Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 24.06.2022
Bayern Munich wanaweza kumnunua Ronaldo ikiwa Lewandowski atawaacha msimu huu wa joto.
Wakala wa zamani wa Neymar anasema mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 ana ndoto ya kuwa mshindi wa Ligi ya Mabingwa akiwa na Paris St-Germain na "hatakoma hadi aifanikishe." (Goal - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 30, anaamua kama atajiunga na Manchester United au abaki Brentford. (Sky Sports)
Chelsea itachuana na Manchester United kumnunua winga wa Ajax na Brazil Antony baada ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Football365)
Barcelona hatimaye wamewasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, ambalo lina thamani ya hadi £34m (euro milioni 40). (Telegraph - subscription required)
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anaripotiwa kuwa na wasiwasi kuhusu biashara ya uhamisho ya Manchester United chini ya meneja mpya Erik ten Hag na anafikiria kuhama Old Trafford. (Record - in Portuguese)
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 29, ana makubaliano kimsingi ya kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa bila malipo. (Sky Italia - in Italian)
Manchester United, Chelsea na Tottenham wanachunguza uwezekano wa kumsajili winga wa Atletico Madrid na Ubelgiji Yannick Carrasco, 28, msimu huu baada ya maelezo ya kipengele chake cha kuachiliwa kwa euro milioni 60 (£51.5m) kuibuka. (AS - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot anataka kuondoka Juventus na kujiunga na klabu ya Premier League. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake, atapatikana kwa kati ya euro milioni 15-20 (£13-17m). (Telegraph - subscription required)
Chelsea wanavutiwa na nyota wa Juventus mwenye umri wa miaka 22 na beki wa kati wa Uholanzi Matthijs de Ligt. (Sky Italia)
Lyon wamehamia kumsajili Tyrell Malacia anayelengwa na Manchester United. Beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anachezea Feyenoord(Metro)
Leicester City wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Rennes Mfaransa Benjamin Bourigeaud, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa na uwezekano wa kuwagharimu Foxes kwa ada ya pauni milioni 8. (Jeunes Footeux - in French)
AC Milan wanafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Aston Villa Douglas Luiz, na maajenti wa Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 24 wamesafiri katika klabu hiyo ya Italia. . (TuttoMercatoWeb - in Italian)
Marseille wanataka kumsajili mlinzi wa Ureno Nuno Tavares, 22, kwa mkopo na Arsenal watafikiria uhamisho huo ikiwa wanaweza kuajiri katika nafasi hiyo. (The Athletic)