Ndugu wanaokimbia kuzunguka ukuta mkubwa wa China
Iliyochapishwa
Vijana wawili wanashiriki mbio za kuzunguka ukuta mkubwa nchini China ambapo ni wachache wamewahi kuimaliza. Wanakimbia urefu wote wa Ukuta huo.
Ndugu hao ambao mama yao ana asili ya China na baba Muingereza, wanamaliza mbio za kila siku walizofanya kwa miezi sita.
Wanakimbia kupitia jangwa, juu ya milima na katikati ya magofu hatari yanayobomoka.









