Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi familia ya watu 14 inavyokabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha
Alipoulizwa jinsi anajipumbaza kutoka kwa ya maisha ya familia na watoto 12, Zoe Sullivan anatania: "Naenda kwenye duka kubwa kwa mapumziko."
"Ina shughuli nyingi lakini hiko ndicho tumechagua kufanya. Nadhani tungekuwa na kuchoka ikiwa hatungekuwa na mengi yanayoendelea," anasema.
Zoe, 43, na mumewe Ben, 47, wanatoka Lossiemouth huko Moray. Mtoto wao mkubwa ana umri wa miaka 17 huku mdogo, mtoto Florence, akiwa na miezi mitatu.
Ben anapofanya kazi kama mhandisi wa RAF, familia ilikodisha nyumba karibu - nyumba ya vyumba vinne na bustani, ambayo Zoe anasema imekuwa njia ya kuwakimu kimaisha watoto, haswa wakati wa vizuizi vya Covid.
Watoto wa Sullivan wanaishi maisha yenye shughuli nyingi, ikijumuisha masomo ya dansi, mechi za mpira wa miguu, mazoezi ya viungo, maandalizi ya chuo kikuu, miradi ya sanaa, kuoka mikate nyumbani, na matembezi ya familia.
Lakini bei nchini Uingereza zinapopanda hadi kiwango cha juu zaidi katika miaka 40, mama Zoe - ambaye anasimamia fedha za familia - analazimika kufikiria njia mpya za kupunguza matumizi.
Gharama ya kila wiki inagharimu pauni 320 - ikijumuisha vyoo, bidhaa za kusafisha, nepi na pesa kwa watoto wakubwa kununua chakula cha mchana mara kwa mara.
Ni takwimu ambazo Zoe ameweza kudumisha katika miaka michache iliyopita kwa kufuatilia gharama ya bidhaa kwenye maduka makubwa mbalimbali - na kuepuka chapa za majina inapobidi.
'Kuhesabu mapeni'
"Kila wakati najugundua kuna ongezeko la aslimia moja au tatu- watoto wanapenda kuwa na kanga ambazo zamani zilikuwa £1. Sasa ni £1.35 kwa hivyo nitakuwa nikinunua chapa tofauti au nikinunua kwingine.
"Tunanunua baadhi bidhaa zenye chapa kwa baadhi ya vitu tunavyopenda sana, kwa mfano Frosties - lakini hali ikilazimu hatuna budi kubadilishana na kununuabidhaa zisizo na chapa."
Zoe ana mikakati rahisi ya milo inayolisha familia nzima huku akipunguza ubadhirifu. Ni pamoja na kutengeneza mlo wa chungu kimoja - ikijumuisha supu, tambi na mash kwa kutumia mfuko wa kilo 1 wa viazi - ambao unaweza kuongezwa na vitu kutoka kwa friji.
"Milo kama tambi bolognese daima ni nzuri na ya bei nafuu kutengeneza," anasema. "Wote wanaipenda - ingawa sisi huwa hatuli nyama nyingi kwa sababu ni ghali sana.
"Tunapika kitoweo kingi wakati wa majira ya baridi kali, ama mboga mboga au nyama ya ng'ombe kwenye sufuria kubwa ambayo unasidia bei kuwa nafuu.
Lakini kuna siku watu wako hapa, pale na kila mahali kwa hivyo kutakuwa na kitu cha haraka kwenye oveni."
Kwa ujumla, familia haili kwenye mikahawa au kwenda nje ya nchi kwa likizo, na Zoe na Ben waliacha kunywa pombe miaka minne iliyopita kwa sababu ilikuwa ghali sana.
Lakini chipsi bado ni baadhi ya vitu ambavyo Zoe amepunguza kwa familia nzima - ingawa anasema hii ni kwa sababu za kiafya kama ilivyo kwa gharama.
Vinywaji vizuri huwekwa kwa wikendi, kama vile vitafunio kama vile chokoleti na crisps.
"Walikuwa na vitafunwa zaidi wakati wa Krismasi lakini tumepunguza ili kudumisha mambo mengine tunayofanya maishani," Zoe anasema.
"Ikiwa tunafanya matembezi kwenda ufukweni, tutabeba biskutiau tutafanya picnic kwa sababu ni nafuu kununua chakula katika maduka makubwa kuliko kula nje."
Mkuu mmoja wa tasnia ya chakula ameonya kuwa bei ya vyakula inaweza kupanda hadi 15% mwaka huu - na kwa wastani wa nyongeza ya mishahara haiendani na kasi hiyo.
Bili za nishati ni mojawapo ya vitu vinavyochangia mfumuko wa bei kwa sasa, kwani bei ya mafuta na gesi imeendelea kupanda kutokana na vita vya Ukraine.
Hili, Zoe anasema, limekuwa changamoto kkabiliana nalo. Bili za gesi na umeme za familia hiyo zimekaribia kuongezeka maradufu, kutoka £240 hadi £400 kwa mwezi, na wamejipata wakitumia £120 hadi £180 kwa mafuta ya magari mawili.
"Hii ni kando na mambo mengine kama kununua nguo," anasema. "Lakini ni sio rahisi - utaendela hivi kwa muda gani.
Tumezoea kutoenda sehemu nyingi na tunaridhika zaidi na kile tulichonacho karibu nasi.