Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 25.08.2024
Chelsea wanamchukulia mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 27, kama chaguo la gharama nafuu zaidi kuliko Victor Osimhen, 25, wa Napoli kutokana na matakwa ya mshahara ya mshambuliaji huyo wa Nigeria. (Sun)
Juventus wameomba Manchester United kulipa sehemu ya mshahara wa Jadon Sancho ili kusaidia kuwezesha uhamisho wa winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Arsenal watamlenga mshambuliaji mwingine watakapokamilisha dili la kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Merino, 28, kutoka Real Sociedad. (Mirror)
Uhamisho wa mkopo wa Armando Broja kutoka Chelsea kwenda Ipswich unakaribia kusambaratika baada ya uchunguzi wa kimatibabu wa mshambuliaji huyo wa Albania mwenye umri wa miaka 22 kufichua dalili za jeraha. (Sun)
Mshambulizi wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, ataondoka Chelsea ili kujiunga na Napoli kwa mkataba wa miaka mitatu. (Mirror)
Porto wamekamilisha usajili wa pauni milioni 12.7 wa mshambuliaji wa Uhispania Samu Omorodion, 20, kutoka Atletico Madrid - wiki chache tu baada ya pendekezo la uhamisho wa pauni milioni 33.9 kwenda Chelsea kusambaratika. (Athletic - subscription required)
Nottingham Forest wana nia ya kumsajili Arnaut Danjuma kutoka Villarreal, huku mshambuliaji huyo wa Uholanzi, 27, akipendelea uhamisho wa kudumu badala ya uhamisho wa mkopo. (Football Insider)
Wolves wako kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa timu ya Burnley mwenye umri wa miaka 19 na Luca Koleosho wa timu ya taifa ya Italia ya Chini ya miaka 21. (Express & Star)
Leicester City wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Morocco Bilal El Khannouss, huku Genk ikitaka angalau pauni milioni 17 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (HITC)
Kiungo wa kati wa Chelsea Tino Anjorin, 22, amekubali kwa mdomo kujiunga na Empoli inayoshiriki Ligi ya Serie A, huku mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza akihama kwa uhamisho wa bila malipo. (Fabrizio Romano)
Kipa wa Brazil Alisson, 31, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Liverpool baada ya kukataa ofa kutoka Saudi Arabia, lakini Reds wamemtambua mrithi wake wa muda mrefu, mlinda lango wa Georgia Giorgi Mamadashvili, 23. (Telegraph - subscription required)
Mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 24, atasubiri hadi mwisho wa msimu huu kabla ya kufanya uamuzi wa kuhamia Saudi Arabia. (ESPN)
Real Sociedad wako kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho ya kumsajili beki wa zamani wa Ujerumani Mats Hummels, 35, ambaye yuko kama mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita. (Athletic - subscription required)
Mshambulizi wa Everton Neal Maupay, 28, anafuatilia kwa karibu kurejea nchini kwao Ufaransa na klabu ya Nice ya Ligue 1. (Nice-Matin - in French)
Imetafsiriwa na Asha Juma