Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Liverpool kumuuza Diaz ili kupata mshambuliaji – Tetesi za soka Jumamosi
Liverpool watamuuza Luis Diaz ili kupata fedha za kumnunua mshambuliaji, Manchester City kuwaondoa uwanjani wachezaji na Arsenal yaanzisha tena azma ya kumnunua Dusan Vlahovic.
Liverpool watamuuza mshambuliaji wa Colombia Luis Diaz, 28, msimu huu ili kufadhili usajili wa mshambuliaji. (Football Insider)
Manchester City itawaondoa uwanjani wachezaji ambao hawawezi kuendelea na ratiba yao kwa sababu ya majeraha au uchovu, pamoja na walio katika tishio wakiwemo kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, na mlinzi wa Uingereza John Stones, 30. (Guardian).
Arsenal wanamtafuta tena mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, 25, huku klabu yake ya Italia ikiwa tayari kumuuza Mserbia huyo kwa kitita cha euro 40m (£33m). (CaughtOffside).
Manchester United, Liverpool na Chelsea wote wanafuatilia uhamisho wa Real Madrid msimu wa joto yenye kumwinda mlinzi wa RB Leipzig na beki wa Ufaransa Castello Lukeba, ambaye kitita chake cha kuweza kumchukua ni milioni 90 (Daily Briefing by Christian Falk - subscription required)
West Ham wamefufua nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David, 25, ambaye anapatikana kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Guardian)
Kipa wa Royal Antwerp Mbelgiji Senne Lammens, 22, amefurahishwa na uvumi unaomhusisha na kuhamia Manchester United msimu huu. (90min)
Manchester United wanaweza kuokoa mamilioni ikiwa watamnunua David na mchezaji wao wa zamani Angel Gomes, 24, kutoka Lille, kiungo wa kati wa Uingereza ambaye pia atakuwa mchezaji huru. (Manchester Evening News)
Manchester United pia wanafuatilia mpango wa kubadilishana wachezaji utakaomruhusu mchezaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, kujiunga na Bayern Munich na kiungo wa Ujerumani Aleksandar Pavlovic, 20, aelekee Old Trafford msimu huu wa joto. (CaughtOffside)
Bayern Munich wako tayari kuwauza wachezaji wawili wa Ujerumani, kiungo Leon Goretzka, 30, na mshambuliaji Serge Gnabry, 29, pamoja na winga Mfaransa Kingsley Coman, 28, msimu huu wa joto. Mshambuliaji wa Uhispania Bryan Zaragoza, 23, ni mwingine ambaye yuko njiani kuondoka, baada ya kukaa kwa mkopo Osasuna msimu huu. (Daily Briefing by Christian Falk - subscription required)
Newcastle hawana wasiwasi kuhusu kumpoteza mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, kwani hawaamini kuwa kuna klabu ambayo itafikia dau lao la £150m. (Teamtalk)
Newcastle pia wamefikia makubaliana na mlinda mlango wa Burnley Muingereza James Trafford, 22, kabla ya kuhamia St James' Park msimu wa joto. (Fabrizio Romano)
Beki wa kushoto wa AC Milan na Ufaransa Theo Hernandez, 27, anataka kujiunga na Real Madrid msimu wa joto, licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumtaka. (Fichajes - in Spanish)
Burnley wanataka dau la £30m kuruhusu Trafford kujiunga na Newcastle. (talksport)
Imefasiriwa na Asha Juma