kwa maneno na winga wa chini ya miaka 21 wa Crystal Palace na Ufaransa Michael Olise, 22, na wanatazamiwa kulipa ili kupata uwezekano wa kupata mkataba huo. (Team Talk)
Manchester City haitakubali ofa zozote kwa mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 24, msimu huu wa joto. (Football Insider)
Arsenal inamuwinda winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 21, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 50m (£42.2m). (Football London)
Brighton wanatazamiwa kumteua Fabian Hurzeler kama meneja wao mpya baada ya kukubali kulipwa fidia na klabu ya St Pauli ya Ujerumani . (Fabrizio Romano), ya nje
Newcastle wamefanya mawasiliano na AC Milan kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Uingereza Fikayo Tomori, 26. (Football Insider), ya nje
Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ana kibarua kipya cha kutoa tathmini ya kiufundi kwenye mechi za Euro msimu huu wa Uefa. (Mail)
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi