Mwanamuziki anayepiga ala ya muziki kutumia vidole vya miguu yake

.

Chanzo cha picha, BOURNEMOUTH SYMPHONY ORCHESTRA

Iliyochapishwa

Ukitazama bango la matangazo la BBC mwaka huu utaona baadhi ya watu mashuhuri kiongozi wa muziki Sir Simon Rattle na mwimbaji nyota Sheku Kanneh Mason.

Lakini angalia kwa karibu zaidi na utamuona mcheza ala ya muziki anayetumia vidole vyake vya miguu.

Felix Klieser ameelezewa kuwa mtu hodari na amefanya maonyesho kote ulimwenguni, ingawa alizaliwa bila mikono anacheza ala hiyo kwa mguu wake wa kushoto.

"Ilikuwa muujiza," Felix anasema, kwa yeye kupiga tarumbeta nchini.

Si kwa sababu ya maumbile yake bali kwa sababu alipoomba kujifunza ala hiyo, akiwa na umri wa miaka minne, familia yake haikujua alichokuwa akizungumzia.

"Sikuwa nimewahi kwenda kwenye tamasha, wala kukutana na mpiga tarumbeta na katika familia yangu hakukuwa na mtu kwenye fani ya muziki. Wazazi wangu walisema: 'Err, mpiga tarumbeta ni nini hiyo?" aliambia BBC Access All podcast.

Familia yake ilifanya utafiti na akabahatika.

Katika jiji la Ujerumani la Göttingen, ambako Felix alikulia "kulikuwa na shule moja ya muziki na katika shule hiyo kulikuwa na mwalimu mmoja anayefundisha ala ya kupiga tarumbeta".

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Felix alijiandikisha na safari ya ndoto yake ikaanza.

Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu kabla maswali kuanza kujitokeza.

Angepigaje ala inayohitaji mkono mmoja kushika tarumbeta na mwingine kutengeneza sauti? Bila vidole, angetumia vipi vali kubadilisha noti?

Mwanzoni haikuwa shida hata kidogo.

Akiwa mtoto Felix aliweza kukaa sakafuni na kufikia mdomo wake huku mtu akiwa ameshika ala hiyo.

Alipokuwa akikua, alifanya kazi na "mtu mbunifu anayeweza kufanya vitu vya kushangaza" kuunda stendi ambayo inashikilia chombo hicho cha muziki mahali pake.

Kuhusu kukosa vidole, Felix aligundua kuwa angeweza kuinua mguu wake mmoja juu na kuutumia ule wa kushoto kama vidole kwa ustadi.

Jinsi anavyouinua mguu huo, inavutia, hata kwa Felix mwenyewe.

"Ninapojiona nafurahia sana. Lakini ninapocheza ala peke yangu ni nafasi nzuri sana kwangu," anasema. "Ni kitu ninachoweza kufanya kwa masaa."

Changamoto kubwa zaidi haikuwa moja kwa moja kimwili bali kufanya ala hiyo isikike kwa ubunifu wa kipekee.

Inajumuisha ile ala yenye kutoa sauti ya shaba ya 12ft, ambayo inafanya sauti kuzunguka mfano wa "kengele " na kutoka.

Wachezaji tarumbeta huweka mkono wao wa kulia kwenye kengele ili kuunda sauti inayojulikana, ambayo huenda pengine umeisikia mfano kwenye muziki maarufu wa filamu.

Bila mkono kuuweka sehemu yenye kukaa kengele, Felix aligundua kwamba angelazimika kuunda sauti kwa jinsi alivyocheza.

"Hakukuwa na mwalimu ambaye angeweza kunifundisha jinsi ya kucheza tarumbeta kwa njia hii. Ilikuwa mtindo wa kujaribu na kujaribu tena. Nina midomo yangu, na naweza kuvuta hewa," anasema.

"Unapaswa kudhibiti hewa kwa njia tofauti na kuangalia namna unavoweka midomo na ulimi wako. Hili labda lilikuwa jambo lililonipa changamoto zaidi, pia nilifanya mazoezi mengi."

Mbinu hii inamfanya Felix kuwa tofauti na wachezaji wengine wa ala.

Alitambuliwa mapema sana katika masomo yake kama wa kipekee kwa kiwango chochote kile, lakini hata wale walio karibu naye walitilia shaka kama angekubaliwa katika ulimwengu wa muziki aina ya classic.

.

Chanzo cha picha, FELIX KIESLER

Akiwa kijana, Felix alisomea masuala ya muziki na mchezo wa kuigiza katika Chuo Kikuu cha Hanover na akashinda tuzo ya kifahari.

Wakati huo, yeye na mwalimu wake walihojiwa kwenye gazeti moja.

Mwandishi alimuuliza Felix ikiwa ana mpango wa kufanya kazi kitaaluma.

"Jibu langu lilikuwa kitu kama: 'Labda inawezekana, sijui kwa sababu bado niko shuleni''."

Kisha mwalimu wake, mchezaji ala maarufu, akamkatisha. "Ni jambo zuri kwako kulifanya kuwa mazoea, lakini hutawahi kuwa mpiga ala kitaaluma. Kamwe, hilo haliwezekani. Huna mkono wa kulia, na kengele ya kutoa sauti inafanya kazi tofauti. Hiyo haitawezekana."

Ilikuwa nyakati zinazoonekana kuwa zisizo na maana lakini hata hivyo zilibadilisha mwelekeo wa matukio yajayo kwa Felix, ambaye ghafla na bila kutarajia alijifunza maisha hukupa machaguo mawili.

"Lazima uamue, nijaribu kuonyesha kwamba inawezekana au nikate tamaa? Hali hizi hutokea mara nyingi sana katika maisha yangu," anasema.

Badala ya kujitahidi kuwa mwanamuziki wa kulipwa, Felix alitaka tu "kucheza tarumbeta vizuri iwezekanavyo," na kuona hilo lingemfikisha wapi.

Imempeleka duniani kote hata kusini mwa Uingereza ambako hivi karibuni alikamilisha miaka miwili akiwa na bendi ya Bournemouth Symphony Orchestra na hata kufanya ziara na mwimbaji, Sting.

Lakini anasema kubwa alilojifunza linarudi katika miaka yake ya awali.

"Jambo muhimu zaidi, nilipokua, ni kujifunza kutatua matatizo," anaongeza.

"Sikuwahi kujua kile kinachowezekana kwangu na kisichowezekana. Lakini unapokuwa na nia ya kufikiria na kusema, 'Ndio, naweza kutatua kila tatizo,' basi una machaguo mengi katika maisha yako.

"Na hili sio suala la kuwa na ulemavu au la, kwa sababu mwishowe sote tuna kitu kimoja au kingine ambacho unafikiria 'Ndio, kina ukomo wake'."

.

Chanzo cha picha, FELIX KIESLER

Imekuwa njia ya kufurahisha kujumuika na mashabiki kote ulimwenguni lakini baadhi watapata kumtazama Felix akifanya onyesho huko London atakapopanda jukwaani katika Ukumbi wa Royal Albert kwa ajili ya uzinduzi wa Matangazo ya BBC tarehe 2 na 3 Agosti.

Atashiriki tamasha la Mozart's Horn Concerto No. 4.

"Nimefurahi," anasema.

"Kwangu mimi jambo muhimu zaidi ni kuwafahamu watazamaji wa hapa.

"Unapokuwa mdogo na kuanza taaluma, bila shaka unalenga kufanya maonyesho na bendi na waongozaji maarufu.

Lakini sasa hivi nataka kuchezea watu ala ya muziki ili kuifanya dunia kuwa nzuri zaidi."